Tetesi: Huenda chama kipya cha Lissu kikasheheni watu waadilifu kama Dkt. Slaa, Prof. Safari, Mnyika, Heche, Wenje na wale wote waliotoka CHADEMA kwa figisu

Mengi uliyoandika hapa yanaeleweka sana. Yapo mengi huko CHADEMA yanayotafakarisha sana. Yanatia shaka na kutibua. LAKINI niliyoyawekea rangi nyekundu yanaonyesha kasoro kubwa ya maamuzi na kukosa uhalisia.

Kuhama chama na kumchagua Magufuli 2015 haikuwa uamuzi wa busara. Nachukulia mlihamia CCM. Ulikuwa uamuzi mbaya kwa watu mliokuwa CHADEMA. Tuseme ilikuwa jazba tu. Najiuliza ilikuwaje 2020 msipige kura?

Wengi hatukufurahishwa na ujio wa Lowasa CHADEMA lakini CCM wala Magufuli hawakuwahi kuwa mbadala sahihi katika harakati za kuondoa matatizo ya nchi hii. Hata leo CCM bado ni tatizo kubwa la kitaifa. Labda mlifanya vile kwa vile mlikuwa makada viongozi kwamba kwenu nyinyi siasa ni kazi/ajira. Sisi tusiokuwa hata na kadi tuko huru zaidi kufikiri na kupima.

Mbowe hatutishi wala CHADEMA sio dini kwetu. Bado ina misingi mizuri na makada wa kuaminika sana. Naamini Mbowe wala mtu yeyote hana jeuri ya kubomoa misingi ya chama. Ataondoka yeye.

Halafu hakuna wakati wowote CCM imetishiwa au kuwa hatarini kuondolewa madarakani. 2015 CCM ingeshinda tu tena kwa kishindo hata kama Lowasa asingekuwa mgombea wa CHADEMA. Mbowe aiokoe CCM? Tena ya Magufuli? Dola itakuwa wapi kupanga matokeo ya uchaguzi mkuu?
Tunatofautiana ndugu.
Wewe unapambana na uchaguzi, mimi napambana na halisia.
Kimsingi hatuwezi kufanana.
 
Wasalaam, JF.

Wakati Tundu AM Lissu akiamua kuasisi chama kipya cha siasa na kuifanya Tanzania kuwa na jumla ya vyama 20 vya siasa akianzia kukisimika chama hicho kipya mkoani kwake Singida kabla ya kuanza harakati Tanzania nzima.

Tayari baadhi ya watu waadilifu kama Dkt. Slaa, Prof Safari, Boniface Mwambukusi, John Heche, John Pambalu, Godbless Lema, wanatajwa kuwa Viongozi wa awali wa Chama hicho ambacho bado jina lake halijajulikana.

Mkakati huu unakuja baada ya Katibu Mkuu wa CHADEMA John John Mnyika kukataa kuendelea kukaa ofisi kwa madai kwamba kazi zote za Katibu Mkuu anafanya Mpwa wa Mbowe ndugu John Mrema akisaidiwa na Bw Reginard Mtumishi ambae ni mjomba wa Freeman Mbowe.

Mkakati uliopo leo CHADEMA ni Freeman Mbowe kugombea tena nafasi ya Uenyekiti wa chama kwa mara ya nne mfululizo ukiacha mara mbili alizokuwa mwenyekiti kupitia BAVICHA na kufanya jumla ya mihula yote hiyo inamfanya Freeman Mbowe kuwa na miaka 30 kwenye uongozi wa CHADEMA bila kupisha yoyote kwenye uongozi Chama hicho.

Tundu AM Lissu ndio nembo pekee iliyosalia ndani ya CHADEMA ambayo imekuwa ikiibeba CHADEMA kama chama tangu kabla wakati na baada ya kupigwa kwake risasi 16 akiwa katika shughuli za kibunge Jijini Dodoma.

Kama Tundu AM Lissu ataihama CHADEMA basi huenda CHADEMA ikasalia kuwa kama CUF, NCCR na hata TLP kwa tayari imeshapoteza agenda yake ya Msingi ambayo ni kupinga Uzembe, Wizi na Ufisadi.

