Mkuu mwenzangu Chabruma; ukweli ni mchungu ila tukiujadili ulivyo kipindi cha kuonja uchungu kitapungua.
Kila wakati CCM ilipofanya uamuzi wa kuutetea muungano tulionao katika vikao vya chama na serikali huipendelea Zanzibar. Kwa mfano mdogo katika hotuba ya Mzee wetu Warioba, anaeleza serikali washirika zitakazoshikilia muungano, viongozi wake wawe na haki na hadhi sawa. Kwa mawazo ya kawaida tu wanahisa katika kampuni huwa na haki na hadhi sawa au hadhi na haki zao huendana na mchango (hisa) zao katika kampuni?
Mtu atadai au kupewaje haki na hadhi bila ya wajibu? Kuhusu namna ya kuchangia gharama za serikali ya muungano (hapa mzee wetu ameliachia Bunge). Ila lojiki tu inatosha kukuonesha namna itakavyoibidi Tanganyika kubeba pakubwa, halafu ati kiongozi wa serikali yake ni sawa na wa Zanzibar. Katika Umoja wa Mataifa (UN) penyewe, Wale wanaochangia pakubwa wana kura ya veto, na walitakalo ndilo hutendeka, sasa hapa mnaniaminisha kazi malipo yawe sawa kwa saa moja na saa nane?