Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 590
- 807
- MAFANIKIO YA MIAKA MITATU YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA
-
- A). Huduma ya majisafi na salama vijijini na mijini imeimarika
- Vijijini kutoka wastani wa 77% Desemba 2022 hadi 79.6 Desemba, 2023
- Mijini kutoka wastani wa 88% Desemba, 2022 hadi 90% Desemba, 2023
Wizara ya Maji imefanikisha malengo ya programu ya PforR (Lipa kwa Matokeo) kwa muda uliopangwa kwa kuvuka lengo la idadi ya wanufaika kutoka watu milioni 3 hadi milioni 4.07,
Benki ya Dunia imeitambua Tanzania kuwa ya nchi ya kwanza kati ya nchi zaidi ya 50 duniani zilizofanya vizuri katika utekelezaji wa Programu ya PforR kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo. Mafaniko hayo yamesaidia kuongezeka kwa fedha za utekelezaji wa programu kutoka Dola za Marekani milioni 350 hadi Dola za Marekani milioni 654 na kuongeza mikoa inayonufaika kutoka 17 hadi 25 na Halmashauri kutoka 86 hadi 137.
MIRADI YA KIMKAKATI YA WIZARA YA MAJI ILIYOKAMILIKA NA INAYOENDELEA
MIRADI YA MAJI YA KIMKAKATI ILIYOKAMILIKA NCHINI
Wizara ya Maji imekamilisha miradi mikubwa na ya kimkakati ikiwemo mradi wa maji Arusha ambao umeongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 40 hadi lita milioni 200 kwa siku na muda wa upatikanaji wa huduma ya maji kutoka saa 12 hadi saa 24 kwa siku pamoja na mradi wa maji wa Butimba unaonufaisha wakazi wapatao 450,000 katika Jiji la Mwanza. Aidha, Mradi wa ujenzi na uboreshaji wa mtandao wa majisafi Nzuguni (Awamu ya kwanza) umekamilika na unanufaisha wakazi 75,968.
B.MIRADI YA MAJI YA KIMKAKATI INAYOENDELEA KUTEKELEZWA NCHINI
| MKOA | MRADI | GHARAMA | LENGO | WANUFAIKA | UTEKELEZAJI |
| ARUSHA | Mradi wa majisafi Oldonyosambu | TZS 6,382,532,295.20 | Kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi | wakazi wapato 29,449 | 47% |
| Mradi wa majisafi Mageri-Ngorongoro | TZS 6,105,995,066.21 | Kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi | wakazi wapato 33,969 | 52% | |
| DAR ES SALAAM & PWANI | Mradi wa Ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji kutoka visima virefu vya Kimbiji | TZS 21,278,706,991 | Kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi | Wakazi 250,000 | |
| Mradi wa ujenzi wa mtandao wa mabomba ya maji Kimbiji – Kigamboni kutoka kwenye tanki la Kimbiji | TZS 8,000,000,000 | Kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi | Wakazi wa Kimbiji | 75% | |
| Mradi wa Ujenzi wa mtandao wa usambazaji maji na Matenki ya kuhifadhia ya maji Kusini mwa Dar es Salaam | TZS 35,149,404,125 | Kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi | Wakazi 450,000 | 19% | |
| Mradi wa usambazaji majisafi maeneo yaliyo nje ya Mtandao | TZS 22,079,079,033 | Kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi | Wakazi 215,380 | 96% | |
| DODOMA | Mradi wa ujenzi na uboreshaji wa mtandao wa majisafi Nzuguni (Awamu ya pili) | TZS 5,509,671,097 | Kuboreshaji mtandao wa majisafi Nzunguni | Wakazi wapatao 80,000 | |
