KERO Huduma mbovu kwa wateja stesheni ya SGR Dar es Salaam

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Na ku extend au ku cancel safari? Ticket yapaswa kuwa na terms/conditions za ku cancel/extend Ticket na uweze kufanya online kama tiketi za ndege. Tiketi ziko plain tu hazina masharti na vigezo vyovyote.
Tiketi hii haina terms wala condition, ukinunua haibadilishwi wala hairudi. Haiwezi kuwa kama ya ndege au bus. Ukiona haiko sawa panda bus au ndege. Option ni nyingi.
 
Mnatamani sana huu mradi ufe, mnapata faida gani ukifa?
Rrondo hatutamani kabisa ufe ila dalili zimeanza kuonekana kabisa hata mimi nilisafiri tu lisije kufa sijapanda na niliyoyaona nilijipongeza kwa kuwahi kulipanda kama kuna mambo yakiendelea vile hata wewe kama hujalipanda kawahi mapemaa usije kusimuliwa.
 
Dalili gani mmeziona wenzetu?
 
Nilivyokuelewa maana yake utatumia simu, vipi aliyetumiwa kwenye kompyuta?? Nahisi lazima aprint au inakuwaje??
Inatumwa kwenye e mail ambayo kwenye simu pia e mail zipo. Usije kuniambia huna smartphone kwasababu dunia ya leo maisha ni rahisi kutumia smartphone. Tiketi imetumwa kwenye e mail sio computer.
 
Tanesco hawa hawa au kuna wengine ?
Hawa unajaza form ya kuunganishwa umeme miezi mitatu inapita
Hawa hamna kitu ,nakataa
 
Yaani hizi.huduma kama mwendokasi, sgr ziendeshwe na sekta binafsi, miundombinu ibaki kuwa ya serikali, nafikiri ikiwa hivyo mambo yatakuwa safi
 
Ukikata mtandaoni wakakurushia tiketi katika email yako kuna sehemu ya ku scan.
Unapeleka moja kwa moja pale pa kupitia jamaa anatizama ana scan unapita.
 
Muwarekodi..msiporekodi watu watasema majungu...
 
Through my observation ya utendaji kazi hili treni ni kwamba, wahudumu wa treni ya umeme SGR wameajiriwa kwa rushwa ya ngono au undugu au kubebana tu ndio maana utendaji kazi wao ni upuuzi mwingi...
Wana poor customer service kuanzia getini, ofisini mwao hadi ndani ya treni... Sisi WaTz sijui nani katuroga tunaanzisha projects kubwa ila usimamiz sifuri... Nilicho observe ktk hili treni kuna uzembe wa makusudi unafanyika ili wahusika wapige pesa waihujumu serikali...
 
Tiketi hii haina terms wala condition, ukinunua haibadilishwi wala hairudi. Haiwezi kuwa kama ya ndege au bus. Ukiona haiko sawa panda bus au ndege. Option ni nyingi.
Wabongo tujifunze maarifa mapya kuondoa usumbufu usio na msingi. Ukiwa na smartphone unaweza kufanya process zote za sgr mwenyewe, tena kirahisi tu.

Pia mkuu RRONDO sasa hivi unaweza kubadili mwenyewe tarehe ya safari baada ya kukata.
 
Nawajibu kimkato watu wanaopenda kulialia. Kila kitu kulialia tu kama last born.
 
Muwasuse tuendelee kutumia mabasi hadi watakapokuwa siriaz
 
Achananeni nao jaman,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…