Tetesi za Mbowe kulamba asali ili aendelee kuwako CHADEMA kama Mwenyekiti ili kumdhibiti Tundu AM Lissu zimemlemea Mbowe na kuamua kurejesha Majeshi yake matiifu kutoka katika orodha ya Wabunge 19 waliofukuzwa.

Mbunge mmoja toka miongoni mwao jina tunalihifadhi anasema namnukuu "Halima ametuambia tusiendee CCM ila tumpambanie Mbowe awe mwenyekiti na Heche makamu ili amtoe Mnyika na Lissu ili turudi CHADEMA" mwisho wa kunukuu.

Taarifa kutoka maeneo mbalimbali zinaunga mkono Lissu kuanzisha chama chake hicho kipya kwani CHADEMA tayari imechafuka na imekuwa ngumu kuitofautisha na Chama tawala cha CCM kimaadili na kimwenendo na hivyo kupoteza tafsiri ya neno "Upinzani"

Tundu AM Lissu anasifika kwa kukemea rushwa na ufisadi ndani na nje ya CHADEMA waziwazi na ndio turufu pekee inayomfanya azidi kuaminika na kipendwa zaidi na Watanzania hasa wa tabaka la chini.

Kitendo hicho kinampa wakati mgumu zaidi Mwenyekiti wa Sasa Freeman Mbowe ambae Uadilifu wake na nyendo zake hasa awamu hii ya sita zinamashaka mengi kutokana na tuhuma nyingi za ulambaji wa asali kwa maeneo na nyakati tofauti tofauti.

Mbowe anaamini mfumo sasa uko tayari kupeleka dola CHADEMA wakati Lissu anaamini mfumo ndio CCM na CCM ndio mfumo wenyewe.

Lissu anaamini katika kutwaa dola kupitia Wananchi wakati Mbowe anaamini katika kutwaa dola kupitia mfumo au dola yenyewe.

Kitendo cha Lemma kujitoa katika kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Kanda ya Kask ni ishara inayoakisi ninachokiandika hapa kwani ni dhahiri ananga'tuka CHADEMA na kuelekea kwenye hicho chama jipya,

Tanzania inahitaji upinzani safi sio bora upinzani, ndio maana waliwakataa CUF, wakawakataa NCCR na hivyo hivyo wakafanya kwa TLP na leo hii ni zamu ya CHADEMA kukataliwa wazi wazi

CHADEMA ndio chama Cha upinzani kinachomiliki mwenyekiti mmoja kwa miaka 30 huku wakiranda randa kuomba katiba mpya kwa wananchi wakati katiba yao inamatundu kama chekecheo.
Nimejuta kusoma huu upuuzi, anyway kosa ni langu
 
Mhe. Mbowe tunakuomba umpishe Lissu. Miaka 30 imekutosha vinginevyo utabaki mwenyewe na CHADEMA yako na Covid-19.
Propaganda za kijinga sana, ingekuwa huko Facebook kidogo watu wangeamini. Sasa jf wanaingia watu wanaojielewa so huwezi kufanikiwa kwa hili
 
Ningekuwa mwanachama wa CHADEMA, hapa mwenyekiti ningemtuhumu kufanya conspiracy ya kukisambaratisha chama ksirisiri
Mkuu utakuwa una tatizo la kiakili, so wewe akili yako imeamini kuwa mleta kaleta habari ya kweli wakati yeye mwenyewe anasema ni hisia! Kweli Tz bado sana kama raia wake ni kama wewe
 
Wapinzani wakuu wa CHADEMA wanapenda sana vyama vyenye viongozi maskini wa fedha na mawazo ili wapate mtelemko ndiyo maana ya kelele za kuhusu uwenyekiti wa Mbowe.
Ingetakiwa hizi propaganda wakafanyie Facebook, huku watu wanajitambua sidhani kama kuna kiumbe anaweza kuamini haya zaidi ya wao kwa wao hao Fisiemu
 
Mimi nilitoka chadema 2015 wakati chama kilipokodishwa kwa lowassa, ninaweza kutangaza nia ya kujiunga na chama kingine makini. Lakini kwa hiki, "chama cha lisu" itanizuia kabisa kujiunga nacho. Nyakati za kujiunga na chama cha mtu zimeshapita, hasa kama mtu mwenyewe ni lisu.
 
