Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel ameonyesha kukasirishwa na huduma mbovu inayotolewa katika Hospitali ya Wilaya ya Siha baada ya wananchi kulalamikia huduma mbovu huku akikiri kujionea kwa macho yake baada ya kushuhudia mgonjwa akiachwa zaidi ya saa moja bila kuhudumiwa.
"Ninaagiza Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Siha aondolewe katika nafasi hiyo abaki kama Daktari wengine, nilifika hapa zaidi ya mara sita na jana nimekuja tena nikakuta Askari aliyepata ajali akiwa ametelekezwa bila msaada wowote," - Dkt Molle Naibu Waziri wa Afya.
Hilo nalo
Alafu Mganga mfawidhi hawezi kuzunguka kila section muda wote wakati Kuna majukumu mengine yanaendelea kumkaba na ni majukumu ya wizara huku akitakiwa taarifa zake zifike immediately.
That's not fair. Then amejaribu hata kuangalia walioko zamu kuwa nao walikuwa na Majukumu gani? Maana wakati mwingine Kuna emergency kubwa zaidi au wapo kwenye chumba Cha upasuaji na waliobaki hawana uwezo wa kuhudumia kutokana na elimu yao na Majukumu yao.
Ukiwa na cheo usitumie mamlaka Yako kuumiza wengine ili kuonekana upo vizuri na kutetea cheo chako.
Ila all in all MUNGU anatuona, na MUNGU atusaidie tu tushushe viburi vya Maisha tukifanikiwa na tukiwa na nafasi Fulani katika jamii.