Huduma za kibingwa na kibobezi za MOI zavutia wananchi maonesho ya 50 ya kibiashara ya Sabasaba

Huduma za kibingwa na kibobezi za MOI zavutia wananchi maonesho ya 50 ya kibiashara ya Sabasaba

Taasisi ya Mifupa-MOI

Senior Member
Joined
Apr 15, 2025
Posts
118
Reaction score
214
Huduma za kibingwa na kibobezi za Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) zimeendelea kuvutia wananchi katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba).

Kupitia maonesho hayo, MOI imesogeza huduma karibu zaidi na wananchi kwa kuendesha kliniki maalum ya matibabu inayotolewa na madaktari bingwa na wabobezi. Huduma zinazotolewa ni pamoja na uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya mifupa, ubongo, uti wa mgongo, mishipa ya fahamu na magonjwa ya ndani.

Aidha, wananchi wanapata huduma za ultrasound, mazoezi tiba (physiotherapy), tiba lishe, huduma za dawa pamoja na elimu kuhusu huduma zinazotolewa MOI, hivyo kuwapa fursa ya kupata ushauri na matibabu bora kwa urahisi katika banda la MOI.

Wananchi wote wanakaribishwa kutembelea banda la MOI katika Viwanja vya Sabasaba ili kunufaika na huduma hizi, ambazo zitaendelea kutolewa kila siku hadi mwisho wa Maonesho hayo tarehe 13 Julai, 2026.

1785504686027.png
MOI NEWS UPDATES 2025-04.jpeg
 

Attachments

  • MOI NEWS UPDATES 2025-02.jpeg
    MOI NEWS UPDATES 2025-02.jpeg
    825.7 KB · Views: 16
  • MOI NEWS UPDATES 2025-03.jpeg
    MOI NEWS UPDATES 2025-03.jpeg
    935.7 KB · Views: 17
Taasisi yenu inahitaji watu wanaonyumbulika ila kwa uchawa nyie ni nyumbu tu
 
Back
Top Bottom