niwaeleze nini, kwani nini maana ya picha....picha zinajieleza kama huelewi usikonde saa zingie ubongo wa watu tofauti unachukua muda kuelewa mambo tofauti, lkn naamini baada ya kuziangalia sana utazielewa wengine haiwachukui muda sana, lkn ndio hivyo......kaka picha tumeziona! moja ni kama hoyce yuko keroro halafu anauliza yani nyie mnasema mimi nimelewa?
yapili sijui ndo kashika bia au pochi haionekani vizuri ni kama imeungwa vile!
ila kaka pamoja na kuosha macho unataka kutueleza nini juu ya picha hizi hasa hapa kwenye jukwaa la siasa?
niwaeleze nini, kwani nini maana ya picha....picha zinajieleza kama huelewi usikonde saa zingie ubongo wa watu tofauti unachukua muda kuelewa mambo tofauti, lkn naamini baada ya kuziangalia sana utazielewa wengine haiwachukui muda sana, lkn ndio hivyo......
Hili suala la lugha hebu tuliweke sawa kidogo. Kama angechaguliwa mtu ambaye kiingereza hakipandi, halafu baadaye wanaenda Sanya, China kwenye Miss World, hivi anafikiri ataulizwa maswali kwa Kifipa? As a matter of fact, lugha rasmi za Tanzania ni Kiingereza na Kiswahili na hili liwe changamoto kwa wale wote wanaotaka kugombea Umiss "wherever" bora wapandishe kiingereza chao na hata lugha nyingine za ziada. Hebu fikiria kama angekuwepo binti kati yao ambaye amepandisha Kiingereza na Kifaransa, halafu akijibu anajibu kwa kiingereza halafu anachombezea na kifaransa kidogo, huoni huyo angescore juu kuliko hata Richa!?
Kama tatizo ni kuwa wengine kiingereza kimekuwa "maimuna" sasa kwanini wamlalamike Richa? Sasa walitaka Richa naye azungumze kiingereza cha kuvunja vunja ili alingane nao?
Nyangumi, yaani wahindi wakioana na watu weusi ndio wanakuwa raia zaidi?
ngojeni afanye vizuri huko miss world, mtaona anavyomwagiwa sifa za "mtanzania mwenzetu",... Hatukawii kusahau, majuzi tu Allan Johnson (wa BBC)watu humu walimwita "mtanzania mwenzetu", kisa; kazaliwa Lindi!!!
Mimi msimamo wangu utakuwa ni kama ulivyo. Sigeuki nyuma nikawa jiwe. Hawa watu wanaubaguzi wa hali juu tena kibaya zaidi wanaufanya kwetu dhidi ya wazawa, lakini watu hawataki kuuona huo wala kuuzungumzia wanataka kuzungumzia ubaguzi aliofanyiwa yeye tu!