Huduma za VVIP na malipo kwa viongozi wa majeshi na wastaafu ziwe kwa watumishi wote wa umma au zifutwe

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Kuna huduma za chini chini kwa baadhi ya viongozi wa majeshi ukizitazama siyo afya kabisa kwa matumizi bora ya kodi!

Sasa hivi nchi inalalamika kuwa deni la taifa limefikia tirioni 96

Lakini kuna hizi mambo kwa baadhi tu ya watu lakini wengine wanalia na njaa

  • Kuna haja gani wakuu wa majeshi wastaafu kulipwa 80% ya aliyepo madarakani wakati walitumikia nchi na kulipwa mafao yao yote kwa mkupuo?
  • Kuna haja gani, au walitumia vigezo gani kwamba kila baada ya miaka minne magari ya wastaafu yanakuwa yamrchoka kwamba wanahitaji kupatiwa mapya 0KM Kila baada ya miaka 3 au 4? Wakati jamii haina ambulance
  • Kuna sababu gani misiba yao na wastaafu inahudumiwa na serikali halafu misiba ya watumishi wengine wa umma tunahangaika kuchangishana walala hoi mtaani?
  • Kuna haya mabasi mapya yamenunuliwa na kusambazwa nchi nzima kwa ajili ya kuwafuata watumishi wa majeshi majumbani na kuwarudisha; Je ni kweli nchi yetu inautajiri huu wa bajeti?
  • Kuna mashangingi kama zawadi ya kuendea saloon kwa wake wa ....... Hili nalo linamaanisha nini katika matumizi!
Mbona hawa watu wana mishahara mikubwa tu hizi huduma nyingine VVIP kama ni mhimu kwanini isifanyike kwa watumishi wote wa uma?

Na hapo sijagusia malipo ya nafasi zingine kama
  • Spika na spika wastaafu
  • Majaji na wakuu wengine wa idara
  • na idara zingine!

Kwamba kuwe na mabasi ya watumishi wa taasisi zingine pia!

Yaani mfano: kuwr pia na mabasi ya walimu mtaani, walimu wakifariki hata kama wamestaafu, ofisi ya mkurugenzi itoe gari na kulipia gharama kama huko majeshi wanavyotoa mabasi na helkopita!
 
Unajifanya una uchungu na Nchi kumbe roho mbaya imekutawala..
 
Sasa hivi hadi wenza wao (wake au waume) zao wanalipwa
 
Ukisikia keki ya uzalendo ndio hiyo siyo kuandamana wala kumtukana raisi!
 
Umeeleza kwa maumivu sana, ila zora tu hakuna namna asee.
 
Shida ipo wapi hapo..mtu ametumikia hadi cheo cha mkuu wa majeshi kwa uaminifu mkubwa then aachwe adhalilike unajua hiko cheo kinalingana na cheo gani uraiani?

Mkuu wa majeshi akiamua kuchukua nchi ni dakika 10 tu ila wanaheshimu democsia zetu uchwara hizi maana ni bora kuliko utawala wa kijeshi..
acheni tu wapewe shukrani.
 
Wanakamatwa kwa sababu ni wazee ili nchi itulie
 
Tukiuliza tunaambiwa hata vidole havifanani, tufanyeje sasa wakati sisi Gen Z zama zimetupita.
 
Kama kila mtumishi wa umma atapata huduma ya VVIP akiwa katika utumishi wa umma na baada ya kustaafu huoni kuwa pesa zote za nchi zitatumika kuhudumia watumishi pekee?
Hata hivyo hazitatosha
Cha muhimu kila mtumishi alipwe vizuri kiasi na akistaafu habari zake ziishie papo hapo bila kujali cheo cha mtu. Kila mmoja atumie mshahara wake kujijenga na kujiandalia mazishi yake baada ya kustaafu.
 
Tanguliza HESHIMA kwanza kwa amani .ulio nayo mpaka ukaandika haya. Ungeweza kuandika haya kweny Ardhi ya Gaza ? Walipo ishia Jeshi la Mungu waendeleee ifike 100kabisa. Jambo Afande.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…