Niliwahi kutokewa na scanerio kama hiyo toka kampuni ya SimbaNet. Nilipigiwa simu kwa ajili ya Telephone Interview.....Unfortunately, nilikuwa sehemu yenye kelele sana hivyo nikamuomba dada aliyenipigia anipe about 3 minutes ili nisogee sehemu muafaka for it; sehemu ambayo tungeweza kusikilizana vizuri! Niliposogea sehemu iliyo tulivu, nikaenda hewani! Simu ikaita sana, lakini haikupokelewa! Nikapiga tena zaidi ya mara tatu; simu haikupokelewa! Nikakata shauri la kuwatumia email....miaka miwili sasa, email yangu haijajibiwa ingawaje natumaini nitajibiwa tu! In short, ma-HR wengi wa Tanzania wapo hivyo.....wanakupigia mara moja, ukishindwa kupokea tu, imekula kwako as if wakati wote ni lazima uwe secure place. Binafsi, sehemu ambayo naamini kuna professionalism kwenye masuala ya HR basi ni pale Standard Chartrered Bank! Ni juzi tu hapa, jamaa walinipigia lakini kwa bahati mbaya walipiga wakati nikiwa kwenye daladala...sikuisikia! Hata hivyo, nusu baadae nilipowapigia, mdada wa HR alipokea na good enough alishafahamu in advance anapigiwa na nani! Four dayz later nikawapigia kutoa appreciation for interview (ingawaje nilishakosa nafasi) bado HR yuleyule ilimchukua robo dakika tu kukumbuka kwamba ni nani alikuwa anaongea nae!! Hawa jamaa hata ukiwapelekea CV, lazima watakuita tu kama una sifa!