Huduma kwa wateja necta bado hazijakidhi ubora mzuri

Huduma kwa wateja necta bado hazijakidhi ubora mzuri

Third eye judge

Senior Member
Joined
Aug 9, 2016
Posts
147
Reaction score
132
Habari,, Tuna Huduma mbalimbali zinazohudumia mamilioni ya wateja nchini kama vile mitandao ya simu, tanesco, mabenki nk.

Ingependeza sana taasisi muhimu kama NECTA ingeweka juhudi zaidi katika ubora wa Huduma kwa wateje hasa wale wa mikoani kwani Huduma muhimu kama vile uthibitisho wa vyeti, notisi ya matokeo (statement of results), barua ya uthibitisho nk, Huduma hizi zikawekewa mfumo unaofikikika na kushughulikiwa kwa wepesi na kwa haraka.

Kwa kufanya hivi utawasaidia Watanzanzania wengi hasa wanao hitaji kujiendeleza kimasomo nje ya nchi kwani linapokuja suala la kuendana na mihula ya masomo, taratibu za kukamilisha verification huchukua mlolongo mrefu sana na kupelekea kuchelewa kipindi Cha udahili wa vyuo vya nje na hatimaye kukosa nafasi ya kujiunga na muhula husika nje ya nchi.

Simu kwa ajili ya Huduma kwa wateja NECTA ni kweli IPO, lakini hadi ipokelewe huchukua muda mrefu sana, na pengine isipokelewe kabisa.

Dunia imebadilika sana kwa Sasa, na imefikia hatua baadhi ya taasisi ambazo zimejizatiti kuwahudumia wateja wao kwa wakati kuamua kuweka what's app namba, licha ya kuwa na namba ya kupiga au kuwa na email ambazo bado zinaonekana kutofanya vizuri sana katika kuhakikisha mawasiliano kwa wakati.

Napendekeza kuwekwe mfumo wa kurahisisha mawasiliano kwa wateja katika taasisi muhimu ya NECTA, kuthamini hitaji la haraka kwa wateja, kwa wakati, Ili kutofifisha ndoto za wengi wenye haki ya kimsingi ya kupata Huduma stahiki katika taasisi hii muhimu sana hapa nchini.
 
Back
Top Bottom