MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,775
- 71,893
Yaliyopita, yaliyopo na yajajo kuhusu Tanzania.
Edwin Mtei na Bob Makani wanahukumiwa vizuri na historia kuliko mwanasiasa mwingine yoyote wa kizazi cha kwanza. Ntakueleza ni kwanini nasema hivi:
Kipimo kikubwa cha uongozi ni KUTOKUWEPO (Absence of a leader). Mara zote kiongozi anaweza kuonekana mzuri kwasababu yupo na anafuatilia vizuri na ukaribu mambo yake. Lakini ukweli mchungu ni kwamba kiongozi huanza kupimwa uwezo wake wakati HAYUPO. Hili linaanzia kwenye ngazi ya kifamilia, ambapo tunaangalia mafanikio ya mzazi kwa kuangalia jinsi watoto wanafanya wakiwa peke yao au mbali na nyumbani. Mara zote wazazi wakifariki ndiyo utafahamu malezi yao yalikuwaje.
Hili linaweze lisiwe ni mstari wa moja kwa moja (Not Linear). Lakini kwenye siasa mara nyingi viongozi bora hupimwa kwa madhara na faida walizoziacha muda mrefu hata baada ya wao kuondoka. Falsafa zao, Sera zao, Sheria walizotunga, Taasisi walizozitengeneza, lakini kubwa ni kuandaa kizazi kinachofuata kuweza kuduma katika misingi ile-ile na kuweza kufanya zaidi ya kizazi kilichopo.
Waisisi wa CHADEMA HAWAPO duniani. Hebu tuangalie ambacho kimeendelea kwenye taasisi yao ilhali hawapo:
=========================================================
Miaka kuanzia ya 1970-2000 mtu wa kizazi kile akimuuliza kuhusu Mzee Edwin Mtei angekwambia kwamba hakuwa kiongozi mzuri kwasababu kadhaa-wa-kadhaa. Hata alipoanzisha CHADEMA mwaka 1992, watu wengi hasahasa CCM akiwemo Mzee Nyerere ungewaambia kwamba chamba ambacho kinaanzishwa na Mchagga wa Marangu na Msukuma wa Shinyanga kuna siku kitakuwa ndicho chama kinachotegemewa na kuaminika na zaidi ya asilimia 50% ya watanzania, nadhani asingekuamini mtu.
KINA MZEE MTEI: Mwaka 1995-2000 hawakusimamisha mgombea wa Uraisi kama ambavyo vyama vingine vya upinzani vinafanya kwenye nyakati za awali. Wao walikuwa wanapambana na Ubunge na Udiwani. Mwaka 1995 uchaguzi mkuu, CHADEMA ilipata viti vitano (5) tu na madiwani arobaini na moja (41) tu, ambapo idadi iliendela kupanda kadiri miaka inavyoendelea mbele.
Binafsi, naamini kuwa ni makosa makubwa sana kwa chama kichanga ambacho kinataka kuchukua nchi kuanza moja kwa moja kwa kusimamisha MGOMBEA NAFASI YA URAISI bila kuwekeza nguvu kwenye nafasi za chini kabisa ili kujihakikishia majimbo ya muhimu.
Tatizo huwa ni kwamba, nafasi ya URAISI ni nyeti mno. Unapoanza kutangaza kwamba unaitaka unafanya taasisi zote nyeti za nchi kuanza kuwafuatilia kwa ukaribu. URAISI nchini Tanzania ni nafasi kubwa mno mnoo. Tena UPINZANI huwa wanakosea sana pale ambapo wanawachukua watu kutoka CCM ambao wamekosana na watawala na kuwasimamisha kwenye nafasi ya Uraisi.
CUF ilipokuwa inaanzishwa, ilitokana na baadhi ya wana-CCM wenye imani ya kiislamu kutoridhishwa na mwelekeo mzima wa jinsi CCM inawapuuza waislamu, na kuonekana kuikandamiza Zanzibar. Kina Prof Kighoma Malima walichukiwa sana na watawala wa CCM, hivyo kwenda nje na siasa zao kuanza kuungwa mkono na CUF kulipekea chama hicho kuanza kufuatiliwa bila sababu.
