hahaha, zinaanza ofa za ajabu, mara ukimwamkia shikamoo haitikii halafu anakulembulia macho huku akikuita mwanangu, anajifanya anapendelea kile upendacho, kama haunywi pombe anajifanya na yeye anataka kujifunza kwako, kama mnafanya naye kazi, ofa, safari, favor kibao...akikuona umesimama na mdada yeyote hata kama mnafanya naye kazi, atawarukia na kuwaambia hamfanyi kazi (kama bosi wako), itafika kipindi mkiwa wawili tu ofisini, anakuja kukuambia tu kuwa anapenda kuwa karibu na wewe deshidechideshiiiii, mara umeumbika you are handsome, story zinabadilike zinakuwa za ngono tu akiwa anaongea na wewe, anapenda kukumiliki, unamwona usoni anakutaka laivu, hajiheshimu akiwa mbele yako kwa vile anavokaa, kwa vile anavyo kusalimia, kukushika au kukukumbatia (hug), anakwambia tu kuwa anakupenda lakini samahani usimwelewe vibaya....
dawa hapo, ni nduki, kama alivyofanya Yusufu, unamwachia na shati hapohapo...hhahaha.