DR HAYA LAND
JF-Expert Member
- Dec 26, 2017
- 23,928
- 63,499
kung'oa ni hatua ya mwisho endapo matibabu yote yameshindikana.Dawa ya jino korofi ni kung'oa tu, nimejikuta ndani ya mwezi wa 12 nimetumia zaidi ya 90 elfu kununua kila dawa ninayoambiwa itanisaidia lakini ndio kwanza likianza kuuma linauma mpaka napoteza hata usikivu, leo nimelitolea mbali, hapa nauguza pengo
E bhana weee dawa ya jino ni kung'oa tukung'oa ni hatua ya mwisho endapo matibabu yote yameshindikana.
Maumivu ya jino yasikie kwa jirani tu, halafu lilivyo na nongwa, linapendelea kuuma usiku mwingi, mchana unaweza ukawa fresh kabisa ila ukijichanganya tu, usiku kazi ipo.
Utotoni mpaka leo nishatoa jino kama mara 5 hivi, na kuna mawili yana matobo, nafikiri kuziba na kufanya root canal, nibaki na meno yangu, ama unashauri nini dr?