KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 32,529
- 76,691
Kopmeyer Marion Rudy - How You Can Get Richer Quicker - PDFCOFFEE.COM
ROVEff • • •SUCCESS METHODSwill multiply your moneyl"By M. R. KOPMEYER AMERICA'S SUCCESS COUNSELORff • • •ha...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umenikumbusha mbali! Tulipokuwa kidato cha tatu na cha nne wenzangu walikuwa wanasubiria nimalize kusoma vitabu vya fasihi na literature kisha niwasimulie kwa sababu kuu mbili:Wengine hatuna muda tupewe summary tu
Ninachopendea soft copy ni portability! Naweza kutembea na vitabu elfu moja kwenye kidude kidogo.Jamani mimi kusoma vitu kwny simu hizo pdf nimeshindwa kabisa..najikuta nasinzia tuu napenda zaidi hard copies...
Salute kubwa mkuu!Hivyo hapo
Buku ya nini mkuu?Una buku ya karibu hapo?
Bila shaka umeshaviona vilivyowekwa na mmoja wa wanafamilia wa JF!Nitumie soft copy ya hicho mkuu
Subiri cha kwangu, (stay tuned), unasoma unakiweka kwapani na kuanzisha biashara mwenyewe yaani simama dede, Kwa kimombo na kiswahiliNani alishakisoma kitabu tajwa? Kimeandikwa na M. R. Kopmeyer.
Ni kati ya vitabu vyangu vya mwanzoni kabisa kukinunua baada ya kuamua kuwa "serious" kwenye usomaji wa vitabu. Nilikinunua Kase Store jijini Arusha mwishoni mwaka 2007.
Nikilipenda sana mwanzoni, lakini baada ya kukisoma chote, nilijikuta kama ninakiogopa vile. Sikutarajia kukutana na niliyokutana nayo humo. Baadhi ya mafunzo yaliyomo yalishabihiana na ya kwenye Biblia.
Kipindi ninakisoma, nilikuwa nimeshaisoma Biblia nzima zaidi ya mara moja. Kukuta kitabu ambacho si cha kidini kikiongelea umuhimu wa kutoa, kuamini, kushukuru, n.k., mambo ambayo nilikuwa nimeyasoma kwenye Biblia, kulinitatiza kidogo. Nilijiuliza ni wapi alikoyatoa hayo huyo mwandishi?
Kwa mfano, kuna sura alipoelezea umuhimu wa kushukuru ambapo alisema chochote mtu anachoshukuru kinaongezeka. Aliongezea na kile alichokidai kuwa ni utafiti uliowahi kufanywa dhidi ya akina mama wenye tabia ya kuyasifia maua ya kwenye nyumba zao na wale wasiofanya hivyo. Wale waliokuwa wakiyasifia maua yao, maua yao yalistawi vizuri zaidi kuliko ya wale wasiofanya hivyo.
Kulingana na mafunzo ya kwenye Biblia, nilikuwa ninafahamu kuwa hata mimea huweza kutii maneno ya "imani". Inasikia. Lakini kukuta jambo kama hilo likiongelewa kwenye kitabu kisicho cha kidini, kulinistaajabisha na kuniweka njia panda kama niendelee kukisoma au la. Kwa ufupi, kiliniogopesha kwa kiasi fulani.
Ni miaka mingi sasa tokea nikisome. Sipo nacho kwa sasa, nilikigawa. Lakini Jana Usiku nimekikumbuka. Nataka nikisome tena. Kwa sasa hakitaweza kuniogopesha. Ninajua kutofautisha wali na chuya.
Kama kuna mwenye pdf yake naomba anisaidie.
Navihitaji na vitabu vingine vya M. R. Kopmeyer:
1. Thoughts to Build On
2. How to Get Whatever You Want
3. Here's Help
Mwenye navyo (soft copy) naomba anisaidie.
Amen GentlemanSalute kubwa mkuu!
Nilikuwa sijaviona. Ama kweli JF unaweza ukapata karibia kila kitu!
Nashukuru sana kiongozi!
![]()
Kopmeyer Marion Rudy - How You Can Get Richer Quicker - PDFCOFFEE.COM
ROVEff • • •SUCCESS METHODSwill multiply your moneyl"By M. R. KOPMEYER AMERICA'S SUCCESS COUNSELORff • • •ha...pdfcoffee.com
🙏🙏🙏Hivyo ninavyo . Nakuekea hapa
Mkuu, kipekee kabisa, ninakushukuru sana wewe na Ibn Anaq kwa vitabu vya Kopmeyer. Nilikuwa nimevikumbuka sana. Nilipanga nifanye mawasiliano na duka la KASE STORES Arusha au HOUSE OF WISDOM BOOKSHOP Dar Es Salaam ili kama wanavyo wanitumie. Japo nahitaji vya hard copy kwa ajili ya Library ya nyumbani, lakini siyo urgently tena. Nitaviagzia wakati mwingine. Kwa sasa acha nisome kwanza soft copy ya HOW YOU CAN GET RICHER QUICKER kisha THOUGHTS TO BUILD ON!![]()
Kopmeyer Marion Rudy - How You Can Get Richer Quicker - PDFCOFFEE.COM
ROVEff • • •SUCCESS METHODSwill multiply your moneyl"By M. R. KOPMEYER AMERICA'S SUCCESS COUNSELORff • • •ha...pdfcoffee.com
🙏🙏🙏Soma , The Greek myths cha Robert graves .
Na The bible & Hellenism cha Thomas l Thompson.
Ukumbuke🙏Subiri cha kwangu, (stay tuned), unasoma unakiweka kwapani na kuanzisha biashara mwenyewe yaani simama dede, Kwa kimombo na kiswahili
Sijapata sir...Tafuta laptop au tablet utaenjoi.
Lakini nilisikia watumishi mmegawiwa vishikwambi hukupata madam?
Vilivyo andikwa na hao waandishi lakini vikatafsiriwa kiswahili.Unamaanisha hivyo nilovyoweka au vyovyote vya kiswahili?
Kuna program inaitwa Pdf translator . Unatafsiri kitabu kwa lugha unayotaka.Vilivyo andikwa na hao waandishi lakini vikatafsiriwa kiswahili.
Karibu kwenye audiobooksJamani mimi kusoma vitu kwny simu hizo pdf nimeshindwa kabisa..najikuta nasinzia tuu napenda zaidi hard copies...