| Mradi wa upanuzi na uboreshaji wa huduma ya majisafi Dodoma na Chamwino | TZS 4,181,321,572.74 | Kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi | Wakazi 150,000 | 40% | |
| MWANZA | Mradi wa kupanua mtandao wa usambazaji maji katika miji ya Magu na Misungwi | TZS 1,939,814,086.65. | Kupanua mtandao wa usambazaji maji. | Wakazi wa Magu na Misungwi. | 70% |
| Mradi wa kuboresha mfumo wa usambazaji maji katika Jiji la Mwanza | TZS 4,624,246,101.32 | Kuboresha mfumo wa usambazaji maji. | Wakazi wapatao 33,000. | 70% | |
| Mradi wa kuboresha mfumo wa usambazaji maji eneo la Ilemela jijini Mwanza | TZS 405,640,707.20. | Kuboresha mfumo wa usambazaji maji. | Wakazi wapatao 12,000. | 70% | |
| MBEYA | Mradi wa kuboresha huduma ya majisafi katika Jiji la Mbeya kwa kutumia chanzo cha Mto Kiwira | TZS 99,659,532,284. | Kuboresha huduma ya majisafi. | Wakazi 1,452,751. | 11% |
| Mradi wa kuboresha huduma ya majisafi katika Kata za Mwansekwa na Iganzo.(Kipande cha 1 na 2) | TZS 5,200,000,000. | Kuboresha huduma ya majisafi. | Wakazi wapatao 42,000. | Kipande cha 1-90% Kipande cha 2-76%. | |
| MARA | Mradi wa Maji Mugango,Kiabakari na Butiama. | USD milioni 30.69 | Kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji. | Zaidi ya wakazi 100,000 | 98% |
| KILIMANJARO-TANGA | Mradi wa Maji Same, Mwanga na Korogwe | Kuboresha huduma ya maji. | Wananchi 456,931 | 86.7% | |
| SIMIYU | Mradi wa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi | TZS bilioni 444.6 | Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi katika Wilaya za Busega, Bariadi, Itilima, Maswa na Meatu | Wananchi 662,500 | 4% |
Wizara imeanza utekelezaji wa mkakati wa Gridi ya Taifa ya Maji kwa kutumia vyanzo vikubwa vya maji vya uhakika ikiwemo maziwa, mito na mabwawa kwa ajili ya kupeleka maji kwenye maeneo ambayo hayana vyanzo vya uhakika. Kwa mfano; mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria ambao umenufaisha miji ya Kahama, Shinyanga, Tinde, Nzega, Tabora, Igunga na Shelui pamoja na vijiji vilivyopo ndani ya kilomita 12 kutoka kwenye bomba kuu. Pia, mradi wa kutoa maji Ziwa Tanganyika kupeleka kwenye mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi, ambao upo kwenye hatua ya usanifu;
Wizara ya Maji imeanza utekelezaji wa miradi ya maji ya kimkakati ikiwemo mabwawa ya Kidunda na Farkwa pamoja na Mradi wa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi – Simiyu.
Wizara ya Maji imekwamua miradi 157 kati ya miradi 177 ya maji vijijini iliyokuwa na changamoto ya kutokukamilika kwa muda mrefu.
Wizara imefanikisha kuimarisha mazingira ya kazi kwa kukamilika na kuanza kutumika kwa jengo jipya la ofisi za Wizara lililopo Mtumba pamoja na ununuzi wa vitendea kazi ikiwemo magari, pikipiki na kompyuta;
Wizara ya Maji imendelea na utekelezaji ujenzi wa miradi ya maji katika miji 28 ambapo utekelezaji upo katika hatua mbalimbali.