MFANO HAI NI HUU: Wakati wakoloni wanatawala Afrika hasa-hasa wala wa Uingereza, ilikuwa siyo jambo rahisi kwa wapigania uhuru kupewa UKUU WA NCHI moja kwa moja. Walikuwa wanaanza na nafasi za chini kama WAZIRI MKUU chini ya Gavana na Malkia kwa miaka kadhaa ndiyo baadaye wakishapata viti vingi bungeni inakuwa rahisi kudai uhuru.
Marehemu Dr.Kwame Nkrumah, alianza kama WAZIRI MKUU mwaka 1952, chini ya Gavana hadi mwaka 1957, nchi ilipopata Uhuru. Angeanza moja kwa moja kutaka UKUU WA NCHI ingekula kwake, na wazungu wangemtandika vibaya sana kama walivyotandikwa Mau-Mau kwenye vita yao dhidi ya kudai uhuru.
Hata Tanganyika, Mzee Nyerere alianza kwanza kama Waziri Mkuu mwaka 1959, kisha baadaye kuwa Raisi baada ya kuwa ndani ya serikali. Kiufupi Gavana Edward Twinning alikuwa anahujumu TANU, na kwenye uchaguzi wa wabunge mwaka 1958 TANU walikuwa wanataka kugomea uchaguzi baada ya Gavana Twinning kugawa majimbo kumi na kutaka kila jimbo litoe wagombea watatu (Moja Mweusi, Moja Mzungu, Moja Muashia).
Wazee wa TANU waligoma, lakini Mzee Nyerere akawashawishi kwamba aheri waanza na nafasi za ubunge kuliko kuzikosa kabisa maana, nafasi hizi zitawasaidia baadaye kwenye kufanya siasa za UWAZIRI MKUU hadi nafasi nyingine kubwa ya nchi. Mwaka 1960 kwenye UCHAGUZI MKUU, TANU ilipata viti 70 kati ya 71, hivyo kupeleka TANU kuteua WAZIRI MKUU, ambaye akawa Mzee Nyerere.
Lakini yote haya yalitokana na uvumilivu kwenye uchaguzi wa wabunge wa mwaka 1958 ambao ulisaidia watanganyika kuingia bungeni na kupata majimbo muhimu na uzoefu wa kisiasa.
Kina Mzee Mtei na Makani, kutokuwa na haraka ndiko kumezaa CHADEMA hii ya leo hii ambayo imefika leo. Mkakati ambao waliupanga miaka ya 90's limekuja kuzaa matunda makubwa leo hii 2026. CHADEMA imejengewa uzoefu mkubwa wa kisiasa wa kuweza kufanya SIASA bila kutegemea vyeo vya kisiasa ndani ya serikali.
Hili siyo jambo rahisi. Leo hii sidhani kama CCM au ACT- Wazalendo wanaweza kufanya siasa kwa nguvu bila kuwa baadhi ya nafasi ndani ya serikali. Sidhani kama wanasiasa wao watakuwa tayari kufanya siasa bila kupewa mishahara ya Ubunge, Posho za Udiwani na Ruzuku Kubwa.
HIVYO BASI: TUNU ya kwanza kabisa ambayo inamfanya Mzee Mtei na Mzee Makani wawe wanasiasa bora wa wakati wote hapa Tanzania, ni kufanikiwa kwa kiwango kikubwa kuijengea taasisi ya CHADEMA falsafa ya kuweza kufanya siasa bila kuwa na nafasi nyingi na kubwa za kisiasa. Hili TANU waliliweza kwa miaka zaidi ya mitano (5), na ndiyo ilikuwa nguvu yao, sidhani kama CCM leo hii wanaweza kufanya siasa za kujitolea bila dola.
Aina hii ya siasa inaweza kufanywa na watu kutoka nchi za Ughaibuni huko. Hapa Afrika mara nyingi vyama vyenye dola vikipoteza nafasi ndiyo huwa unakuwa mwisho wake, kwasababu havina TUNU ya kuweza kufanya siasa bila fedha au vyeo.Yaliyopita, yaliyopo na yajajo kuhusu Tanzania.