Huduma mbovu zinazotolewa sasa na benki ya CRDB

Huduma mbovu zinazotolewa sasa na benki ya CRDB

sinzahome,
CRDB wanatutesa kwa kweli wateja wao.Kadi unaisubiri miezi wakat wakongwe NBC unapewa hapo hapo!Aibu kwa kweli.
 
Toka january nafuatilia kadi wanasema sababu ya corona outbreak, materials wanayotengenezea kadi hawajayapata kwa sababu wanachukulia china.

Nikawauliza ina maana dunia nzima hayo material yako China tu? Kwa nini wasiangalie nchi nyingine ya kuagiza? Wakadai wanafuatilia sehemu nyingine.

Wakiona unafuatilia sana wanakushauri wakupe ile Gold card ambayo makato yake yako juu.
 
sinzahome,
Kama mishahara ya watumishi wanaopitishia kwenye hiyo bank inatoka kwa wakati basi haina shida hayo mengine unayoyalalamikia ni kawaida tu.
 
Usisahau network down, ATM kutokuwa na mkwanja.
Bodi ya Wakurugenzi, Wadhamini mpo?
CRDB inaelekea kuwa SACCOS
 
Leo nmetoka kuhudumiwa CRDB Meru branch nmehudumiwa vizuri sana tena kwa haraka.
Mwaka jana kadi yangu ya ATM iliisha muda wake nikaenda kubadili, niliipata baada ya wiki mbili.
Kila nikienda CRDB napata huduma nzuri.
Nadhani changamoto zinategemea na wahudumu.
 
Mimi ni mteja wa Benki ya CRDB zaidi ya miaka 10 sasa, maana kwa ninavyokumbuka niko pale kama mteja wao tangu mwaka 2008,

Tangu nilipoijua CRDB mwaka 2008 huduma walizokuwa wanatoa ndio zilinifanya nijiunge na benki yao, ila kwasasa huduma wanazotoa zitanifanya niikimbie benki yao na kurudi kule nilikokuwa kwa maana kuna nafuu wa huduma bora za Kibenki kuliko hii CRDB ya sasa, Huduma zake kwa wateja zimekuwa mbovu kupindukia hadi kuna kuda namkumbuka DKT. CHARLES KIMEI, hadi kuwa najiuliza tuu hivi huyu mzee aliondoka na Benki yake au? Kama hali yenyewe ndio hii ya sasa sisi wateja tutakimbia wengi na kwa mtazamo wangu miaka 10 ijayo hii benki wasipo angalia inaelekea kufa kabisa.

HUDUMA MBOVU Mfano: Kadi za ATM za wateja wa CRDB zilizoisha Muda wake za tangu mwaka jana Novemba 2019 mpaka sasa Machi 2020 kwa wateja wao wa Tanzania nzima hawajapatiwa kadi mpya za kuendelea kufanya huduma za kifedha kwa kutumia KADI ZA ATM, ni malalamiko tuu kila siku kwa wateja ukienda Tawi lolote la Benki hiyo na majibu wanayotoa wafanyakazi ni hata wao hawajui hizo kadi zitakuja lini, mimi najiuliza Tuu Benki kubwa kama CRDB kweli Kadi za ATM tuu ndio zinawateteresha hivyo hii hatari.

Yako mengi tuu ya hiyo benki ila kwa sasa tuongelee hili linalokiki huko kwao ambalo kwa ukubwa wa CRDB Benki linanishangaza, kuna madudu kama kwenye mikopo, foleni kubwa benki kuliko hata benki Fulani Fulani zile tulizokuwa tunazilalamikia au kuzihama huko awali, n.k

Nadhani DKT. CHARLES KIMEI toka aondoke mwaka 2018 ameondoka na Benki yake maana huduma zimekuwa mbovu kupindukia tofauti na wakati wake alipokuwepo, na kinachonifanya niamini kuwa DR.KIMEI ameondoka na benki yake, ni tangu aondoke huduma za benki hiyo zimekuwa zinaporomoka kila siku iendayo kwa Mungu. Natamani DKT CHARLES KIMEI huko aliko sasa arudi CRDB hata Wiki 1 tuu aje kuweka mambo sawa maana hali ya Benki kwa sasa ni tete saaaaana.

Namshauri BW. ABDULMAJID NSEKELA awasiliane na DKT. CHARLES KIMEI ampe mbinu za benki alivyokuwa akiiongoza maana utendaji yeye wa sasa toka aachiwe kiti unaishusha Benki siku hadi siku

IMETOLEWA KWAKO na Mpenda Benki ya CRDB kimaendeleo.

Mlioko CDRB mna mchango gani?
Acha tu huduma mbovu bali pia hiyo bank ni wezi.

Nilikuwa na mkopo katika bank yao, mkopo huo nilikuwa naulipa kupitia makato ya mshaharavwangu. Nikamaliza deni na salary slip ikasoma 0 katika deni lao. Tena ikapita mda ndiyo mwezi wa 3/2020 nikabaini kukatwa mshahara wangu. Nilifuatilia na kubaini pesa yangu imekatwa na kupelekwa crdb bank kama malipo ya deni. Kuwauliza wanasema walikosea kuna pesa haikujumlishwa katika makato yangu hivyo wameanza kuyakata hayo malipo ambayo hayakujumlishwa katika mkopo wangu.

Ninaongea na wanasheria kuona ntawashitaki vipi wezi hawa wa mshahara wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasiasa wa CCM wanapoingia madarakani uhakikisha kila sehemu wanaweka watu wao ambao wakiamlisha wanataka pesa watapewa fasta

Ukumbuke serikani inakopa sana hii so usikute ndani na nje usikute Kimei alitaka watu wafate sheria sio wakitaka pesa kuchota tu ndio labda uyu akiambiwa tupe bilion 50 fasta anatoa na uwenda aliwekwa kimkakati.

Unakuwa na plan za kipumbavu unaweka mtu sehemu ili utimize haja zako bila kujua nyuma ya kioo unaua iyo taasisi pengine hata izo pesa utakazokuwa unazitaka kuna muda utafika hautazipata.
Hii inahusianaje na huduma mbovu zinazolalamikiwa na wateja kamanda? [emoji2221][emoji2221][emoji2221]
 
Back
Top Bottom