KERO Huduma mbovu basi la Alys Star

KERO Huduma mbovu basi la Alys Star

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Rugeji

New Member
Joined
Feb 11, 2013
Posts
3
Reaction score
4
Wakuu habari za usiku,
Natumai nyote mko salama.

Naomba kushare uzoefu mbaya nilioupata katika moja ya mabasi ya Alys Star yanayofanya safari za Mwanza - Dar.

Katika harakati za kutafuta mkate nikitokea pande za kanda maalum kurudi Daslam kupitia Mwanza usafiri ulikua shida kidogo mabasi yalikua yamejaa mapema katika kuhangaika nikapata Alys Star ya mchana saa 9;00 katika safari yangu nimeona vifuatavyo kama kero kwa wasafiri ndani ya hilo basi

1. Rough Drivers
Gari ilikua inaendeshwa bila kuzingatia ubora wa barabara eneo husika kupelekea mizigo ya abiria kwenye carrier kuanguka hovyo ndani ya basi pia kona zonakunjwa kama tunakimbizwa

2. Mziki mkubwa usiku wa manane

Saa nane usiku mziki mkubwa ni mwendo wa bongo flavour + old school za mbele huu ni muda ambao abiria tunahitaji japo kupumzika bila kujali baadhi ya abiria wamekaa karibu na spika na pale walipotaarifiwa hakuna aliyesikilizwa this is unacceptable

3. Tunatembea na takataka kwenye gari zaidi ya mikoa mitatu na tunasimama vituo mbalimbali kwa ajili ya kuchimba dawa pia dustbins kubwa zinazuia movement ya watu kuingia na kutoka.

Pamoja na hayo yote gari ina wahudumu wanne hawa wako serious kweli + kusimamisha abiria kama daladala corridor yote watu wamesimama.

Mambo ni mengi hayo machache kwa leo.
 
Kuna bus lina huduma nzuri kuliko shabiby kweli maana ukipanda amna mambo ya kukaguana ticket wala usumbufu mwingi mhudumu mmoja tu
 
Hawajawazidi Super Feo kwa huduma mbovu......nimejaribu hizi gari mara nne kwenda kusini mwishowe nimeamua bora kupanda hata Costa za kuunga unga kuliko SUPER FEO
 
Ni kweli mkuu juzi kati nilikua na safari ya mwanza mbeya nilikata ticket ya gari ya chakaby, kumbe siku hiyo gari haikuwepo agent alipo gundua akainipigia cm kuni taarifu na semahanini nyingi,nikakubali kinyonge aka shauli nipande allisy nilijuta nika apa kusafiri na allisy tena sijui.
 
Back
Top Bottom