omarilyas
JF-Expert Member
- Jan 24, 2007
- 2,130
- 150
(c) Hajakomaa kisiasa, mkomavu kisiasa kamwe hawasifii mafisadi kwa lolote. Fedha walizoiba mafisadi ni zaidi ya mazuri waliyofanya
Hitimisho: Hotuba hii ni chini ya kiwango na inanufaisha CCM kuliko Chadema. Inaonyesha woga wa Zitto dhidi ya CCM, imeshindwa kuonyesha malengo na mikakati ya Chadema kujipanua katika majimbo mengine, na kibaya zaidi inawashukuru mafisadi ambao hata CCM yenyewe haijawashukuru. Wapinzani tuna safari ndeeeeeeeeeefu.
Hivi kati ya Zitto na CCM nani anamhofia mwenzake?
Na hizi fikira mgando za kukomaa kisiasa nazo tumechoka nazo. Ukweli ni kuwa katika nchi inayoendeshwa chini ya mfumo fisadi kama nchi yetu kukomaa kisiasa kuna maana kuwa compromised kiasi cha kutosha kuonea haya uozo kwa manufaa ya mfumo.....na pia kuna maana ya kuwa tayari kufanya siasa zilipendwa zilizojaa fitina, uadui, majungu, rushwa na uchafu wa kila aina huku tukijidai tunapigania demokrasi na maendeleo...Zitto anatufunza kuwa kuna siasa mbadala wa hizi siasa hovyohovyo tulizoea na hayo ndiyo tunapaswa kuyaona kwa mwanasiasa kijana....
omarilyas