- MIRADI YA MAJI MIJI 28 INAYOTEKELEZWA
KIPANDE | ENEO/MIJI | UTEKELEZAJI |
| 1 | Handeni, Korogwe, Muheza na Pangani | 30% |
| 2 | Kilwa Masoko na Nanyumbu | 28% |
| 3 | Ifakara, Rujewa, Chunya, Njombe, Makambako na Wanging’ombe | 9% |
| 4 | Kiomboi, Singida, Manyoni, Mugumu, Chemba na Chamwino | 9% |
| 5 | Kasulu, Mpanda, Sikonge, Urambo na Kaliua | 40% |
| 6 | Kayanga, Chato na Geita | 10% |
| 7 | Newala, Nanyamba, Tandahimba na sehemu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara | 24% |
| 8 | Mafinga | 17% |
| 9 | Miji ya Rorya na Tarime | 13% |
| 10 | Mji wa Songea | 3% |
Wizara ya maji imekamilisha ujenzi wa mabwawa 12 ya ukubwa wa kati na madogo ya kuvuna maji ya mvua kwenye maeneo mbalimbali nchini yenye uwezo wa kuhifadhi maji lita bilioni 1.86. Uwepo wa mabwawa hayo unaongeza uhakika wa maji nchini (water security).
Wizara ya Maji imekamilisha uchimbaji wa visima 283 kutokana na matumizi ya seti 25 za mitambo ya kuchimba visima na seti tano (5) za mitambo ya ujenzi wa mabwawa vilivyonunuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wizara ya maji kwa kutumia mitambo ya uchimbaji wa visima na mabwawa imefanikiwa kusaidia kukabiliana na janga la maafa yaliyotokea Hanang’ mkoani Manyara kwa kuchimba visima nane (8) na kurejesha huduma ya maji kwa wananchi ndani ya saa 48.
Wizara ya Maji imefanikisha kuchimba visima na mabwawa yanayohudumia wananchi waliohama kutoka Ngorongoro kwenda Msomera.
Kuimarika kwa usimamizi wa Jumuiya za Watumiamaji (CBWSOs) ambapo kwa mara ya kwanza katika mwaka 2022/23, Wizara kupitia RUWASA imeziwezesha CBWSOS 136 kuandaa Vitabu vya Hesabu (Financial Statements) za mwaka 2023/24 na kukaguliwa na CAG. Kati ya hizo, CBWSOs 133 sawa na asilimia 98 zimepata Hati safi. Vilevile, katika kuimarisha udhibiti wa mapato ya fedha za umma, CBWSOs 661 zimejiunga katika Mfumo wa GePG na kuanza kukusanya mapato ya mauzo ya maji kupitia mfumo huo.
VIPAUMBELE NA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2024/25
Wizara imeweka vipaumbele ambavyo vitazingatiwa katika mpango na bajeti ya mwaka 2024/25 ili kufikia lengo la kuwapatia huduma ya maji safi na salama kwa zaidi ya asilimia 85 ya wananchi wa vijijini na zaidi ya asilimia 95 ya wakazi wa mijini. Utekelezaji wa vipaumbele, utazingatia majukumu ya Wizara yakiwemo kuimarisha usimamizi, uendelezaji, uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya maji; kuimarisha na kusimamia huduma za ubora wa maji. Vipaumbele hivyo ni kama ifuatavyo:-
Kukamilisha utekelezaji wa miradi inayoendelea na kuendelea na ujenzi wa miradi mikubwa;
Kuongeza kasi ya uvunaji wa maji ya mvua kwa kujenga mabwawa ya ukubwa wa kati na mabwawa ya kimkakati;
Kufikisha huduma ya maji kwenye vijiji ambavyo havina huduma;
Kukamilisha uandaaji wa Mpango Kabambe wa Taifa wa Maji (Water Master Plan), Mtandao wa Taifa wa Kusambaza Maji (National Water Grid) na mapitio ya Sera ya Taifa ya Maji;
Kupunguza upotevu wa maji;
Kuongeza kasi ya ufungaji wa dira za malipo kabla ya matumizi ya maji (prepaid meters);
Kuongeza kasi ya uwekezaji kwenye usafi wa mazingira; na
Kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika uwekezaji na uendeshaji wa skimu za maji.
USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA MAJI
Wizara itaendelea kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa mwenendo wa rasilimali za maji kwa kukarabati vituo 100 vya usimamizi wa rasilimali za maji; kutoa vibali 600 vya matumizi ya maji; kuunda jumuiya 18 za watumia maji; na kuunda kamati tisa (9) za vidakio vya maji.
