A
Anonymous
Guest
Wakuu, salaam.
Leo, tarehe 27 Septemba 2026 majira ya saa 1 usiku, nilikumbana na tukio ambalo nimeona ni muhimu kulishirikisha ili watumiaji wengine wa huduma ya parking katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wawe makini.
Nilifika kwenye kibanda cha malipo ya parking ili kulipia huduma hiyo. Mhudumu aliyenihudumia alipokea malipo yangu, akanirudishia chenji pamoja na risiti, lakini hakunirudishia kadi ya parking. Nilipofika getini ndipo nilipogundua kuwa sikuwa na kadi hiyo, hivyo nilirudi haraka kwenye kibanda kumuuliza.
Badala ya kukiri kuwa alisahau kunirudishia kadi, mhudumu huyo alisisitiza kuwa “anaijua kazi yake” na kuniambia nilipie Lost Ticket ya Shilingi 20,000. Nilimweleza kuwa tayari nilikuwa nimelipia parking, nilikuwa na risiti inayoonyesha malipo, na kadi haikupotea kwangu bali haikunirudishwa baada ya malipo. Hata hivyo, hakukubali maelezo hayo.
Ili kuepusha mabishano na usumbufu zaidi, niliamua kulipa Shilingi 20,000 kupitia Lipa Namba. Cha kushangaza, mhudumu huyo alikuwa akisisitiza nifanye malipo kwa fedha taslimu (cash), jambo lililonifanya nihoji zaidi kuhusu uwazi wa utaratibu huo wa malipo.
Taarifa zilizopo kwenye tiketi niliyopewa ni kama ifuatavyo:
Hii ni hospitali ambayo watu wengi wanaofika huwa wana wagonjwa na mara nyingi wako katika hali ya msongo wa mawazo. Haitakuwa sahihi hali hiyo kutumiwa kuwatoza wananchi fedha bila utaratibu unaoeleweka.
Naomba uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na kampuni inayoendesha huduma ya parking ufanyie kazi suala hili, uchunguze kilichotokea na kunirejeshea fedha nilizolipishwa kimakosa.
Wakuu, tuwe makini na kuhakikisha tunatunza risiti zetu kila tunapofanya malipo.

- Lost Ticket: 0125/0012/00704
- POS: 4
- Tarehe: 27/09/2026
- Muda: Saa 19:23
- Mteja ambaye tayari amelipia parking na ana risiti ya malipo anawezaje kulipishwa tena gharama ya Lost Ticket?
- Kwa nini mhudumu anasisitiza malipo ya fedha taslimu wakati kuna mfumo rasmi wa malipo kupitia Lipa Namba?
- Je, kuna kamera za CCTV katika eneo la kibanda cha malipo? Ikiwa zipo, naomba zifanyiwe ukaguzi ili ukweli wa tukio hili ubainike.
- Kuna utaratibu gani rasmi wa kushughulikia malalamiko ya wateja wanaopata changamoto kama hii?