Yule mzee ni kilaza sana na true colors zake zimeshaonekana. Watanzania wanasali sana kuliombea taifa lao, kwenye wimbo wa taifa wanamtaja MUNGU na kuomba baraka zake. Ni ngumu sana sehemu penye ulinzi wa MUNGU mtu kama mbowe ambaye hana karama na Hekima ya uongozi kuweza kufanikiwa.

Jamaa ana tamaa sana. Hela anazo, kwanini analazimisha kuendelea kuwapo katika wadhifa ambao haumtaki for 30 years. Mzee takataka.
Mbona mnaoumia sana ni CCM kuliko wenyechama chao? Chama hakikuhusu lakini unapiga kelele badala ya kwenda kichapisha form moja huko kwenu
 
Kama wayajua hayo basi kaa kwa kutulia waachie wenye chama chao
 
Mimi sioni kama Chadema itameguka kuelekea uchaguzi mkuu 2025.
Kwani ikimeguka kwa namna yoyote utakuwa ushindi mkubwa kwa CCM.
Chadema wasiongezee matatizo they need to read between the lines,Ukiweka changamoto za Covid 19 + Msigwa na Kanda ya Nyasa +Katibu Mkuu Myika+ Mwenyekiti Mbowe + Makamu Lissu =???
Chadema imefika wakati mjitambuwe mapema vinginevyo........
Acha kujivua akili na kuamini huu ujinga, kuwa kama uko Jf na siyo Facebook
 
2020 kulikuwa hakuna uchaguzi wenye tija.
Wapiga kura wengi walliukubali utawala wa Magufuli.
Kosa ni kubwa ccm walitaka kufuta upinzani jumla.
Ila ulikuwa uchaguzi ambao hata wasingeiba kura wangeshinda tu.
Kuna mtu timamu kweli angeweza mchagua jiwe? Labda wale waliokuwa wanajiita wanyonge wakidhani unyonge wao umeletwa na watu wenye mafanikio
 
Hakun wa kuamini huu ujinga ila ni mafisiemu yanafarijiana
Walidanganywa kuwa CHADEMA imekufa, walifanya hujuma ife haikufa. Sasa wana weweseka kuchanganya watu, inavyoonekana Mbowe kawachanganya sana.
 
Ningekuwa mwanachama wa CHADEMA, hapa mwenyekiti ningemtuhumu kufanya conspiracy ya kukisambaratisha chama ksirisiri
Kama ungekuwa mwanachama wa CDM basi ingekuwa ni hasara sana kwa hicho chama, yaani unaamini huu ujinga wa mleta mada [emoji848]
 
Mbona mnaoumia sana ni CCM kuliko wenyechama chao? Chama hakikuhusu lakini unapiga kelele badala ya kwenda kichapisha form moja huko kwenu
Acha upuuzi
Kuipinga chadema haimaanishi unaikubali Ccm.
Chadema ya Mbowe sio chama cha upinzani kwa sasa ila ni Ccm iliyopoa kidogo. Wanapambana kuibakiza Ccm ya Samia madarakani.

Tumechoka unafiki wa hao watu.
 
Wasalaam, JF.

Wakati Tundu AM Lissu akiamua kuasisi chama kipya cha siasa na kuifanya Tanzania kuwa na jumla ya vyama 20 vya siasa akianzia kukisimika chama hicho kipya mkoani kwake Singida kabla ya kuanza harakati Tanzania nzima.

Tayari baadhi ya watu waadilifu kama Dkt. Slaa, Prof Safari, Boniface Mwambukusi, John Heche, John Pambalu, Godbless Lema, wanatajwa kuwa Viongozi wa awali wa Chama hicho ambacho bado jina lake halijajulikana.

