Kimbweka
JF-Expert Member
- Jul 16, 2009
- 8,597
- 1,690
Hii huduma ni nzuri sana lakini imekuwa na mapungufu katika kipengere cha kutaka kujua akaunti yako ya benki ina kiasi gani cha fedha kupitia simu yako pamoja na mengine kadhaa. Je kuna tatizo gani na kwa nini hii huduma haitendeki na inamkataza mtumiaji kuitumia kwa kumuambia kuwa haruhusiwi kuitumia hiyo huduma na kama kuna mapungufu kwa nini yasirekebishwe na kuweza kuitumia hii huduma ? Hii ni sambamba na huduma ya kutoa fedha kwenye akaunti ya benki yako na kuipeleka kwenye akaunti yako au ya mwingine ya ZAP pindi unapokuwa mbali na Benki na ungali una shida muhimu badala ya kufika benki. Kama ina matatizo yarekebishwe na kwa hakika kama itajitokeza kampuni yenye kutoa huduma hii na pasiwe na mapungufu wala wizi wengi wataamia huko na kuwaacha hao Airtel na basi lao Jekundu