House girl wangu anataka likizo na marupurupu!

Simba Mkali

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2012
Posts
620
Reaction score
239
Sijui kama ni sawa au si sawa, msaidizi wangu wa kazi ameniambia kuwa anataka likizo ili aende kwao, hilo kwa roho za kibinaadamu naona ni jambo zuri sana, lakini anataka na mshahara wa mwezi mmoja, nauli na fedha za matumizi ya njiani. Kama vile haitoshi anasema kuwa anapaswa kulipwa fedha za nauli za jamaa yake ambaye amepanga kwenda kumtambulisha huko kijijini kwao, hebu niambieni kuna haki hapa?
 

Mzee, mbona hiyo kawaida... kwani wewe ukienda likizo si unapewa hela ya likizo ya kusafirisha wewe na familia ya watoto wanne mpaka kijiji ulichotoka. Tatizo liko wapi hapo ndugu? Kwani mshahara wake wewe unamlipa kiasi gani mpaka uone tabu kumpa hiyo hela ya mwezi mmoja, au unaona atatoroka? kama ni hivyo mpe hiyo hela ila mwambie akutumie mwenzie mwingine kama yeye hatarudi. Hii ni kwakuwa ulisha amua kumruhusu. Au vipi kamanda?
 
aisee hii imekula kwako...huyo ndio anaondoka harudi tena..Asilimia 98 ya ma housegirl wakisema wanaenda kwao ujue ndio kimoja hawarudi....huyo ashapata kazi sehemu nyingine au ndio anaenda kuanzisha biashara huko kwao...we mpe aende lakini anza kutafuta h/girl mwingine
 
hakuna tatizo.fanya kiubinaadamu.mimi house girl ambae anaishi na mama,kila akisafiri kwenda kwao,huwa namlipa hela,za mwezi mzima na huo haufanyii kazi,akirudi mshahara wake unaendelea kama kawaida.huwa namlipa kila baada ya miezi minne kwa mkupuo,ili hela zake afanyie la maana
 

Unahitaji house boy? niko tayari.....:help::help:
 
Mkuu kama tena anaenda kumtambulisha mwenzi huyo ni mstaarabu sana. Mwingine angeshaona na yeye anakaribia kuanza maisha yake angekupiga bao then akatambaa na mtarajiwa wake. Amekuonyesha ustaarabu na wewe mpatie hamasa. Lakini zaidi ya hapo, hawa watu ni wa muhimu sana kwasababu wanafanya shughuli zinazobeba uhai wetu. Thamini mchango wake katika maendeleo yako na familia yako. Muongeze na zaidi ya anachokitaka um-delight!
 
Kwanza kwenda likizo ni haki ya mfanyakazi hata kama mwajiri ana roho ya binadamu au ya mnyama! Pili naona kwamba mfanyakazi wako hajashtuka vizuri maana angedai pamoja na overtime, nahisi anafanya kazi zaidi ya masaa 45 kwa wiki. Mpe haki yake ili nawe upate yako.
 
Mpe tu nae ni binadamu au unataka awe anajilipa
 
Kweli kabisa lakini kazini miye nikienda likizo nalipwa mshahara wa mwezi mmoja tu, hakuna marupurupu wala nini,si unajua tena haya makampuni yetu ya watu binafsi.
 
huyo 'jamaa ' yake hana aibu dume zima?
Likizo ni haki yake,
kumpa mshahara nayo si tatizo.....(ingawa private sector hakuna hii, ila naweza kumpa)
Kumpa nauli ya kwenda na kurudi nayo si tatizo

ila nauli ya huyo mwanaume wake asahau..........
Fedha za matumizi njiani simpi maana nishampa mshahara.....hataki anaacha
 
usisahau kumfungia kitenge na tshirt kama zawadi kwa wazazi wake...
 
kaaaaaaaaaaaaazi kweli kweli
ndo mambo ya ajira mama
 
mpe mshahara wa mwezi mmoja yeye ndo ajue atafanyaje,lakini angalia na pesa yenyewe isije ikawa anaenda kigoma we unampa 20000/=, akirudi mshahara wake utabaki pale pale mkuu...
 
kumpa Mshahara wa mwezi mmoja haijakaa sawa. labda kama siku hiyo anayondoka kwenda likizo ndiyo siku anayopokea mshara wake. Ila nauli na posho ya safari sawa ni haki yake. Pia kwa mwezi atakaokuwa likizo lazima alipwe mshahara wake. utaribu ni ule ule kama wewe unavyovuta huo mkwanja wakati ukienda likizo.
 
Mkuu fanya ubinadamu,kwanza inaonekana mmeishi vizuri pia mpaka wakati huu nawe umeridhia aende. Nivema kama mfuko unaruhusu ukampa atakacho lakini inakubana mpe kiasi,halafu umweleweshe kuwa uwezo ni mdogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…