Tetesi: Huenda chama kipya cha Lissu kikasheheni watu waadilifu kama Dkt. Slaa, Prof. Safari, Mnyika, Heche, Wenje na wale wote waliotoka CHADEMA kwa figisu

Wasalaam, JF.

Wakati Tundu AM Lissu akiamua kuasisi chama kipya cha siasa na kuifanya Tanzania kuwa na jumla ya vyama 20 vya siasa akianzia kukisimika chama hicho kipya mkoani kwake Singida kabla ya kuanza harakati Tanzania nzima.
Hii agenda ya cdm na Mbowe mmeishikia bango Sana na Nina uhakika dau limeongezeka kutoka buku 7 Hadi 30 kwa kila Uzi wa kuichapa cdm na Mbowe!

Watanzania ni watu werevu kwa sasa na siyo wajinga wasiojua mbinu za ccm zilizopitwa na wakati. Wanajua mnahamisha goli la bahari na madini kupewa mkorea. Wanajua jinsi dp world alivyosababisha gharama za makontena kuongezeka.

Wanajua jinsi mnavyogawana vibali vya kuagiza sukari na kuifanya iwe bei juu!
Na wewe mleta Uzi ni kijana Tena under 40 na unashabikia ujinga wa raslimali za taifa kugawiwa Kama njugu za kuonjesha. Be ashamed!
 
CCM ni chama chepesi sana kukitoa madarakani ni vile upinzani wamejaa mabwege nazi tu.
 
Hakika njuka umejipanga na hadithi zako!

Bado hatujasikia ongeza mapambio!
 
Vyama vya upinzani vipo kuungana na ccm kuwanyonya watanzania
 
Kama hao wote wamekuwepo Chadema,NCCR na CuF na Bado hakuna kitu wamefanya ,Sasa hao wanaharakati ndio watakuwa na jipya gani?
 
just like others,...at the end he will get diluted......
 
Mkuu kumbukumbu ni muhimu sana, ccm kama kutoka madarakani, kwa sanduku la kura ingeshatoka zamani, ukisema katiba hii" umeshitua sana, kilichotokea? uchaguzi wa 2020. Sina hamu ya kuona uchaguzi kwa katiba hii?!!?
 
Mkuu kumbukumbu ni muhimu sana, ccm kama kutoka madarakani, kwa sanduku la kura ingeshatoka zamani, ukisema katiba hii" umeshitua sana, kilichotokea? uchaguzi wa 2020. Sina hamu ya kuona uchaguzi kwa katiba hii?!!?
 
Hii mada haina maana yoyote; imejaa ujinga mwingi hata mingi ya michango yake inaakisi ujinga. Imejaa uongo na mikingamo kibao (paradoxes, contradictions). Wanaodai wananchi wameichoka CCM lakini hawaoni chama makini cha upinzani ni sehemu ya propaganda za CCM kujaribu kete ya mwisho ku-equalize CCM na CHADEMA ili wananchi wasione chaguo bora. Ndio msingi wa ujinga wa mada kama hii.

Ukweli na uhalisia ni kwamba hadi leo hii CHADEMA, kama kilivyo, ndicho chama kikuu, chama makini na chama tishio cha upinzani nchini. Kimekuwa hivyo tangu kabla ya 2010. CHADEMA sio chama cha siasa tu, bali ni jukwaa (platform) la sauti za upinzani wa kweli (voices of dissent) dhidi ya uovu na utendaji mbovu wa serikali. Watumiaji wa jukwaa hilo ni wananchi wa vyama vyote, watendaji wa serikali hata waliomo kwenye vyombo vya dola wanaoona mambo yakienda ndivyo-sivyo. Ndio sababu ya watawala kuiogopa sana CHADEMA kiasi cha kujiapiza mara kwa mara kuiua na baadhi ya viongozi wake virtually and literally.

Kipimo cha ubora wa CHADEMA dhidi ya CCM ni kimoja tu: ni tume huru ya uchaguzi inayolindwa na katiba makini ya kidemokrasia, period. Hadi hapo ndipo Watanzania watakaposema wenyewe kuhusu chama kipi ndio chaguo lao kwenye sanduku la kura. Nje ya hapo, kama ilivyo kwenye mada hii ni kupiga ramli chonganishi!
 
Mkuu kumbukumbu ni muhimu sana, ccm kama kutoka madarakani, kwa sanduku la kura ingeshatoka zamani, ukisema katiba hii" umeshitua sana, kilichotokea? uchaguzi wa 2020. Sina hamu ya kuona uchaguzi kwa katiba hii?!!?
2020 kulikuwa hakuna uchaguzi wenye tija.
Wapiga kura wengi walliukubali utawala wa Magufuli.
Kosa ni kubwa ccm walitaka kufuta upinzani jumla.
Ila ulikuwa uchaguzi ambao hata wasingeiba kura wangeshinda tu.
 
Sikio la kufa halisikii dawa.
Kweli tume ya uchaguzi inakasoro hiyo haipingwi.
Ila kumbuka tume hii hii ndio iliyoleta upinzani 2010 Kikwete chupu chupu na 2015 kujaza kwa wingi wapinzani bungeni.
Unategemea Ccm watakuletea katiba na tume bora ili watoke kirahisi madarakani?
Upinzani unatakiwa kuwa upande wa wananchi na sera za upinzani zieleweke kwa wananchi walio wengi.

Chadema ilikuwa chama kikuu cha upinzani ni kwa ajili ya juhudi za kina Dr Slaa, Mnyika, Zito n.k kupambana kupenyeza agenda zao kwa wananchi hadi vijijini huko. Leo imekuwa One man show.
Gia ya angani ndio anguko la chadema. Walionywa wakawa na matusi bila hoja.
Mbowe na Samia lao moja.
Tusidanganyane, ukweli usemwe chadema ya sasa haipo kwa wananchi, yaani haina tofauti na CCM.
 
Nawasikitikia wasiojua siasa ya hii nchi inapokaribia uchaguzi mkuu, wengi hapa ni wachanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…