Huduma ya M- -Pesa imekufa

Huduma ya M- -Pesa imekufa

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,207
Reaction score
13,839
Kwa siku tatu sasa huduma ya Mpesa imekufa!

Tokea jumamosi nimekuwa nikijaribu kutumia huduma hii bila mafanikio.
Cha kushangaza waendeshaji wa huduma hiyo wako kimya as if kila kitu kiko sawa!

Wadau ni mimi tu au kuna wengine wenye tatizo kama langu?
 
ni kila mtu mkuu - it is a disaster!! wasijegeuka DESI. wataumiza wengi. haijawahi tokea kwa M-PESA kuwa hivi na wao kukaa kimya zaidi ya kusema wanarekebisha tatizo la ufundi.

Jana TIGO nayo ilikuwa na usumbufu lakini sio MPESA ambayo iko KAPUT.
 
Kuna uhusiano gani wa M-PESA na ITV, CHANNEL 5 & TV1? maana nazo leo ni siku ya 3 hazipatikani kupitia kisimbusi cha Star times...
 
Kwa siku tatu sasa huduma ya Mpesa imekufa!

Tokea jumamosi nimekuwa nikijaribu kutumia huduma hii bila mafanikio.
Cha kushangaza waendeshaji wa huduma hiyo wako kimya as if kila kitu kiko sawa!

Wadau ni mimi tu au kuna wengine wenye tatizo kama langu?

Na mimi pia nimepata tatizo hilo, ila sasa hivi wamenipa taarifa kupitia sms kuwa nisiwe na wasiwasi, hela ziko salama.
 
Na mimi pia nimepata tatizo hilo, ila sasa hivi wamenipa taarifa kupitia sms kuwa nisiwe na wasiwasi, hela ziko salama.
Hela kuwa salama na upatikanaji wa huduma ni vitu viwili tofauti.

Waeleze kuhusu huduma.
 
Na mimi pia nimepata tatizo hilo, ila sasa hivi wamenipa taarifa kupitia sms kuwa nisiwe na wasiwasi, hela ziko salama.

Dah afadhali maana mabilioni niliyoyaweka kwenye sim yakipotea itakuwa hatari
 
hata wakipotea mwezi mzima,ili mradi wakirudi nikute pesa zangu kwa mpesa tu
 
Hela kuwa salama na upatikanaji wa huduma ni vitu viwili tofauti.

Waeleze kuhusu huduma.
Hili ni tatizo kubwa sana .
Na Regulator wa huduma hii haijulikani kama ni BOT(Benki Kuu) au TCRA, maana usipopata huduma hii ambayo ni sawa na huduma ya mawasiliano kibenki, waweza poteza maisha.
Tsh 20,000 tu asipopata mtu kijijini kutatua tatizo kwa mfano dawa muhimi twaweza kumpoteza mtu.
Pili sijui huduma isipopatikana kwa wakati ule tunapoihitaji , tushitaki na kupata haki zetu kwa sheria ipi?
 
at last vodacom wametuma sms ya kuomba radhi na kuwa fedha zangu ziko salama nisiwe na wasiwasi
 
Toka Jumamosi Juzi nilikuwa naumwa nataka pesa naambiwa technical problem try again later!! nikaondoa aibu maana mfica maradhi...nikakopa kwa jirani nikanunua dawa ,Jumapili yote mchezo ule ule,nauli ya dalala kwenda sina!! nikakopa tena nikijua Jtatu mambo yatakuwa fresh..... ooooh nimeganda hapa posta naishi CHANIKA nauli na kodi ya Meza nipata wapi?? NIMEKWAMA HAPA CJUI NTAONDOKAJE!!
 
Sijawahi kuamin kabisa kutunza pesa kwenye laini yyt ile.
Nikitumiwa naitoa fasta,km ni kias kikubwa napeleka bank
km haizid alfu hamsini,juc keep in my pocket
 
wametuaibisha kwa kweli mi nilifanya booking sasa nataka nilipie kila nikijaribu inazingua itabid kesho nidamke niende mpaka ofisi za fastjet mjiniiii nikalipe usumbufu wa kijinga huu
 
Back
Top Bottom