How You Can Get Richer... Quicker!: Kitabu nilichokipenda, nikakiogopa, lakini nataka nikisome tena!

Attachments

Wengine hatuna muda tupewe summary tu
Umenikumbusha mbali! Tulipokuwa kidato cha tatu na cha nne wenzangu walikuwa wanasubiria nimalize kusoma vitabu vya fasihi na literature kisha niwasimulie kwa sababu kuu mbili:
1. Baadhi hawakuwa na muda wa kusoma vitabu "vikubwa" japo havikuwa vikubwa.

2. Wengine walikuwa hawawezi kukisoma kitabu na kukimaliza. Visingizio? Vinaboa!

Nikishawasimulia ndiyo baadhi walikuwa wanavisoma, na wengine walikuwa wakiishia kusoma summary pekee.
 
Jamani mimi kusoma vitu kwny simu hizo pdf nimeshindwa kabisa..najikuta nasinzia tuu napenda zaidi hard copies...
Ninachopendea soft copy ni portability! Naweza kutembea na vitabu elfu moja kwenye kidude kidogo.

Hard copy zina umuhimu wake, na hata mimi ninazipenda sana. Lakini soft copy zinanisaidia sana pindi niwapo safarini.
 
Subiri cha kwangu, (stay tuned), unasoma unakiweka kwapani na kuanzisha biashara mwenyewe yaani simama dede, Kwa kimombo na kiswahili
 
Mkuu, kipekee kabisa, ninakushukuru sana wewe na Ibn Anaq kwa vitabu vya Kopmeyer. Nilikuwa nimevikumbuka sana. Nilipanga nifanye mawasiliano na duka la KASE STORES Arusha au HOUSE OF WISDOM BOOKSHOP Dar Es Salaam ili kama wanavyo wanitumie. Japo nahitaji vya hard copy kwa ajili ya Library ya nyumbani, lakini siyo urgently tena. Nitaviagzia wakati mwingine. Kwa sasa acha nisome kwanza soft copy ya HOW YOU CAN GET RICHER QUICKER kisha THOUGHTS TO BUILD ON!

Nakushukuru sana mkuu๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™
 
Vilivyo andikwa na hao waandishi lakini vikatafsiriwa kiswahili.
Kuna program inaitwa Pdf translator . Unatafsiri kitabu kwa lugha unayotaka.

Ziko nyingi playstore , Kuipata bora angalia Maelezo yake iwe inachukua file la kitabu kuanzia MB10.

Changamoto; Kiswahili kinachotafsiriwa humo muda mwingine kinakua kibovu kisichoeleweka. Lakini kinaeleweka!! Gentleman

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