Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
- Thread starter
-
- #41
Kaka nadhani ni kutokomaa tu na upande mwingine bila ya shaka anawakilisha mawazo wa watu wetu wengi tu ambao hawakupata nafasi ya kuwekewa mic. Alichosema siyo kilichonishtua sana kilichonishtua ni ukimya wa jamii kumkemea. TAtizo kubwa ninaloliona ni baadhi ya watu kuwaweka wahindi wote kwenye kundi moja. Huyu Binti ni Mgoa siyo Mhindu, na sidhani kama mila na desturi zake zinamzuia kuolewa nje ya wagoa...
Ndiyo maana mimi nilikuwa nasema kama madai yangekuwa Richa ametoa rushwa, alipata upendeleo au alibebewa, tungeyaangalia kwa makini, lakini kitu ambacho hana uwezo wa kukibadili kama rangi na nasaba, ni kuwa low tha low itself! Ndiyo maana nimesema tutawapinga wabaguzi hawa mahali popote watakapojitokeza. Wanatumia lugha ya "kizalendo" kuficha dhambi hii! Hata Hitler alipokuwa anawaona watu duni alisema hivyo hivyo "for mother Germany" akitukuza "the superiority of the aryan race"
Hata wale KKK wanapotaka kuwaua watu weusi au wageni wowote wale, wanatumia jina "la Marekani yetu"!
Mjengwa Blog said:
Pamoja na kumpongeza mshindi wa shindano la Vodacom Miss Tanzania, Bi. Richa Radhia nimejaribu kufuatilia malumbano yanayoendelea sasa juu ya matokeo yaliyomtoa mshindi huyo. Kupitia televisheni nimemwona na kumsikia Hoyce akizungumza na watangazaji wa habari. Nimesoma pia maelezo yake yalivyoripotiwa na vyombo vya habari. Nadhani baadhi ya watu wa habari ama kwa kuelewa au kwa kutokuelewa, wanapotosha hoja ya msingi ya Hoyce Temu.
Ni vema Hoyce Temu akaaminiwa, kuwa hapingi matokeo hayo kwa misingi ya rangi ya mshindi isipokuwa ukiukwaji wa taratibu ambazo waandaaji wenyewe wa shindano hilo wamezikiuka. Mawili ya msingi aliyoyaanisha Hoyce ni matumizi ya lugha ya Kiingereza na kuondolewa kwa shindano la vazi la ubunifu . Hilo la mwisho lina umuhimu kutokana na jitihada zetu za kitaifa kutafuta vazi la utambulisho wetu wa kitaifa. Inahusu umakini na uaminifu. Kuna haja ya watangazaji wa habari kuinua kiwango cha mjadala. Kwamba waandaaji wa shindano hilo wana maswali ya kujibu na kutoa ufafanuzi. Watangazaji wa habari wanayo maswali hayo, wasikae nayo mifukoni.
mimi niliopoa binti wa Kihaya aliitwa Rose Ngaiza.. wazazi wake walipogundua kuwa mimi ni mtu wa pwani, wakanitolea nje. Tuliibia ibia, lakini haikuweza kwenda mbali.. sasa sijui niwafikiri vipi Wahaya wote...
Kaka nadhani ni kutokomaa tu na upande mwingine bila ya shaka anawakilisha mawazo wa watu wetu wengi tu ambao hawakupata nafasi ya kuwekewa mic. Alichosema siyo kilichonishtua sana kilichonishtua ni ukimya wa jamii kumkemea. TAtizo kubwa ninaloliona ni baadhi ya watu kuwaweka wahindi wote kwenye kundi moja. Huyu Binti ni Mgoa siyo Mhindu, na sidhani kama mila na desturi zake zinamzuia kuolewa nje ya wagoa...