kiben10
JF-Expert Member
- Apr 28, 2018
- 613
- 791
Kuna uwezekano nyoka akawa mwenye sumu au asiwe mwenye sumu,mgojwa kupoteza fahamu au kushindwa kupumua vizuri.Kama una uhakika kuwa nyoka aliyehusika hana sumu basi mtibu mgonjwa kwa kutumia njia za kawaida za kutibu vidonda (Note,kama una uhakika).
Katika nyakati ambapo mtu anakuwa hana uhakika wa aina ya nyoka aliyehusika (au kama ni moja kwa moja nyoka mwenye sumu ) basi hatua zifuatazo zifanyike;
1-Utambue muonekano wa nyoka huyo (kama ameonekana) ili uweze kueleza kwa wataalamu wa afya2
-Mlinde mgojwa kwa kufanya yafuatayo
-Muelekeze mbali na eneo ajali ilipotokea
-Mlaze chali huku usawa wa kifua ukiwa juu (unaweza kumuwekea mto mgongoni)
-Mtulize mgojwa pia muondolee wasiwasi ili kupunguza msukumo wa damu unaoweza kupelekea usambazwaji wa sumu husika kwa kiwango kikubwa
-Mtolee viatu na soksi (kama ameng'atwa mguuni)
-Funika kidonda kwa kitambaa au bandage safi
-Mfunge mgonjwa na kitambaa au nguo sehemu ya juu kidogo na usawa alipong'atwa ili kuzuia usambaaji wa sumu mwilini
-Mpeleke hospitali mara moja kwa matibabu zaidi
VITU AMBAVYO HUTAKIWI KUFANYA
-Kuchanja au kuikata na kitu chochote sehemu iliyong'atwa na nyoka
-Kujaribu kuifyoza damu au sumu iliyopo kwenye kidonda kwa kutumia mdomo
-Kuiosha sehemu husika kwa maji au barafu
-Kumpa mgonjwa pombe au kinywaji chochote chenye kemikali ya caffein kama vile soda au kahawa
-Kumnywesha mgojwa dawa yoyote hata ya kupunguza maumivu (paracetamol au aspirin)
MUHIMU
Kuna baadi ya nyoka wana sumu kali kama vile venom phosphokinase na nyingine nyingi zisizoharibiwa wala kutibiwa kwa matibabu ya kawaida (inakuwa hai hadi nyuzi joto 100°C ) hivyo ni bora kumpeleka hospitalini kabla ya kufanya hatua yoyote ya matibabu.
#Afya_info
@dr.mpoto_jr
[HASHTAG]#YourPartinerInHealth[/HASHTAG]