Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekula au kunywa sumu

Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekula au kunywa sumu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mtu akila sumu (poisoning by mouth) anahitaji kufanyiwa huduma ya kwanza haraka sana. Sumu iliyoingia tumboni inaweza ikapunguzwa nguvu kwa kunywa maziwa Fresh au maji mengi. Halafu mgonjwa ashawishiwe kutapika.

Kuna njia za kuweza kumfanya atapike. Unaweza kumtia kichefuchefu kwa kumpa bilauri ya maji ya moto yaliyotiwa hamira (backing powder), ama yaliyotiwa povu la sabuni (soapsuds). Kama anakataa anyweshwe kwa nguvu.

Baada ya kumpa maji hayo na akawa hatapiki, kumtekenyatekenya kwa vidole nyuma ya shingo yake au mbele kooni kunaweza kumtapisha. Baada ya kutapika apewe bilauri ya maziwa yaliyotiwa kijiko kimoja kidogo cha chumvi ya haluli (epsom salt).

Mchanganyiko huo hupambana na sumu (antidote) na kumletea nafuu aliyekula sumu za aina nyingi. Kama inaonekana mgonjwa anapoteza fahamu, ama kupatwa na shock, yafaa atiwe joto mwilini kwa kumpa kahawa, chai au kinywaji kingine cha moto.

Mkimbize mgonjwa hospitali haraka kwa matibabu zaidi.
 
Ila mtoto akinywa mafuta ya taa kamwe huruhusiwi kumtapisha kwasababu yanaweza kuingia kwenye mapafu na kusababisha madhara zaidi.Asante
 
Back
Top Bottom