How I Met My Wife

Ahsante sana KigaKoyo kwa simulizi inayosisimua.

Ahsante tena kwa muda wako maana kuandika nako kunachukuwa muda wa kutosha.

Shukrani nyingine pia ziwaendee waliofuatilia uzi huu na watakao endelea kufuatilia, wale wote wa kimya kimya na ambao wamejitokeza kueleza hisia zao ama chchote kile.

Niliona ni vyema kuitenga simulizi hii kwa kuanzisha uzi huu ili wasomaji waifuatilie kwa urahisi.

Nitoe rai, kwamba, yeyote mwenye simulizi ya jinsi alivyompata mwenza wake, ambayo anadhani ina mafunzo ama kusisimua basi asisite kuileta hapa.

Simulizi kama hizi husaidia sana baadhi ya watu walio 'grounded' kwa lockdown ama karantini kutokana na sababu zozote zile, husaidia wale ambao hawapendi kushika volume kubwa ya kitabu na kuanza kusoma ukurasa kwa ukurasa, husaidia pia wadau ambao hawapendi kusoma kabisa lakini kutokana na simulizi hizi ama vitabu tajwa katika simulizi, huamua kutafuta na kuanza kusoma hatimaye kujenga tabia ya kujisomea.

Karibuni sana.
____

CC
KigaKoyo

James Jason
 
Asante kwako pia nadhani umemuibua kiga na wengine watakafuata baada ya kuleta stori yako tamuu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je ipo haja ya kuanzisha uzi mwengne au tunaendeleza hapa hapa? Kwa wale wenye story ya jinsi tulivyokutana na wenza wetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salute boss.
 
Shukrani mzee wangu. Kama ulivyosema story hizi zinasaidia sana kujenga au kudumisha tabia ya kujisomea.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji87]am speechless broo
[emoji1538] sidhani nyakuja kutana na kisa kama hiki kwakweli

Ahsante kwa uwepo wako hapa jf
 
1st Of Nzi Chuma

Nami nimetamani sana kushare "how I met my wife" baada ya kuisoma hii ya Kiga, imenisisimua sana. Kama ilivyokua hiyo, utamu unaweza kuchelewa kukolea kidogo, lakini mdogo mdogo tutafika.

