Mkuu zama zimebadilika, na mchina bado yuko nyuma sana kiteknolojia ila watu hawalielewi hilo
Hiyo 6x4 ambayo inasemwa kuwa ni kwa ajili ya rough road ilikuwa miaka hiyo, hata scania zile zilizokuwa zinaundwa hapo kibaha miaka ya 90, zilikuwa ni 6x4 ( 113 310 pamoja na 143 450 zilishawahi kuundwa kibaha)
Kuna aina mbili za 6x2, mid lift, na tag axle , mid lift ni ile ambayo diff ipo nyuma, hizi gari ni kwa ajili ya barabara nzuri tu hazitaki shurba
Mbadala wa 6x4. Ni tag axle , kwa wasioelewa tag ni 6x2 ambayo diff iko katikati , hizi zina u wezo.wa kunyanyua akseli ya nyuma na kuifanya diff ibebe mzigo wote hivo kufanya mgandamizo mkubwa .kwa maana hiyo diff ya tag huwa imekuwa designed kubeba hadi tani 15 , angalia hata clips za truck ulaya utaona tag inatumika katika mazingira magumu .
6x4 ina limitation nyingi sana hasa, moja wapo ikiwa ni uzito , na ulaji wa mafuta, kama mtu ndo anangia kwenye biashara halafu anategemea kulipwa kwa tonnage , 6x4 kaa nayo mbali