Huduma za matibabu zimeshuka kiwango, zimekuwa mbovu, na ni kero kutokana na maboresho ya bima kwa kushusha bei serikali chukueni hatua

nusu kaputi

Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
54
Reaction score
122
Habari za Leo wananchi!

Hali inayoendelea katika nchi yetu katika HUDUMA afya baada ya kushuswa bei za Bima NHIF kutokana na Maboresha HUDUMA katika hospital zetu zinazidi kuwa mbaya, Hospital zimefunga baadhi ya HUDUMA na kupunguza watumishi wakujitolea.

Hali hii imeanza kuonekana Kwa Kasi hasa kuanzia mwezi Huu July, Hospital kubwa zinasuasua Kwenye HUDUMA za kibingwa kutokana uendeshaji umekuwa ni Changamoto, KCMC imepunguza watumishi, Mbeya nayo hivyohivyo, MoI imeshindwa vifaa vya kutumika Kwenye mifupa vina bei ,bima bei ya chini. Wakinamama kujifungua Kwa operation gharama kushuka Toka 600,000 mpaka 200,000, MNH na BMC wanapasua kichwa uendeshaji wa Hospital, Serikali hakuna hatua yoyote

Wagonjwa wakulipia wanapigwa kweli kweli Ili hizi hospitali ziweze kujiendesha

Mama Samia Hili swala linakuja Kwa Kasi kuchafulia, Washauri wako hawakupendi wanataka uangauke

Katibu wa afya Hafai

Waziri wa afya Angalia hili swala linakwenda kukundosha

Mkurugenzi wa NHIF angefukuzwa ni jipu

Kunauwezekano vifo kuongezea Kwa kukosa HUDUMA

Kizazi kitajicho kuasilika na usugu wa Dawa Kwa maana Maduka ya Madawa yakageuka kuwa hospital,
Hospital kulipisha bill kubwa wagonjwa Ili kujiendesha

HUDUMA Kwa mteja inaenda kufa, majibu tunayoyaona Tunaoenda kutibiwa majibu ni ovyo Kwa sababu watumishi wa afya Hawana motisha

Mungu inusulu nchii hii imekuwa kipofu

Pia soma:ACT Wazalendo: Vitita vipya NHIF vinageuza huduma ya afya kuwa biashara, Serikali ifute vitita vipya
 
Hii ni kweli hata hospitali private zinasua coz NHIF haijapeleka pesa huko za bima karbia miezi 5.
 
Wanataka tufe wote wabaki wao tu na familia zao ili wajinafasi vizuri.
Halafu ngoja waendelee tu kuwachokoza watu, iko siku uvumilivu utaisha na cha moto watakiona.
 
Ni kweli kiwango cha huduma za afya nchini kipo chini sana, hii ni kuanzia kwenye uwezo wa kitaalam wa madaktari, wataalam wa maabara mpaka wauguzi.

Serikali irudishe utaratibu wa kuwapeleka wataalam kwenda kupata mafunzo nje ya nchi hasa kwenye specialization, na kwenye vipimo maalum vya maabara. Mpaka sasa kwa hospitali kubwa zote madaktari wanaoonekana kumudu vyema kazi zao unakuta wengi wao ni wazee na hao walipata mafunzo nje ya nchi.

Viwango vya malipo ya bima viangaliwe kwa umakini mkubwa. Vikiwa vidogo sana, hospitali hazitaweza kugharamia mafunzo ya wataalam, ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa na vyenye ubora, ununuzi na utoaji wa madawa bora yenye gharama kubwa, na wala hazitaweza kutoa malipo mazuri kwa watendaji kazi wake; na hata hazitaweza kupanua na kuongeza huduma kwa urahisi.

Hospitali nyingi nchini, ukishuhudia ubora wa huduma zinazotolewa, japo zinaitwa ni hospitali, kiuhalisia zimekuwa kama vituo vya afya. Zimekuwa hospitali majina, kwa sababu ya kukosa watu wenye ujuzi mahiri. Kuna wakati inakuwa ni nafuu upate ushauri kupitia online doctors waliopo nje ya nchi kuliko doctor unayekutana naye ana kwa ana, ambaye yupo nchini, japo kiuhalisia kuna mazingira ambayo online doctor hawezi kuwa na masaada wowote, mgonjwa anahitaji huduma ya daktari ambaye yupo na mgonjwa.

Ingawa nchi imeshindwa katika.mengi, basi angalao tungramua tuwekeze heavily kwenye tiba. Itawasaidia wananchi wetu, itatoaajira kwa vijana wetu, itaingiza pesa nyingi za kigeni toka nchi jirani, na itaongeza tekinolojia ya tiba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ummy yupo busy na posho peke
 
Asee kama ni kweli tumeisha
 
Bima kuwa gharama nafuu na matibabu kushuka bei ni muhimu kwa mwanachi kupata access ya huduma za afya kwa kuwa na uwezo wa kuzimudu.

Serikali inatakiwa kutenga na kuchangia fedha za kutosha kwenye huduma za afya ili kuboresha miundombinu na kucover fedha zinazotakiwa baada ya kushusha bei ya bima na gharama za matibabu.
 
Serikali hasa Ummy ni wapiga dili
 
Unaposhusha bei hakikisha hata bei ya soko ya hizo Dawa zimeshuka,Vifaa vimeshuka,Umeme umeshuka,ushuru umeshika, material ujenzi yameshuka,maji yameshuka(◍•ᴗ•◍)Dollar imeshuka ,
Ili mteja wa Bima apeta HUDUMA stahili.
Kwa ujumla ni kwamba hii nchi tumewapa vibaka Kwenye vitango Muhimu ,
Hata Raisi Hana washauri wa maana. Ukichezea afya za watu umeharibu Kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…