Tuanzie mwaka 2007 ambapo niliripoti advance shule moja Kilimanjaro kwenda kusoma PCM baada ya kukamilisha masomo yangu ya Olevel kule Tanga. Kutokana na ucheshi nilionao, uongeaji wangu na ubishi wangu, wengi wa wanafunzi wenzangu waliniambia nimekosea sana kuja kusoma PCM, nilitakiwa kusoma masomo ya arts ambayo wao waliamini yangenitoa zaidi. Upande wangu mimi kilichonivutia kusoma PCM ni kwa sababu naipenda sana hesabu, sana tena na ndo ambayo baadae niliifanyia degree yake na ndo inayoniweka mjini kwa sasa. Mwaka 2008 waliripoti form 5 wapya sisi tukawa rasmi ni kaka sasa maana shule yetu haikuwa na Olevel. Madogo wa form 5 wakanizoea sana haswa wa bwenini kwangu na walipenda sana ucheshi wangu na jinsi ninavyopiga nao story. Siku moja ukazuka ubishi mzito baada ya kuwaambia madogo kuwa mimi ninao uwezo wa kumtongoza demu yeyote kupitia simu ambaye nitapewa namba yake. Wengi walibisha wakidai kwamba haiwezekani, kama vipi nipewe namba. Sote tunajua kuwa simu haziruhusiwi shuleni lakini wakorofi walikuwa nazo na ukizingatia ni shule ya boys tupu tena advance only, hakuna mwalimu alijali sana. Basi kijana mmoja kwa jina la Mzamil yeye akatoa namba akidai kwamba huyu dada yeye alikosea namba na kumpigia. Kwahy akataka nimpigie huyo demu na kumuweka loudspeaker ili bweni zima wasikie ninavyosaundisha, nikapewa na simu ambayo ina salio la kutosha kwa ajili ya kazi hiyo. Nikaipiga ile namba ambayo nakumbuka ilikuwa ikiishia na 999 ikaita sanaa lakini haikupokelewa (kumbuka ulikua ni usiku wa saa 4), bila shaka huyu dada atakuwa alikua amelala. Basi wale jamaa wakaona hiyo sio shida, nipewe namba nyingine ya dada ambaye anaitwa Sophy. Huyu Sophy alikuwa na ukaribu na huyu mtoa namba huko kwao Morogoro, jamaa alidai kuwa ni mtoto wa mjombaake. Nikampigia Sophy na kwa bahati nzuri akapokea.. Haloo.. Hellow Sophy... Nani mwenzangu..? .. Nzi Chuma hapa.. Nambie Nzi Chuma... Nikamwambia mimi nahitaji urafiki mwema na ww dadaangu... Urafiki gani hatujuani...?? Jamaa wakacheka bweni zima baada ya mimi kujibiwa hivyo kitu kilichomfanya Sophy ashtuke na kukata simu. Wengi walinikejeli kwamba sina jipya na wengine waliniambia unaweza. Basi mimi nikaomba namba zote mbili, ile ya Nai inayoishia 999 na ya Sophy nikasave kwenye simu yangu kisha nikajipumzisha.
Wakati nautafuta usingizi, simu ile ya kwanza ambayo niliitumia kupiga namba za Nai ikawa inaita, jamaa mwenye simu alipoona ni Nai ndo mpigaji akaniletea hadi kitandani kwangu, mimi nikashuka na kwenda kuongea nae nyuma ya bweni. Licha ya kuwa Nai hakuwa ananifahamu, lakini alionyesha anapenda sana urafiki, akafurahia maongezi yetu ambayo niliongea nae kwa zaidi ya saa nzima. Kabla ya kukata simu nikamwambia kuwa hii sio namba yangu, simu yangu ilizima tu chaji ndo maana nkatumia namba ile kumtafta, hivyo nitamtext kwenye namba yangu na tutaitumia hiyo namba kuwasiliana. Uzuri wa Nai alikuwa muelewa saaana, alinielewa bila ubishi. Kesho yake tena, Sophy akapiga kwenye ile namba, jamaa akaniletea simu, nikaongea na Sophy ambaye alinieleza vitu vingi sana kuhusu yeye, ikiwemo suala la jana usiku ambapo alikuwa amelewa halafu mimi nikawa namzingua. Nikahisi hapa kwa Sophy nimepotea njia, mimi na pombe wapi na wapi? Sikuwahi kujaribu wala kukaa sehemu wanapokunywa na wakati huo ndo kwanzaa nipo form six basi mtu akitaja mambo ya Pombe sijui nilikuwa namuona vipi..
Siku zikawa zinaenda, sikuacha kuwasiliana na yeyote kati ya Nai wala Sophy, tulichat sana, kuongea sana na simu usiku.. Kuna kipindi ilikuwa inabidi nitumie uongo ili niweze kuongea nao wote wawili. Naweza nikaongea na mmoja kisha nikamwambia ngoja nikasome kwanza kisha nikampigia mwengine. Nai yeye alikuwa mwanamke wa mfano wake (na nikiri kuwa sijawahi kukutana na mwanamke wa sampuli hii maishani mwangu), yeye ukimwambia "wait nitakupigia" hatosumbua mpaka umpigie. Yaani ni mwanamke flan ambaye nahisi amelelewa katika mazingira flan ya kustaajabisha au amejiongeza tu. Kipindi hiki ambacho mimi nipo form six, wote Nai na Sophy walikuwa wapo mtaani tu baada ya kumaliza form 4. Nadhani tulimalza nao form 4 lakn matokeo yao hayakuwa mazuri kuendelea na advance. Sophy yeye alikuw ni mtoto wa mwalimu na Nai alikuwa mtoto wa kigogo flaniz wote Sophy na Nai waliishi Moro.
Siku hazigandi, nikamaliza form six nikarudi nyumbani Tanga, nikaenda shule niliyosoma Olevel kuomba part time (kipindi kile shule zilikuwa na uwezo wa kuajiri) nikapewa part time nikawa nafundisha Physcs & Maths kwa malipo ya sh 150k kwa mwezi mmoja, nikaona sio mbaya nikaendelea kupiga piga hapa kwa sababu kutokea February nimemalza form six mpaka October kwenda chuo ni muda mrefu sana. Nikafundisha pale kwa mwezi mmoja na kupewa cheque yangu ya 150k, kwakuwa mawasiliano yangu na Nai pamoja na Sophy yalikuwa yanaendelea kama kawaida, nikaona sasa ni muda muafaka wa mimi kwenda Moro kuonana na kufahamiana na watu wote hawa wawili. Nikachomoka Ijumaa ya wiki ile jioni kama saa 10 nikapanda basi na kwenda moja kwa moja mpaka Dar, nakumbuka nilifika dar yapata saa 4:30 usiku.. Moja kwa moja hadi Tandale ambapo nilienda kwa dada yangu na kulala hapo ili safari ianze asubuhi ya kuelekea Morogoro.

Wazee nimeona nianze kidooogoo.. Leo sina nguvu sana, ila kuanzia kesho itaendele kwa urefu sanaa..

Tuwe pamoja mpaka tuone nilipataje mke wangu, msichoke kufuatilia wala msikate tamaa mapema, naamini kuna mengi sana ya kujifunza katika story hii...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naamini leo usiku sana ntapata muda wa kuiendeleza, ngoja kwanza nimbembeleze wife alale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…