Hudhuria maonesho ya kanda ya nane nane 2019

Narubongo

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
2,768
Reaction score
2,753
Kwa wadau wote wa kilimo na ufugaji,

muda wa kupata maarifa mapya ni huu mpaka tarehe 8/8.

Tuepuke kufanya ufugaji na kilimo cha mazoea. Ukihudhuria maonesho haya utajifunza mengi kitaalam kati ya haya

Mbegu bora, nafaka, spices, matunda kama strawberry etc

Namna ya kuhudumia shamba na mifugo

Namna ya kukabiliana na changamoto

Masoko

Teknologia

Utaona mifugo bora kabisa na connection ya kuinunua iwapo utahitaji mfano ng'ombe, mbuzi, nguruwe, kuku, mbwa, bata etc

Utapunguza kuwa muhanga wa kuuliza maswali mepesi sana JF.

Itakupa uwezo wa kufanya maamuzi sahihi ya nini cha kufuga au kulima

Itakupa ujasiri wa kufanya kivitendo

Kukubadili kimtazamo

Nashauri ukifika kwenye maonesho haya uwe na lengo la kujifunza kwa kina kwa kuuliza chochote kile, usiende kutalii tuu, angalau masaa 5 kila siku kwa siku 4 utajifunza kitu. Kuna mengi sana mazuri huku.

Usione gharama za usafiri, malazi na chakula kama kikwazo. Faida ni kubwa sana usingoje mwakani.. too far, nenda sasa uanze kujipanga taratibu kufikia malengo yako.

Kwangu mimi nilipenda sana maonesho ya mwaka jana ya kanda ya kaskazini Arusha-njiro. Mwaka huu nitakuwa southern highlands mbeya.
 
Mzee ukiwa vizuri pia mwezi wa 9 mwishoni kabisa nenda Nairobi kenya kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo ya ya Nairobi. Yale ni Makubwa East and Central Africa. Mkuu kule unaweza toka kichwa mimeflashika vibaya mno.

Ni maonyesho mazuri mno na makubwa sana ile Sabasaba ni cha mtoto
 
Binafisi nimekuwa naenda san maonyesho ya Nairobi na this time napanga tena kwenda.

Kama unataka kuwekeza hasa kwenye Mifugo au Kilimo basi kule ndo kwenyewe.
 
Mkuu hua ni tar ngp je gharama za chumba bei gani per day! !
 
Naendaga na kurudi. Nairobi huwa naenda na kurudi kulala arusha. Naondokaga saa 10 asubuhi ikigika saa 12 niko boda nisha gonga muhuri na by saa 3 au 4 niko Nairobi na kule natoka saa 12 kamili jioni na by saa 4 niko Arusha
Mkuu hua ni tar ngp je gharama za chumba bei gani per day! !
 
Naendaga na kurudi. Nairobi huwa naenda na kurudi kulala arusha. Naondokaga saa 10 asubuhi ikigika saa 12 niko boda nisha gonga muhuri na by saa 3 au 4 niko Nairobi na kule natoka saa 12 kamili jioni na by saa 4 niko Arusha
jamma kaulizia nauli ya Nai to arachuga, chakula NK
 
Asante mkuu, nitaangalia ratiba zilivyokaa, huwa nachota maarifa mengi kutoka Kenya. Jamaa wapo vizuri sana kwenye kilimo biashara duniani
 
Arusha hadi Namanga sh 7000 na Namanga hadi Nairobi ni kama sh 12000 sasa times 2 utapata ni how much go and return.
Kutoka Nairobi Stend hadi Maonyesho yalipo ni kama sh 1500 hivi
 
Kula ni kama sh 8000 inatosha. So ukiwa na Laki 1 inatosha na Chenji inabakia na kama utafanya na manunuzi basi pia inatosha kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…