meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,425
- 4,768
mkuu Ruta nitarudi!
Vipi meningitis? rudi bana umpe jamaa shule aelewe hali halisi, naona mkuu Jackbauer amefafanua ipasavyo. Wananchi hata wanapoambiwa huduma ya mama na mtoto ni bure wakati budget inayoletwa haitoshi ni issue kumweleza akanunue catheter ama IV fluids. Mkoa wa Kilimanjaro hospitali ya mkoa haina chumba chaupasuaji tangu 2010 december this is a holly joke!!
MKUU RUTASHUBANYUMA NAKUPONGEZA SANA KWA THREAD HII!!
Vipi meningitis? rudi bana umpe jamaa shule aelewe hali halisi, naona mkuu Jackbauer amefafanua ipasavyo. Wananchi hata wanapoambiwa huduma ya mama na mtoto ni bure wakati budget inayoletwa haitoshi ni issue kumweleza akanunue catheter ama IV fluids. Mkoa wa Kilimanjaro hospitali ya mkoa haina chumba chaupasuaji tangu 2010 december this is a holly joke!!
Hapo sasa!
Jackbauer nakushukuru nawe pia.........na nilisahau ya kuwa huduma za maabara zapaswa kuwa masaa 24...............yawaje wagonjwa siku za wikiendi na sikukuu hususani wagonjwa wapya wasahaulike kupata vipimo kabla ya tiba na matokeo yake utakuta wanapewa matibabu ya kubahatisha kwa gharama kubwa kwa mgonjwa na kwa umma kugharimia magonjwa ambayo huenda siyo yaliyomsibu mgonjwa..................
Tanzania kwa sasa hatuna huduma za afya bali tuna usanii wa kiafya.
Kumpeleka hospitali za umma mgonjwa wako ni sawa na kumsindikiza kaburini.
Tatizo la huduma ya afya Tanzania linasabishwa na bad or non existent healthcare financing policy.
Hata Marekani na nchi nyingine zilizoendela kama zingekuwa na mfumo wa kutoa huduma za afya bure au kwa kuchangia basi huduma zingekuwa duni hivihivi.
Tunahitaji mfumo wa bima ya afya ambao utawezesha kusupport healthcare system na serikali kusubsidize kwenye mapungufu. Ni vema tungechukua utaratibu wa compulsory health insurance ambayo inakatwa kutokana na kipato cha mtu.
Nitafurahi siku nikiona mwanasiasa au chama cha siasa kinakuja na healthcare bill ambayo ina features zenye kuonyesha matumaini ya kuutoa mfumo wetu wa afya hapa ulipo.
Mkuu Rutashubanyuma fikiria hospital ya rufaa machine ya CT Scan imeharibika kwa kipindi cha mwaka mzima unategema nini.......ni sio kwamba nini serikali inaweza kununua machine zaidi ya moja kama wataacha ubinafsi......Hospital kama Mount Meru ilipashwa kuwa na hiyo machine......wao wanajali nini wakati wahatatibiwa kwenye hizo hosp wametuachia sie wakata mkonge
kwa mara ya kwanza tunajenga nchi moja bila kugombea fito!
ndio maana Tanzania Tunaongoza kwa usugu wa magonjwa, dawa zinapatikana mpaka sokoni. kila unapoenda kuna dawa za marelia, za kutuliza maumivu n.k. mtu akisikia kichwa kinauma anasema nina maleria, tumbo linauma nina amiba, mara taifodi n.k. anajitibu mwenye huyo. Mwisho wa siku magonjwa hayo yakikupata hizo dawa hazikuponyi tena ndio mwanzo wa kupanda kwa gharama za matibabu na wenye uwezo kwenda india.mkuu kwa swala maabara ni uzembe wa hospitali husika,wahudumu wa afya(madaktari au waganga) na wateja wenyewe.
Nianze na mteja,hivi unakubali vipi kupewa dawa kabla hujaambiwa tatizo lako?ukiambiwa una malaria unapaswa kuhoji uthibitisho wa matokeo ya vipimo au unapaswa kuelezwa na kuridhika kuwa kipimo hakijaonyesha lakini kwa dalili ulizonazo zinaelekea kuhusiana na ugonjwa flani hata kama vipimo havionyeshi hivyo.wazungu wana demand kujua tatizo lao kabla ya kutumia dawa,na sisi tuanze kujenga utaratibu huu.
Kwa upande wa madaktari/waganga ni muhimu na wajibu kwao kuhakikisha wanatoa matibabu kulingana na ushahidi wa vipimo isipokuwa pale mazingira ya ya kupata majibu au vipimo yanapokuwa magumu na mgonjwa yupo kwenye hatari ya kufa.mfano ni upuuzi kumpa mtu dawa ya malaria wakati vipimo vya malaria vinapatikana kwa urahisi ndani ya muda mfupi.
Kwa upande wa uongozi wa hospitali,hawa wanawajibika kuhakikisha vipimo muhimu na vya kawaida vinapatikana muda wote.
Ni kichekesho kukuta maabara ya hospitali ya mkoa au wilaya inashindwa kutoa huduma kwa masaa 24 !