Simba Mkali
JF-Expert Member
- Jan 31, 2012
- 620
- 239
Sijui kama ni sawa au si sawa, msaidizi wangu wa kazi ameniambia kuwa anataka likizo ili aende kwao, hilo kwa roho za kibinaadamu naona ni jambo zuri sana, lakini anataka na mshahara wa mwezi mmoja, nauli na fedha za matumizi ya njiani. Kama vile haitoshi anasema kuwa anapaswa kulipwa fedha za nauli za jamaa yake ambaye amepanga kwenda kumtambulisha huko kijijini kwao, hebu niambieni kuna haki hapa?