Huduma mbovu zinazotolewa sasa na benki ya CRDB

sinzahome,
CRDB wanatutesa kwa kweli wateja wao.Kadi unaisubiri miezi wakat wakongwe NBC unapewa hapo hapo!Aibu kwa kweli.
 
Toka january nafuatilia kadi wanasema sababu ya corona outbreak, materials wanayotengenezea kadi hawajayapata kwa sababu wanachukulia china.

Nikawauliza ina maana dunia nzima hayo material yako China tu? Kwa nini wasiangalie nchi nyingine ya kuagiza? Wakadai wanafuatilia sehemu nyingine.

Wakiona unafuatilia sana wanakushauri wakupe ile Gold card ambayo makato yake yako juu.
 
sinzahome,
Kama mishahara ya watumishi wanaopitishia kwenye hiyo bank inatoka kwa wakati basi haina shida hayo mengine unayoyalalamikia ni kawaida tu.
 
Usisahau network down, ATM kutokuwa na mkwanja.
Bodi ya Wakurugenzi, Wadhamini mpo?
CRDB inaelekea kuwa SACCOS
 
Leo nmetoka kuhudumiwa CRDB Meru branch nmehudumiwa vizuri sana tena kwa haraka.
Mwaka jana kadi yangu ya ATM iliisha muda wake nikaenda kubadili, niliipata baada ya wiki mbili.
Kila nikienda CRDB napata huduma nzuri.
Nadhani changamoto zinategemea na wahudumu.
 
Acha tu huduma mbovu bali pia hiyo bank ni wezi.

Nilikuwa na mkopo katika bank yao, mkopo huo nilikuwa naulipa kupitia makato ya mshaharavwangu. Nikamaliza deni na salary slip ikasoma 0 katika deni lao. Tena ikapita mda ndiyo mwezi wa 3/2020 nikabaini kukatwa mshahara wangu. Nilifuatilia na kubaini pesa yangu imekatwa na kupelekwa crdb bank kama malipo ya deni. Kuwauliza wanasema walikosea kuna pesa haikujumlishwa katika makato yangu hivyo wameanza kuyakata hayo malipo ambayo hayakujumlishwa katika mkopo wangu.

Ninaongea na wanasheria kuona ntawashitaki vipi wezi hawa wa mshahara wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii inahusianaje na huduma mbovu zinazolalamikiwa na wateja kamanda? [emoji2221][emoji2221][emoji2221]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…