How he built a billion dollar business in Tanzania

Baada ya kusoma comments za wadau nimegundua kuwa somo lililotolewa kwenye hii article halijaeleweka kwa wengi. Hii article inazungumzia pesa. Kwahiyo mjadala wake inabidi ubase zaidi kwenye pesa.

Mo alianza na 1 mil. USD. Sasa hivi annual revenue zao zinakadiriwa around USD 1.1 bil. na wanasema wameajiri watu 24,000. Hii maana yake ni kwamba on average kila mwajiriwa mmoja anaingiza annual revenue ya 45,800 USD ambayo ni sawa na milioni 73. Average salary ya mfanyazi mmoja ikiwa sh. laki 6 (This is an over estimation though) atalipwa sh. mil 7.2 kwa mwaka.

Hapo maana yake ni kwamba mfanyakazi mmoja ameleta revenue ya sh. mil 65.8, ambayo ni sawa na mil. 5.4 kwa mwezi au 180,000 kwa siku. Get this right fellas - on average every day kila mfanyakazi wa Dewji anamuingizia sh. 180,000.

Narudia. Mo alianza na 1 mil. USD ambayo ni sawa na bil. 1.6 TZS. Kwahiyo iwapo vijana 10 wenye mawazo mazuri ya biashara watachanga sh. mil 16 kila mmoja, watapata mil. 160 ambazo ni 10% ya mtajia alioanza nao Mo. Miaka 15 later watu hao wanaweza kuongeza revenues zao 1000 fold (kama alivyofanya Mo) na kuwa na revenue za shilingi bilioni 160!

Mo baba yake alikuwa tajiri akamkopesa bilioni. Wewe kama baba yako sio tajiri usikae chini na kutoa machozi au kujifariji kwa kumsema vibaya Mo. Be creative, shirikiana na mwenzako ambaye baba yake sio tajiri ili mpate mtaji wa kuweza kuingia sokoni. Hii ni dunia ya ushindani - huwezi kushinda kwa maneno matupu ya wivu...
 
Jamani kama ni wezi, mbona Watanzania ni wezi namba moja halafu tunaishia kuhonga mademu magari? Mimi naamini katika kufanya kazi kwa bidii na mipango na malengo. kama huna malengo na mipango, kila mwisho wa mwezi unashinda baa mpaka mshahara unaisha in one week, sahau maendeleo. Tutabaki kulalamika kila siku watu wanafanya mambo.
 
Waswahili sisi ni kazi sana kufikia level hizi..kwanza kabisa wengi wetu tunathamini sana kuajiriwa which inturns makes us slaves en workin class, pili hatuna umoja personally naonaga tu wahindi au waarabu wako na umoja na wanafanya kazi in families lakini sisi ukisema umshirikisue kaka ako either atakufilisi au atataka kukuzulumu au kuwazulumu wanao..ila inabidi tufahamu kwamba wahindi wengi au waarabu waliuza unga sana kipindi cha mzee ruksa..ndo mana wakatengeneza hizo start up capitals mpaka huyu jamaa ameomba $1 million si mchezo..zetu sisi waswahili ni kuona fahari mtu kufanya kazi TRA, BOT, EWURA etc na kulipwa milioni kadhaa ambazo baada ya miaka kadhaa utastaafu nila kuwaaachia wanaolegacy yoyote ile ya kuiendeleza..over..!!
 
Behind any successful story....!!!!!

Biashara especially za level hiyo ni zaid ya story za forbes.,achana na recorded stories; kwa walio karibu na wafanyabiashara wakubwa mtashuhudia haya maneno yangu!!!!!
 
hate it or luv it,its so inspiring,tukibadili mfumo wa elimu yetu,mitahala ianze kuandaa enterpreneurs na sio employee,tz ni miongoni mwa nchi chache dunia ambazo kuna fursa za kufa mtu,enterpreneurs ndio watatawala dunia,pamoja na kuwa familia imembeba lkn pia elimu aliyoipata Mo abroad ilimuandaa vizuri kuwa succesful enterprenuer,by the way tuliopo humu humu na elimu yetu hii hii inawezekana tukatoboa hata km hatuna background nzur ya kifedha,ujasiriamali na utajiri unachangiwa na ubunifu,fursa,wazo,kujiamini na kusimamia maamuzi.
 

chasaka 🙂
 
Hongera sana Mo! kusema kweli, ni story nzuri ambayo inatia moyo. kuchangamkia fursa ni kitu cha muhimu sana katika maisha, na kwa story hii naona wewe ni mfano mmojawapo wa kuigwa. vijana wa tz tunatakiwa kuchangamkia fursa na kuzitafuta popote pale zilipo na zinapotokea, mwenzetu alichangamkia pamoja na mambo mengine, fursa za wakati wa privatization. kitu kingine ambacho nimekipenda sana ni kwamba, wakati baba yake kwa kipindi yeye yupo wallstreet, baba yake kusema kweli sio kwamba alikuwa masikini, kwa maandishi hapo juu ni kwamba alikuwa na billions of shillings, lakini hata hivyo yeye hakubweteka kukaa nyumbani ili ale mabilioni ya baba yake kama watoto wengine wa matajiri wanavyofanya, hakuvuta mibangi na unga kama watoto wengine wa vigogo/matajiri wanavyofanya, aliamua kujitegemea akaanza kufanya kazi ya kipato kidogo marekani, napenda ninavyoona baba yake aliamua kumweka kwenye mazingira ya kujitegemea asimtegemee baba yake, akakataa hata kumtumia hela marekani, na kusema dogo njoo huuku home tz uchangamkie fursa..., aliporudi, utakuta dingi yake hakumwacha abweteke, mo alikopa pesa (sio kupewa bure), ambazo ilibidi afanye kazi hadi aje azirudishe deni kwa baba yake....hii ni mfano mzuri, ukiwa na watoto hata kama wewe unao uwezo, lazima uwaweke kwenye mazingira ya kujitegemea kama huyu mzee alivyofanya, sio kuwalisha tu. hongera sana bro.
 
