House girl aliyemkata shingo mtoto wa mwajiri wake akamatwa na polisi

Analog

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2024
Posts
323
Reaction score
618
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemkamata Dada wa kazi za nyumbani (House Girl), Clemensia Cosmas Mirembe (19) aliyekuwa anatafutwa kwa kosa la kumjeruhi Mtoto wa Boss wake Maliki Hashimu (5) Mkazi wa Goba Jijini Dar es salaam ikidaiwa alimkata na kitu chenye ncha kali shingoni kilichotenganisha njia ya hewa chini ya sanduku la sauti na kumsababishia kushindwa kupumua, kuongea, kupata maumivu na kupoteza damu nyingi sana.Akiongea leo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema ——— >

“Baada ya tukio Mtuhumiwa alikimbia, upelelezi wa tukio hilo la kikatili ulianza mara moja na July 21, 2024 saa 4:00 usiku Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata Mtuhumiwa huyo akiwa amejificha kwenye jumba bovu maeneo ya Goba Kizudi Kinondoni

Mtuhumiwa huyo anahojiwa kwa kina na atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo kwa hatua zaidi za kisheria, nitoe wito na kuwawashauri Wazazi, Walezi, Walimu na Jamii kwa ujumla kuwafundisha Watoto kujenga tabia ya kutembea katika makundi lakini pia Watoto wasikubali kuwa karibu na Watu wasiowafahamu, Watoto wasitumwe maeneo ambayo kwa mazingira ni hatarishi ikiwa ni pamoja na kuacha kuwatuma Watoto wadogo maeneo mbalimbali nyakati za usiku”Mtoto huyo alijeruhiwa July 15,2024 majira ya saa 12 jioni eneo la Goba Kinzudi, Kinondoni ambapo alipelekwa Hospitali ya Mloganzila na baadaye alihamishiwa Hospitali yaTaifa ya Muhimbili anapoendelea kupatiwa matibabu mpaka sasa, Polisi iliahidi kuwa Mtuhumiwa lazima akamatwe na leo imetangaza kufanikisha hilo.

PIA SOMA
- Anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa kumchinja mtoto wa mwajiri wake
View attachment 3049507
 
Sasa hiii inahusiana nn na tukio hili amabalo mtoto kafanyiwa ubaya na mfanyakazi wa ndani?
pengine ni kama tahadhari tu maana matukio ni mengi yanayoshaabiana na ayo
 
Usikute alikuwa anateswa sana na muajiri wake .
 
Mbona matukio hivi
 
Alafu neno kuchinjwa limetumikaje apo ilihali mtoto hakufa.
waseme tu alimjeruhi shingoni maana kuchinjwa Shingo inatakiwa iwe imekatika unaponaje sasa
 
kuwawashauri Wazazi, Walezi, Walimu na Jamii kwa ujumla "kuwafundisha Watoto kujenga tabia ya kutembea katika makundi lakini pia Watoto wasikubali kuwa karibu na Watu wasiowafahamu"! Sidhani kama ushauri huu unahusiana na tukio, kwani mtoto na mtuhumiwa walikuwa wakiishi nyumba moja kama mtoto na dada yake. Ninajiuliza endapo ingekuwa mume au mke amemkata koromeo mwenzi wake sijui angetutaka tujihadhali kuishi na watu! Kwani hata ndugu huuana.
 
Mimi na suspect kwamba kulikuwa na kijiugonvi kisu kikafika bahati mbaya shingoni. Damu ilipoonekana hosgerl akakimbia. Alafu ikazushwa taarifa nzito mtoto amechinjwa na dada wa kazi. Kumbe ni kujeruhiana tu. Watu hawajua maana ya kuchinja
 
Jana mmoja kaiba tv.
Yaani kaletwa juzi Jana kalianzisha.
Na katoka mkoa.
Kwa broo mmoja katoka bush na mimba changa amekuja na maelekezo atakayejichanganya tu mpe mzigo fasta ,
Bahati nzuri tukamgundua mapema na ndio kutupa kisa chote kwamba aliyempa mimba ni mchunga mbuzi huko kwao kijijini kwa hiyo wakapanga aje mjini ampe mtu mimba

Hawa wadada wa kazi hawa wanatumika na shetan sana nao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…