John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel ameonyesha kukasirishwa na huduma mbovu inayotolewa katika Hospitali ya Wilaya ya Siha baada ya wananchi kulalamikia huduma mbovu huku akikiri kujionea kwa macho yake baada ya kushuhudia mgonjwa akiachwa zaidi ya saa moja bila kuhudumiwa.
"Ninaagiza Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Siha aondolewe katika nafasi hiyo abaki kama Daktari wengine, nilifika hapa zaidi ya mara sita na jana nimekuja tena nikakuta Askari aliyepata ajali akiwa ametelekezwa bila msaada wowote," - Dkt Molle Naibu Waziri wa Afya.