Hotuba ya Rais Samia; Mfumo wa hotuba za viongozi wetu ni ule wa 'kusadikika'

Hotuba ya Rais Samia; Mfumo wa hotuba za viongozi wetu ni ule wa 'kusadikika'

Sijali

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
2,672
Reaction score
1,814
Baada ya kuisikiliza hotuba ya rais wetu Samia Suluhu Hassan, naungana na wengine kuwa kwa ujumla ilikuwa nzuri, ya matumaini tuendako na ya usuluhishi wa kitaifa. Ni dhahiri kwamba rais asingeweza kusema yoooote yanayotaka kusemwa, lakini ameifanyia uadilifu fursa ya kuwepo pale.

Tatizo langu, kama la hotuba za viongozi wengine waliopita, bado mfumo wa hotuba za viongozi wetu ni ule wa 'kusadikika' . Ahadi za kufanya hili na lile na kwa ujumla kuleta 'feel good' kwa raia. Hii inafaa sana kwa raia wengi ambao wangependa kutiwa imani na matarajio. Lakini kwa wale wachache wanaoangalia mambo mapana zaidi na hata yanayohusisha dunia nzima....kuna 'kupwea'.

Kwa mfano, ahadi zilizotolewa, kama zote zikitekelezwa, zitahitaji zaidi ya dola bilioni 20 hivi kwa mahesabu ya haraka haraka, wakati GDP ya Tanzania bado ipo kwenye dola bilioni 63.7 . Dhahiri haiwezekani kutegemea mapato ya ndani kwa kutekeleza hata nusu ya ahadi hizo.

Ingesaidia sana pia kutufahamisha fedha za kukamilisha miradi hiyo zitatoka wapi? Na kama ni kukopa, miradi mingi ina sifa ya 'kijamii' na si kibiashara....pesa hizo zitarudishwa vipi? Maana kuna msemo "kula na kulipa' Tayari jirani zetu wanaanza kuonja joto ya jiwe kwa kukopakopa kiasi bei ya mafuta imepanda zaidi ya mara 1.5 ya Tanzania, kutokana na msukumo wa wadai!

Deni letu katika miaka hii limepanda sana hadi sasa limefikia dola bilioni 25 na linaongezeka. Nadhani raia inabidi tujue kwa vile ni sisi hasa tutakaolipa!

CAUTION: Mara hii Jamii ikizuia tena barua kutoka kwangu nitajua aina gani ya michango wanayoipenda wao!
 
Back
Top Bottom