Ukienda kukata tiketi ya boti hapo bandarini iwe Azam ama Zanzibar One, ndani ya dakika tatu (maximum) mchakato mzima umekuwa umeisha! Namaanisha ukishatoa hela plus nyaraka pale dirishani!
Nenda ofisi za SGR ukaone mziki wake! Picha linaanza huo muda utakaotumia mpaka ufike dirishani! Ongezea ukishafika dirishani huyo mkata tiketi muda atakao utumia kukuhudumia! Hata ukikata online lazima uende hapo dirishani, utajuta!
Mwendo ni uleule ajira za kujuana! Basi wajue hata kufanya kazi, hamna lolote!