Baada ya kutoka US ame amplify production na productivity ya kampuni za familia na kutengeneza 3% ya GDP ya TZ na siyo revenue ya Tanzania. Kampuni za namna hiyo nyerere alizitengeneza kama mashirika ya umma na kuajiri wakurugenzi wenye elimu na vipaji labda sawa au zaidi ya Bw. Mo. Ikikumbukwa kwamba yalikuwepo zaidi ya 200 infact the largest number in south of sahara, halafu hata kama robo yake tu 50 enterprises zingeongozwa na wenye uaminifu kama mo kwa baba yake, yange generate equivalent ya 150% ya GDP ya sasa na of course GDP yenyewe ingekuwa kubwa zaidi kwa kuwa sekta nyingine zingekuwa kubwa zaidi. GDP ingekuwa kubwa kwa EAC yote combined. Fundisho kuwa indeed state owned enterprises zilihitaji reforms kitu ambacho tuliharibu na just kuziuza kwa hasara lakini cha maana zaidi, ufisadi na mbaya zaidi mafisadi wasio na vision ndiyo wameletea sekta ya uzalishaji imefifia kwa kuwa hata waliofilisi mashirika hawakuwa focused on enterpreneural growth but rather on starehe and ulimbukeni mwingine. Hiyo ndiyo shida kubwa yetu kama nchi na hata race watu weusi. Ni lazima tujifunze na tujirudi.
 

Wewe ndio hopeless coz unaamini wahindi kwa wizi wao Uliza ushahidi tuu utajua wizi wao wa kutoa mtaji wa dola 26ml hewani wewe kaa kimya kama hujui
 
Wewe ndio hopeless coz unaamini wahindi kwa wizi wao Uliza ushahidi tuu utajua wizi wao wa kutoa mtaji wa dola 26ml hewani wewe kaa kimya kama hujui
Hongera wewe ni mwenye miakili lakini next time watch the movement of your fingers while typing.....ni ushauri tu coz' usizani watu hatufahamu hizo lugha za hovyo hovyo!
 
Mijitu roho mbaya tu humu, mnaona wenzenu wanaziona fursa na kuzitumia nyie mmelala, mnabaki,sijui pembe za tembo, sijui wizi.

Fanyeni kweli, fursa zimejaa Tanzania.
Sina macho nini mana sizioni hizo fursa....please show me mzee wa system at work.
 

Haaaahaaa....we acha tu. Nilichoka sana yule mzee wa diamond motor alipofariki akaandikwa kwenye magazeti likiwemo Daily News juu ya jinsi alivyokuwa mfanyabiashara hodari. Biashara inachanganywa na mambo mengine ili iwahi kutengeneza mamilioni.
 
amasema vema "ni rahisi kutengeneza fedha toka kwa pesa kuliko kuzitengeneza kutoka sifuri." Sie tuliotoka kimanzi na kiraracha, tukasoma St. Kanumba na kuishia kariakoo kubeba magunia tunapaswa kuwa kama Mo senior tuwaandalie wanetu $1 mil. za kuwakopesha. Inawezekana tukiacha visingizio.
 
amasema vema "ni rahisi kutengeneza fedha toka kwa pesa kuliko kuzitengeneza kutoka sifuri." Sie tuliotoka kimanzi na kiraracha, tukasoma St. Kanumba na kuishia kariakoo kubeba magunia tunapaswa kuwa kama Mo senior tuwaandalie wanetu $1 mil. za kuwakopesha. Inawezekana tukiacha visingizio.
 

acha magumashi,,patrick ngowi kasoma wapi??
 

acha magumashi,,patrick ngowi kasoma wapi,,baba yake ghulam kasoma wapi because he says his father is smarter than him,,ondoa inferiority complex
 
Mo hana lolote,angekuja na mtaji+ideal. ding ndo hiro aliweza kumsomesha, kupata mtaji,aliona fulsa akamrudisha hom.
 

Jamaa kumbe is very smart
 
hofu yangu ni cc watoto wa wakulima coming frm families having no political & business background/tuliopitia kayumba primary schools,tutafikia level za MO..?.

kila kitu kinawezekana mkuu if u'll believe in it and then ukaamua kutake action don't ask urself WHY? But ask urself HOW?
 
I love the story though watu wengi inaonekana wamekata tamaa baada ya jamaa kusema kuwa alikopeshwa 1 million Us dollar na baba yake so wao wanaamim hawezi kufanikiwa kwasababu tu ya background ya wazaz wao (kwamba hawana pesa na ni wakulima). Cha msingi inabidi tuelewe kuwa "we can't path the same way" ndugu zangu sio kweli kwamba matajiri wote wakubwa wamepita katika njia zinazofanana hapana haipo hivyo ndugu zangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…