Mkakati huu unakuja baada ya Katibu Mkuu wa CHADEMA John John Mnyika kukataa kuendelea kukaa ofisi kwa madai kwamba kazi zote za Katibu Mkuu anafanya Mpwa wa Mbowe ndugu John Mrema akisaidiwa na Bw Reginard Mtumishi ambae ni mjomba wa Freeman Mbowe.

Mkakati uliopo leo CHADEMA ni Freeman Mbowe kugombea tena nafasi ya Uenyekiti wa chama kwa mara ya nne mfululizo ukiacha mara mbili alizokuwa mwenyekiti kupitia BAVICHA na kufanya jumla ya mihula yote hiyo inamfanya Freeman Mbowe kuwa na miaka 30 kwenye uongozi wa CHADEMA bila kupisha yoyote kwenye uongozi Chama hicho.

Tundu AM Lissu ndio nembo pekee iliyosalia ndani ya CHADEMA ambayo imekuwa ikiibeba CHADEMA kama chama tangu kabla wakati na baada ya kupigwa kwake risasi 16 akiwa katika shughuli za kibunge Jijini Dodoma.

Kama Tundu AM Lissu ataihama CHADEMA basi huenda CHADEMA ikasalia kuwa kama CUF, NCCR na hata TLP kwa tayari imeshapoteza agenda yake ya Msingi ambayo ni kupinga Uzembe, Wizi na Ufisadi.

Tetesi za Mbowe kulamba asali ili aendelee kuwako CHADEMA kama Mwenyekiti ili kumdhibiti Tundu AM Lissu zimemlemea Mbowe na kuamua kurejesha Majeshi yake matiifu kutoka katika orodha ya Wabunge 19 waliofukuzwa.

Mbunge mmoja toka miongoni mwao jina tunalihifadhi anasema namnukuu "Halima ametuambia tusiendee CCM ila tumpambanie Mbowe awe mwenyekiti na Heche makamu ili amtoe Mnyika na Lissu ili turudi CHADEMA" mwisho wa kunukuu.

Taarifa kutoka maeneo mbalimbali zinaunga mkono Lissu kuanzisha chama chake hicho kipya kwani CHADEMA tayari imechafuka na imekuwa ngumu kuitofautisha na Chama tawala cha CCM kimaadili na kimwenendo na hivyo kupoteza tafsiri ya neno "Upinzani"

Tundu AM Lissu anasifika kwa kukemea rushwa na ufisadi ndani na nje ya CHADEMA waziwazi na ndio turufu pekee inayomfanya azidi kuaminika na kipendwa zaidi na Watanzania hasa wa tabaka la chini.

Kitendo hicho kinampa wakati mgumu zaidi Mwenyekiti wa Sasa Freeman Mbowe ambae Uadilifu wake na nyendo zake hasa awamu hii ya sita zinamashaka mengi kutokana na tuhuma nyingi za ulambaji wa asali kwa maeneo na nyakati tofauti tofauti.

Mbowe anaamini mfumo sasa uko tayari kupeleka dola CHADEMA wakati Lissu anaamini mfumo ndio CCM na CCM ndio mfumo wenyewe.

Lissu anaamini katika kutwaa dola kupitia Wananchi wakati Mbowe anaamini katika kutwaa dola kupitia mfumo au dola yenyewe.

Kitendo cha Lemma kujitoa katika kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Kanda ya Kask ni ishara inayoakisi ninachokiandika hapa kwani ni dhahiri ananga'tuka CHADEMA na kuelekea kwenye hicho chama jipya,

Tanzania inahitaji upinzani safi sio bora upinzani, ndio maana waliwakataa CUF, wakawakataa NCCR na hivyo hivyo wakafanya kwa TLP na leo hii ni zamu ya CHADEMA kukataliwa wazi wazi

CHADEMA ndio chama Cha upinzani kinachomiliki mwenyekiti mmoja kwa miaka 30 huku wakiranda randa kuomba katiba mpya kwa wananchi wakati katiba yao inamatundu kama chekecheo.
No comment
 
Back
Top Bottom