Huduma ya AVA ya Akili Unde (AI) yazinduliwa leo Septemba 29, 2026

Huduma ya AVA ya Akili Unde (AI) yazinduliwa leo Septemba 29, 2026

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
DSC06230.jpg
Taasisi ya Jamii Afrika imezindua Huduma ya AVA (Ask Viamo Anything), teknolojia ya akili unde (AI) inayomuwezesha mtumiaji kuuliza maswali na kupata majibu kupitia simu bila kuhitaji intaneti

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ziada Seukindo, Mkuu wa Programu kutoka Jamii Afrika, amesema huduma hiyo imetengenezwa kwa kushirikiana na kampuni ya teknolojia ya Viamo kutoka Canada.
DSC06206.jpg

DSC06208.jpg
Balozi Emily Burns: Taarifa zinazoaminika na sahihi zinasaidia kufanya maamuzi
Akizungumza katika Uzinduzi AVA (Ask Viamo Anything), Balozi wa Canada nchini Tanzania, Emily Burns amesema “Najivunia Canada inaunga mkono mpango huu ambao unalenga kukabiliana na changamoto za Wananchi wengi maeneo mbalimbali ya Tanzania kupunguza pengo la Kidijitali.”

Ameongeza “Taarifa zinazoaminika ni muhimu katika kumwezesha Mwananchi kufanya maamuzi kuhusu hali ya Afya, Maisha na Shughuli za Kiuchumi, Kilimo, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na huduma za umma, bado watu wengi wanakabiliwa na vikwazo vya kupata taarifa hizo.”
DSC06239.jpg

DSC06219.jpg
Emily Burns: Akili Mnemba ya Sauti inaweza kusaidia makundi mengi ya Wananchi
Balozi wa Canada nchini Tanzania, Emily Burns anasema “Ushahidi unaonyesha Akili Mnemba (AI) inayotumia teknolojia ya sauti (Kupitia Ask VIAMO Anything - AVA) inaweza kusaidia makundi ya Wananchi ambao hawajahudumiwa vya kutosha.

Amesema “Tunafurahi kwamba Jamii Africa na VIAMO wanaleta suluhisho hili hapa Tanzania, na huduma hii itapatikana kwa Kiswahili ili kuwafikia Watanzania wengi zaidi. Teknolojia haipaswi kuwahudumia tu wale wenye simu janja na wanaopata kwenye Intaneti.

“Inapaswa pia kuwahudumia Wakulima wanaotafuta ushauri, Vijana Wajasiriamali wanaotafuta fursa, Wanawake wanaofanya maamuzi kuhusu afya zao, pamoja na familia za vijijini zinazotafuta taarifa zinazoaminika kwa lugha yao (Kiswahili).”

=======================​

AVA ni huduma ya AI inayokuwezesha kuuliza maswali na kupata majibu kwa njia rahisi bila Intaneti bure. Inapatikana kwa kupiga namba 0901760321 kwa Watumiaji wa Vodacom Pekee.

1. Piga 0901760321.
2. Utasikia ujumbe wa karibu na menyu ya awali.
3. Chagua 1 – AVA ili kupata huduma ya AVA. (ASK VIAMO ANYTHING)
4. Kisha unaweza kufuata maelekezo ili kuzungumza na AVA. Unangoja nini? Piga sasa!
 
1. Piga 0901760321.
2. Utasikia ujumbe wa karibu na menyu ya awali.
3. Chagua 1 – AVA ili kupata huduma ya AVA. (ASK VIAMO ANYTHING)
4. Kisha unaweza kufuata maelekezo ili kuzungumza na AVA. Unangoja nini? Piga sasa!
Kwanini sio kwa njia ya maandishi kama ilivyokuwa Jamii Forum enzi hizo wakati inapatikana bure kupitia (FreeBasics)?
 
Usahihi wa lugha kwa watanganyika ndo kipengele (R) na (L)
Hiyo AVA itakuwa na kazi+
 
Back
Top Bottom