FL1,
Ni vibaya sana kuwatuhumu wanaume, kwani kila kitendo cha Mwanaume ku-womanize huendana na Mwanaume (Mtenda) na Mwanamke (Mtendewa) - ikiwa hivyo ndo sahihi. Huyo mwanaume anayewominize na mwanamke anayekuwa womanized wote ni wahusika. Kinachofanya tendo hilo lionekane linatendwa zaidi na wanaume tu ni hiki hapa:
Wanaume wako tayali ku-admit kuwa wanafanya hivyo kwani mila na desturi zinawafanya wanaume waone kufanya hivyo ni kama ushujaa fulani. In fact wanaume wengi wanapenda wajulikane kuwa wana wanawake wengi (wengine hata kujisingizia) - aitwe KIDUME. Wanawake wanapokuwa womanized hu-keep low profile kwa sababu kwao ikijulikana ni soo katika jamii (Waume zao wanaweza hata kuwaua au kuwaacha, wanapoteza heshima mbele ya jamii, n.k.). Mwanamke akiwa katika ndoa ata-admit kuwa mumewe ni womanizer na Mashoga zake watajua, familia yake watajua, n.k. Lakini Mume akijua kuwa mke wake anakuwa wominized na mwanaume mwingine ata-keep low profile (sana sana ugomvi na soo lake litakuwa ndani). Kwake ni aibu kubwa kwa marafiki zake, ndugu, au yeyote anayemhusu kujua kuwa mke wake anakuwa womanized na mwanaume mwingine.
Kutokana na hayo, nje nje inaonekana wanaume ni womanizers na wanawake hawafanyi. Lakini ukweli ni kuwa kwa kila mwanaume womanizer, kuna Mwanamke womanized! uwiano ni 1:1. Fanya utafiti kwenye jamii utayaona wazi wazi. Tena mie kwa tafiti zangu zisizo rasmi, wanawake womanized ni wengi zaidi. Sababu yake ni kuwa Mwanaume mmoja anaweza akawa ana-womanize wanawake kadhaa mtaani. Akajulikana sana yule mwanaume, lakini wake za watu anaowa-womanize wakawa hawajulikani.
Ukifanya utafiti wa ndani zaidi naona uwiano ni kama 1:4. Yaani Mwanaume womanizer mmoja, wanawake womanized 4.