Huduma ya kujitenga (self exclusion) kwenye makampuni ya kubashiri iwe kwa mujibu wa sheria

Huduma ya kujitenga (self exclusion) kwenye makampuni ya kubashiri iwe kwa mujibu wa sheria

Chipupute

Member
Joined
May 1, 2024
Posts
5
Reaction score
35
Huduma ya kujitenga kwa muda ama moja kwa moja (temporary self exclusion or permanent self exclusion) kwenye makampuni ya michezo ya kubashiri (online) haipaswi kuwa ni huduma ya hiari kwa watoa huduma bali itengenezewe sheria na kuwa ya lazima.

Katika nchi duniani huduma hii inasimamiwa kwa mujibu wa sheria. Kwa hapa kwetu makampuni mengi ya michezo ya kubashiri hayajajumuisha huduma hii kwenye betting sites zao. Ni wakati sasa serikali ya JMT kupitia Bodi inayosimamia michezo ya bahati nasibu kupitisha sheria zitakazowalinda watumiaji wa huduma hizo ili kupunguza madhara makubwa yanayoweza kuepukika.

Sambamba na hilo watoa huduma ya kubashiri wameachwa wajisimamie na kujiongoza vile wanavyoona inafaa jambo ni hatari sana kwa taifa letu. Michezo casino online kama vile AVIATOR, AVIATRIX na mingine ya aina hiyo ifanyiwe uchunguzi ili kubaini fairness yake kwa watumiaji huduma.

Michezo hii inachota mamilioni ya watumia huduma kila siku tofauti na nafasi za ushindi zinazotolewa. Serikali kuendelea kuangazia kodi tu bila kujali madhara kwa umma wa watanzania ni kulikosea taifa.
 
Hawawezi kuwakazia kwasababu wanapokea pesa nyingi kutoka kwenye makampuni haya ya kamari
 
watu wazima addictions zao wageuzie kampuni utadhani wao ni watoto

Labda uniambie kwa wote under 18,ila ni majitu mazima yenye miaka zaidi ya 18 na ya mvi

Yaani
 
Back
Top Bottom