Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kulalamika kuwa Wakazi wa Kijiji cha Kemakorere, Kata ya Nyarero Wilayani Tarime wana changamoto ya kukosekana kwa huduma ya maji kwa muda wa zaidi ya miezi miwili sasa, hatimaye huduma imerejea.
Aidha, Mdau alidai kuwa Ofisi za Wakala wa Maji na usafi Mazingira Vijijini (RUWASA) zilizopo kijijini hapo zimekamilika muda mrfefu lakini hazitumiki licha ya kuwa majengo yana ubora na yamekamilika.
Hoja ya Mdau bofya ~ Wakazi wa Nyarero- Tarime hatuna maji mwezi wa pili sasa, RUWASA wametelekeza Ofisi
SERIKALI ZA MTAA WAKIRI CHANGAMOTO YA MAJI
Mwenyekiti wa Kemakorere, Chacha Manga amesema “Ni kweli kulikuwa na changamoto ya maji, hakukuwa na huduma ya maji kwa muda wa wiki mbili, tulipokuwa tunauliza tulisikia wanasema kuna tatizo la umeme.
“Ilidaiwa ukosefu wa umeme ulisababisha maji yashindwe kupanda kuingia kwenye mabomba, ila kwa sasa maji yamerejea.”
Kuhusu majengo ya RUWASA ambayo hayatumiki licha ya kukamilika, Mwenyekiti anasema “Ofisi imejengwa pale kwenye tenki lakini sijui tatizo ni nini, hakuna wahudumu pale, tukiwa na shida tunapiga simu wanasema wanakuja lakini kukaa pale ofisini hawakai licha ya kuwa majengo yapo na ni mapya.”
RUWASA WATOA NENO
Alipotafutwa Meneja wa RUWASA Tarime, Mhandisi Malando S Masheku amesema “Maji yalikatika siku moja kutokana na changamoto ya umeme na sasa huduma zinaendelea kama kawaida.”
Ameongeza “Mradi wa Kemakorere unahudumiwa na CBWSO ya INCHAGE, ambayo inasimamia Miradi ya Magoma, Nyamwigura, Morega A, Magoto, Kebweye na huu wa Kemakorere.
“Mpaka sasa mradi huu wa Kemakorere unafanya kazi na tayari tuna house connection 102.
“Kuhusu Ofisi, ni Ofisi ya CBWSO inafanya kazi na mafundi wapo muda mwingi kuunganishia maji majumbani.”