How You Can Get Richer... Quicker!: Kitabu nilichokipenda, nikakiogopa, lakini nataka nikisome tena!

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Nani alishakisoma kitabu tajwa? Kimeandikwa na M. R. Kopmeyer.

Ni kati ya vitabu vyangu vya mwanzoni kabisa kukinunua baada ya kuamua kuwa "serious" kwenye usomaji wa vitabu. Nilikinunua Kase Store jijini Arusha mwishoni mwaka 2007.

Nikilipenda sana mwanzoni, lakini baada ya kukisoma chote, nilijikuta kama ninakiogopa vile. Sikutarajia kukutana na niliyokutana nayo humo. Baadhi ya mafunzo yaliyomo yalishabihiana na ya kwenye Biblia.

Kipindi ninakisoma, nilikuwa nimeshaisoma Biblia nzima zaidi ya mara moja. Kukuta kitabu ambacho si cha kidini kikiongelea umuhimu wa kutoa, kuamini, kushukuru, n.k., mambo ambayo nilikuwa nimeyasoma kwenye Biblia, kulinitatiza kidogo. Nilijiuliza ni wapi alikoyatoa hayo huyo mwandishi?

Kwa mfano, kuna sura alipoelezea umuhimu wa kushukuru ambapo alisema chochote mtu anachoshukuru kinaongezeka. Aliongezea na kile alichokidai kuwa ni utafiti uliowahi kufanywa dhidi ya akina mama wenye tabia ya kuyasifia maua ya kwenye nyumba zao na wale wasiofanya hivyo. Wale waliokuwa wakiyasifia maua yao, maua yao yalistawi vizuri zaidi kuliko ya wale wasiofanya hivyo.

Kulingana na mafunzo ya kwenye Biblia, nilikuwa ninafahamu kuwa hata mimea huweza kutii maneno ya "imani". Inasikia. Lakini kukuta jambo kama hilo likiongelewa kwenye kitabu kisicho cha kidini, kulinistaajabisha na kuniweka njia panda kama niendelee kukisoma au la. Kwa ufupi, kiliniogopesha kwa kiasi fulani.

Ni miaka mingi sasa tokea nikisome. Sipo nacho kwa sasa, nilikigawa. Lakini Jana Usiku nimekikumbuka. Nataka nikisome tena. Kwa sasa hakitaweza kuniogopesha. Ninajua kutofautisha wali na chuya.

Kama kuna mwenye pdf yake naomba anisaidie.

Navihitaji na vitabu vingine vya M. R. Kopmeyer:

1. Thoughts to Build On
2. How to Get Whatever You Want
3. Here's Help

Mwenye navyo (soft copy) naomba anisaidie.
 
Kabla hata ya uwepo wa biblia na dini hayo mafundisho ya namna hiyo yalikuwepo tangu enzi za kale hata Africa , waandishi wa biblia ndio waliokopi mafundisho mengi kutoka kwenye mila za kale, na hadithi mbalimbali za kale kwenye tamaduni mbalimbali hasa ugiriki ya kale.
 
Una uthibitisho wa kimaandishi?
 
Nani alishakisoma kitabu tajwa? Kimeandikwa na M. R. Kopmeyer.

Ni kati ya vitabu vyangu vya mwanzoni kabisa kukinunua baada ya kuamua kuwa "serious" kwenye usomaji wa vitabu. Nilikinunua Kase Store jijini Arusha mwishoni mwaka 2007.

Nikilipenda sana mwanzoni, lakini baada ya kukisoma chote, nilijikuta kama ninakiogopa vile. Sikutarajia kukutana na niliyokutana nayo humo. Baadhi ya mafunzo yaliyomo yalishabihiana na ya kwenye Biblia.

Kipindi ninakisoma, nilikuwa nimeshaisoma Biblia nzima zaidi ya mara moja. Kukuta kitabu ambacho si cha kidini kikiongelea umuhimu wa kutoa, kuamini, kushukuru, n.k., mambo ambayo nilikuwa nimeyasoma kwenye Biblia, kulinitatiza kidogo. Nilijiuliza ni wapi alikoyatoa hayo huyo mwandishi?

Kwa mfano, kuna sura alipoelezea umuhimu wa kushukuru ambapo alisema chochote mtu anachoshukuru kinaongezeka. Aliongezea na kile alichokidai kuwa ni utafiti uliowahi kufanywa dhidi ya akina mama wenye tabia ya kuyasifia maua ya kwenye nyumba zao na wale wasiofanya hivyo. Wale waliokuwa wakiyasifia maua yao, maua yao yalistawi vizuri zaidi kuliko ya wale wasiofanya hivyo.

Kulingana na mafunzo ya kwenye Biblia, nilikuwa ninafahamu kuwa hata mimea huweza kutii maneno ya "imani". Inasikia. Lakini kukuta jambo kama hilo likiongelewa kwenye kitabu kisicho cha kidini, kulinistaajabisha na kuniweka njia panda kama niendelee kukisoma au la. Kwa ufupi, kiliniogopesha kwa kiasi fulani.

Ni miaka mingi sasa tokea nikisome. Sipo nacho kwa sasa, nilikigawa. Lakini Jana Usiku nimekikumbuka. Nataka nikisome tena. Kwa sasa hakitaweza kuniogopesha. Ninajua kutofautisha wali na chuya.

Kama kuna mwenye pdf yake naomba anisaidie.

Navihitaji na vitabu vingine vya M. R. Kopmeyer:

1. Thoughts to Build On
2. How to Get Whatever You Want
3. Here's Help

Mwenye navyo (soft copy) naomba anisaidie.
Nitumie soft copy ya hicho mkuu
 
Endelea kusoma vitabu kwa bidii kila kitu na historia mbalimbali utajithibitishia humo mwenyewe.
Vitabu ni vingi sana mkuu! Labda ungenitajia jina la kitabu ili nisisumbuke sana kukitafuta kwa kubahatisha.
 
Back
Top Bottom