House girl ataka kutorosha mtoto ili kulipa kisasi kwa mwajiri wake

House girl ataka kutorosha mtoto ili kulipa kisasi kwa mwajiri wake

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limeanza uchunguzi wa tukio la mtoto ambaye jina lake limehifadhiwa (10) anayedaiwa kukamatwa na wasamaria wema katika stendi ya mabasi ya Nyegezi jijini Mwanza katika harakati za kutoroka na mtoto wa mwajiri wake kwenda mkoani Mbeya.

Taarifa ya mtoto huyo ilisambaa kuanzia jana Jumatano Februari Mosi mwaka huu katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha binti huyo akihojiwa na mwanamke ambapo alinukuriwa akijibu kuwa kichanga hicho ambacho ni cha mwajiri wake.

Akizungumza leo na Mwananchi Digital Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema katika mahojiano binti huyo alidai kusafirishwa kutoka kwa wazazi wake mkoani Mbeya na mwalimu wa Shule ya Msingi Ilendeja iliyoko Kisesa wilayani Magu mkoani hapa kwa lengo kuja kumsaidia kazi huku kukiwa na ahadi ya kumsomesha jambo ambalo halikufanyika.

"Februari Mosi mwaka huu aliamua kutoroka na mtoto huyo kwa lengo la kwenda Mbeya kwa sababu alikuwa amechoka kukaa na yule mwalimu ambaye anamtuhumu kwamba alikuwa akimfanyia vitendo vya ukatili kwa kumchapa mara kwa mara," amesema Mutafungwa

Mutafungwa amesema jeshi hilo pia lilikutana na mwalimu huyo, Diana Mwaihoji ambaye alikiri kuwa kichanga hicho ni chake huku akikiri kuwa binti huyo alikuwa hausigeli wake ambaye alimtoa mkoani Mbeya kwa ajili ya kumsaidia kazi za ndani.

"Tunashirikiana na wenzetu (Polisi) wa mkoa wa Mbeya ili kufika katika familia ya binti huyu kufahamu ilikuwaje wakamruhusu binti huyo kuja kufanya kazi mkoani Mwanza ilihali ni mwanafunzi,"

"Baada ya kumaliza mahojiano na mwalimu huyo ambaye alikiri kuishi na binti huyo kama mfanyakazi wake, tulimkabidhi mtoto wake lakini tunaendelea na upelelezi kwa hatua zaidi za kisheria," amesema Mutafungwa.

MWANANCHI
 
Watu huonesha upendo wakiwa makanisani, harusini na sehemu nyinginezo zenye mkusanyiko wa watu.

Lakini fika majumbani mwao sasa, ni mashetani kasoro mikia!

Kwa hiyo huyo mwalimu tena msimamizi wa sera za: "elimu kwa wote bila malipo", aliwezaje kuwarubuni wazazi wa huyo mtoto na kuja kumfanyisha utumwa kwake?

Yeye angelikubali watoto zake wakafanye kazi za ndani kwa watu?

Na kwa nini Polisi wasianze naye wakamwachilia?

Hovyo kabisa.
 
mpwayungu village njoo uone maadui zako huku.

Tukiwa serious, ulinzi wa mtoto ni wajibu wa kila raia mwema. Na hii tabia ya child labour ni unyonyaji mtoto wa miaka 10 anakuwaje house maid. Yeye mwenyewe mtoto mwishowe achome nyumba
 
Nae achukuliwe hatua kwa kufanyisha kazi mtoto
 
Hawa ma house girl wa hivi wamesababisha kuanzishwa kwa kasi vituo vya kulea wato day care ili wazazi wenye shughuli wapeleke watoto kulelewa huko kwa malipo. Maana mabinti wa kazi za nyumbani siku hizi hawaaminiki kulea watoto watawafanyia visa vya ajabu wasipolipwa haki zao.
 
WAFANYAKAZI WA NYUMBANI MTIHANI KWELI KWELI.
jenga urafiki nao na muone kama ndugu yako.utakaa naye mpaka utapokea posa kwa ajili ya wazazi wake.
 
"Tunashirikiana na wenzetu (Polisi) wa mkoa wa Mbeya ili kufika katika familia ya binti huyu kufahamu ilikuwaje wakamruhusu binti huyo kuja kufanya kazi mkoani Mwanza ilihali ni mwanafunzi,"
Mwalimu anamtorosha mwanafunzi na kumfanya house girl!!! Tanzania yangu uzalendo uko wapi!!!?
 
Kuajiri mtoto wa miaka 10 sio akili kabisa,sasa anawezaje kumlea mtoto mwenzie kama sio kumletea matatizo tu
 
Back
Top Bottom