Houseboy achomwa kisu na bosi wake baada ya kufumaniwa na mke

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532


Maisha ya kibarua mmoja (house boy) katika Kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya yako hatarini baada ya kuchomwa kisu na mwanaume ambaye alimkuta kitandani na mkewe.

Inadaiwa kuwa mume huyo alikuwa ameondoka nyumbani kuelekea kazini Jumatatu asubuhi, lakini akagundua alikuwa amesahau kitambulisho.

Hata hivyo, aliporejea nyumbani alishangaa kumkuta mfanyakazi huyo kitandani na mkewe, ndipo akapandwa na hasira na kuchukua kisu, akamdunga mikononi na sehemu nyingine za mwili, akimsababishia majeraha tele mwilini.

Mshukiwa alipiga mayowe akitafuta msaadaa, mayowe yake yaliwashtua wakazi wengi ambao walimwokoa na kumkimbiza katika hospitali ya binafsi ya White Rose, ambapo bado anatibiwa baada ya kushonwa majeraha.

Mume husika alikamatwa na polisi wa utawala eneo hilo na bado anazuiliwa akihojiwa, wakazi wakisema alikuwa karibu kumuua mfanyakazi huyo.
 
angeua hata nisingeshangaa jamani, kula ale, mshahara apate, fedhea amletee bosi wekeeee? upumbavu uloje
 
Mshahara umlipe na mke ajisevie! Kinachofuata ni kujimilikisha nyumba kabisa...
... na mali yako yote. Kisha wakuajiri kama house boy. Alafu ndio uwe unasikia kilio kwa mbaaali, cha mke wako 'akitumbuliwa jipu'. [emoji1] Boss, tufanye collabo tuandike script ya movie moja babkubwa ya Nollywood. [emoji38]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…