Huenda Edwin Mtei na Bob Makani ndiyo wanasiasa bora wa wakati wote Tanzania

Ni muhimu pia kuzingatia evolution ya CCM kutoka kuwa chama cha siasa mpaka sehemu kamili au extension ya dola.
It's not that way!, hakuna evolution but it's the formation of CCM, tangu CCM inazaliwa ile Februari 5 mwaka 1977, ilizaliwa kwenye mfumo wa chama kimoja, na wakati huo Tanzania tulikuwa na mfumo wa chama kushika hatamu za kuiongoza serikali, party supremacy, hivyo hii katiba yetu ya mwaka 1977 ni katiba ya CCM ndio imegeuzwa katiba ya nchi, ni katiba ya mfumo wa chama kimoja, ambapo CCM sio tuu ni chama cha siasa, CCM ni chama dola, ni dola! "CCM sio tu ni chama cha siasa, CCM ni chama tawala kinachotawala Dola, CCM ni chama Dola, CCM ni Dola!"

Tulipoanza mfumo wa vyama vingi ile 1992, tulipaswa tubadili kwanza katiba kutoka katiba ya mfumo wa chama kimoja tuje katiba ya mfumo wa vyama vingi, CCM irudishe serikalini zile rasilimali za taifa ilizohodhi enzi za mfumo wa chama kimoja, ndipo kishindane na vyama vingine, hili halikufanyika!, JPM alipoingia alitaka kufanya kitu na tukampongeza Kwa Uamuzi Huu, Pongezi Sana Rais Wetu Magufuli, Utabarikiwa na Mungu, na Taifa Pia Litabarikiwa!

Hivyo bila katiba mpya, hakuna siku upinzani utakuja kuingia Ikulu ya Tanzania!Wenye Matumaini na Upinzani Kushika Dola! Sahauni! CCM Inajiandaa Kuua Kabisa na Kuuzika Jumla

Na ndio maana CCM kutumia Hooks & Crooks Kushinda Chaguzi, Inajua Ikishindwa Ndio Itakufa Jumla, Itakubali?

Na itatawala milele! Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.
P.
 
CCM kama wakoloni walivoondoka ni hivyo CCM itaondoka tena siyo mbali saana.
 
CCM kama wakoloni walivoondoka ni hivyo CCM itaondoka tena siyo mbali saana.
Siasa ni Sayansi, political science, inafuata kanuni za kisayansi, scientific principles , ili CCM iondoke lazima itumie formula ya Newton's law of motion, lazima itokee force kubwa zaidi ya CCM to move it, force hiyo kwa Tanzania bado haipo!, kinatakiwa kwanza kitokee chama chenye nguvu zaidi ya CCM cha kuungwa na watu wengi zaidi ya zile asilimia 98% ndipo kiiondoshe CCM!.

Kwa sasa chama hicho bado hakipo!, hivyo CCM bado ipo sana!.
P
 


Prof. Kighoma Ali Malima (Profesa wa kwanza wa Uchumi wa Kitanzania katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - UDSM) alipokuwa Waziri wa Elimu (1987–1989), alibadili mfumo wa udahili wa wanafunzi wa sekondari na vyuo vikuu kwa kuanzisha mfumo wa kuweka namba badala ya majina ya wanafunzi kwenye mitihani ya taifa (anonymous examination numbering system).

Hatua hii ilipunguza uwezekano wa upendeleo wa kimfumo (systemic bias). Hata hivyo, ilimjengea maadui wengi ndani ya mtandao wa utawala, wakimtuhumu kwa kile walichokiita "kuhudumia agenda za kiislamu".

I stand to be corrected
 
Siyo kweli. Chama cha siasa ni taasisi kama taasisi nyingine. Taasisi yeyote inaweza kuanguka yenyewe kwa makosa yake yenyewe bila external force. Nothing lasts forever.
 
Usiogope, mtandoka tu muda ukifikia.
 
Siyo kweli. Chama cha siasa ni taasisi kama taasisi nyingine. Taasisi yeyote inaweza kuanguka yenyewe kwa makosa yake yenyewe bila external force. Nothing lasts forever.
Sayansi inafuata kanuni, ili CCM ianguke na tubaki salama, ni lazima kwanza kuwe na replacement ili CCM ikianguka hiyo nafasi yake ishikwe na mwingine!, Tatizo kwa Tanzania, bado hakuna mbadala wa CCM, as a results CCM inaendelea kuwepo mpaka apatikane mbadala ndipo ipishwe, ikianguka bila mbadala, nchi itaparaganyika!.

Mfano ile 2015, ndio uchaguzi wa kwanza wa vyama vingingi ambapo Tanzania we had a choice GE2015 - Octoba 2015:Tanzania Has a Choice Kati ya Kuendelea na Umasikini, au Kuchagua Utajiri!. Jee... ?!

Tatizo lilikuwa Chadema GE2015 - CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!

Mwaka 2020 nikauliza In 2015 Election, Tanzania had A Choice To Choose From. Jee Kwa 2020, Do We Still Have A Choice?

P
 
 
Usiogope, mtandoka tu muda ukifikia.
Ni kweli, kila lenye mwanzo lina mwisho, ila kwa waliozaliwa wakaikuta Tanzania imetawaliwa na chama kile kile kimoja tangu ipate uhuru wake na wakafa wakakiacha, kwao ni chama hicho kimetawala milele yao!, hivyo CCM bado ipo sana!, na kwa vile mimi umri wangu saa hizi nitayari jioni, then niko very right kusema CCM itatawala milele!
Rejea

Mzee Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…