USIMAMIZI WA HUDUMA YA UBORA WA MAJI
Wizara itaendelea kufanya tathmini na ufuatiliaji wa ubora wa maji katika vyanzo vya maji 2,200, mifumo ya usambazaji maji 8,245 vijijini na mijini, na mifumo 150 ya majitaka.
Wizara imepanga kuweka mifumo ya ukusanyaji na utunzaji wa takwimu na taarifa za ubora wa maji; kuendelea na utekelezaji wa mkakati wa kupunguza madini ya flouride kwenye maji ya kunywa na ya kupikia; na kuwezesha uandaaji na ufuatiliaji wa utekelezaji wa mipango ya usalama wa maji katika mamlaka za maji 40 na CBWSOs 120.
Wizara itaendelea kuziboresha maabara za maji kwa kuzipatia vitendea kazi na kuziwezesha kupata na kudumisha hadhi ya ithibati katika viwango vya kimataifa.
HUDUMA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI
Wizara imepanga kuendelea kutekeleza jumla ya miradi 1,054 ya usambazaji maji vijijini katika maeneo mbalimbali. Aidha, kwa vijiji ambavyo havijafikiwa na huduma ya maji, Serikali imepanga kuchimba visima vitano (5) katika kila jimbo la uchaguzi kwenye maeneo ya vijijini na kwa kuanzia, Wizara itaanza na uchimbaji wa visima 900.
Wizara itaendelea kubadili mitambo inayotumia dizeli na kuweka umeme wa gridi ya taifa au nishati ya jua ili kupunguza gharama za uendeshaji wa skimu za maji; kuimarisha usimamizi wa mauzo ya maji na makusanyo kwenye CBWSOs kwa kufunga dira za malipo kabla ya matumizi (prepaid meters); kuweka mfumo wa pamoja wa utunzaji wa kumbukumbu za wateja na uandaaji wa ankara (Unified Maji Billing System); na kujiunga kwenye mfumo wa makusanyo ya fedha za umma (GePG).
Wizara itaendelea kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi katika utoaji wa huduma ya maji, kuzijengea uwezo CBWSOs 1,382 na kuendelea kuziunganisha CBWSOs ili kuimarisha uwezo wa kujiendesha.
HUDUMA YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MIJINI
Wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo pamoja na sekta binafsi imepanga kutekeleza jumla ya miradi 245 ya maji kwenye maeneo ya mijini. Baadhi ya miradi itakayoendelea kutekelezwa ni mradi wa ujenzi wa miundombinu ya kutoa maji Mto Kiwira kwenda Jiji la Mbeya; mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi Simiyu; mradi wa kutoa maji Mto Ruvuma kwenda Mtwara; mradi wa kutoa maji Mto Rufiji kwenda mikoa ya Dar es Salaam na Lindi; na mradi wa maji wa miji 28. Vilevile, Wizara imepanga kuendelea na ujenzi wa miradi ya uondoshaji wa majitaka katika miji mikuu ya mikoa, miji mikuu ya wilaya na miji midogo.
KUIMARISHA UTOAJI WA HUDUMA YA MAJI NA KUPUNGUZA UPOTEVU WA MAJI
Wizara imepanga kuboresha utoaji wa huduma ya maji kwa kudhibiti bei za maji, kuondoa migawo ya maji, kuunganishia wateja huduma ya maji kwa wakati na kupunguza malalamiko ya wananchi yatokanayo na huduma ya maji. Katika kufikia azma hiyo, Wizara imepanga kusimamia ufungaji wa dira za maji za malipo kabla (prepaid water meters) na kuendelea kuboresha mfumo wa pamoja wa ankara za maji (Unified Maji Billing System). Lengo ni kupunguza kiwango cha maji yanayopotea kutoka wastani wa asilimia 35.3 hadi kufikia kiwango kinachokubalika kimataifa cha asilimia 20