Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Tatizo la wewe Pasco ni moja, kuleta hoja bila kuzifanyia tafiti. Mimi nashangaa wanaosumbuka na Freeman Mbowe, baada ya kuangaika na Dr Slaa akaonekana kuwa ni kisiki sasa naona mnaamia kwa Mbowe. Kwa kumbukumbu zangu, Freeman Mbowe alikwisha tamka mara kadhaa kuwa hatagombea tena nafasi hiyo. Pili, hivi ni kweli kwa akili za kawaida kabisa, Mbowe anaweza akachomoa hicho kipengele na wajumbe wote wa mkutano mkuu wakamuangalia na kumchekea? Kwanini tusiwe wa kweli kuwa, kama hicho kipengele akipo basi wakulaumiwa ni wajumbe walipitisha hiyo katiba na sio Mbowe.

Zaidi sana, mimi nazichukulia tuhuma hizi ni upepo ulioanza tangu katikati ya mwezi huu, kuanzia kwenye ruzuku, pesa za uswisi na sasa hili la katiba. Hii ni mipango mkakati wa watu wasioitakia mema CHADEMA kujifanya wanaipenda sana CHADEMA kiasi cha kuwa wasemaji wa chama hiki.

CHADEMA ni mpango wa MUNGU, akuna wa kuwa kinyume chake.
 
Nafasi ya Uenyekiti wa Chama mbona inawatoa watu jasho namna hii?Huku ni kuzunguka tu.....Hebu nendeni straight kwenye point.

Nadhani ikithibitika hivyo basi ofisi ya msajili nayo itabidi kuwajibika.Ni kwanini isemwe kipindi hiki na si wakati wowote?

Hahahahahaa wanatafuta ajenda ya uchaguzi, wapiga kura tunawaangalia uchaguzi utafika tutawapa wanachostahili, wanataka kutucheleweshea ukombozi tu vibaraka wa CCM hawa..
 
Tatizo la wewe Pasco ni moja, kuleta hoja bila kuzifanyia tafiti. Mimi nashangaa wanaosumbuka na Freeman Mbowe, baada ya kuangaika na Dr Slaa akaonekana kuwa ni kisiki sasa naona mnaamia kwa Mbowe. Kwa kumbukumbu zangu, Freeman Mbowe alikwisha tamka mara kadhaa kuwa hatagombea tena nafasi hiyo. Pili, hivi ni kweli kwa akili za kawaida kabisa, Mbowe anaweza akachomoa hicho kipengele na wajumbe wote wa mkutano mkuu wakamuangalia na kumchekea? Kwanini tusiwe wa kweli kuwa, kama hicho kipengele akipo basi wakulaumiwa ni wajumbe walipitisha hiyo katiba na sio Mbowe.

Zaidi sana, mimi nazichukulia tuhuma hizi ni upepo ulioanza tangu katikati ya mwezi huu, kuanzia kwenye ruzuku, pesa za uswisi na sasa hili la katiba. Hii ni mipango mkakati wa watu wasioitakia mema CHADEMA kujifanya wanaipenda sana CHADEMA kiasi cha kuwa wasemaji wa chama hiki.

CHADEMA ni mpango wa MUNGU, akuna wa kuwa kinyume chake.

Niko na wewe 100%+ only83
 
Last edited by a moderator:
WanaJF,

Pamoja na kuwa sitaki kuingilia mjadala katika hatua hii, naomba kuthibitisha kuwa:
I) Katibu Mkuu wa Chadema, kwa mujibu wa Katiba na Kanuni ya Chadema, ndiyo mhimili mkuu na mwenye jukumu la kutunza na kuhakikisha Katiba ya Chama inatunzwa.

2) Nataka kuwahakikishia wanachadema wote, kuwa nilikuwepo nimekuwa ndani ya Chadema kuanzia 1998 ambapo nilikuwa Makamu Mwenyekiti Bara, na baadaye 2003 Kaimu Katibu Mkuu, na hatimaye Katibu Mkuu. Hivyo nimeshiriki kikamilifu kuandaa Katiba ya 2004 na pia Katiba ya 2006 baada ya Rebranding ya Chama. Nataka niwahakikishie wanachadema, hakuna toleo lolote la Katiba ndani ya Chadema imeweka " muda wa Uongozi kuwa vipindi viwili tu", kuanzia Katiba aliyoiasisi Mzee Mtei na kupitishwa na Mkutano Mkuu, wala si ya 2004 au ya 2006. Kama kuna mtu anasema ilikuwepo na imeondolewa kinyemela, basi aonyeshe kifungu hicho kwenye Katiba yeyote ile, au miniti za kikao chochote kile.

3. Mimi Dr Slaa, ndiye niliyewasilisha Miniti za Mkutano Mkuu wa 2006 kwa Msajili ikiambatana na Katiba iliyopitishwa na Mkutano Mkuu. Tulichobishana Mimi na Msajili, na kwa maandishi, ni kuwa Msajili alit aka nimwasilishie nakala ya Katiba kwa Kiingereza. Nilimkatalia kwa msingi kuwa Katiba yetu ilipitishwa na Mkutano Mkuu kwa kiswahili na Mkutano Mkuu na hivyo siwezi Mimi kumpelekea kwa Kiingereza. Msajili alidai kuwa ni hitaji la kisheria. Nilimjibu kuwa sheria hiyo inapaswa kufanyiwa marekebisho. Hata hivyo, baadaye tulikubaliana kuwa nitengeneze " literal translation" lakini kwa mahitaji ya kisheria itatumika Katiba ya Kiswahili ambayo ndiyo iliyopitishwa na Mkutano Mkuu. Hivyo, ninathibitisha kuwa hakuna kipengele chochote kilichoingizwa kinyemela.

Wanachadema, wapenzi, na wananchi kwa ujumla, huo ndio ukweli. Kama mtu anadhani kuna utata aende kwa Msajili akague Katiba ya 1992, 2004 na 2006, nadhani utaratibu wa Msajili itaruhusu ukaguzi huo. Ndio njia pekee ya kuacha kabuni na kuwa watabiri kwa misingi ya waganga wa kienyeji. Tufanye kaki kisayansi, na tusiwatie hofu wananchi bila sababu.

Kama mtu Ana ajenda yake ya siri, huyo hatuwezi kumsaidia! Wananchi, tuna mambo ya muhimu zaidi kuliko hizi propaganda, tunahitaji kutumia muda wetu kwa mambo hayo, mathalan madai ya Katiba Mpya, kupigania maslahi ya Taifa na Watanzania hasa walala hoi ambao kila siku wanazidi kupigika, kupambana na manyanyaso Kama yaliyotokea Serengeti na Babati ambao wananchi wameteswa viajabu katika nchi inayojitangaza kuwa na utawala wa sheria nk.
 
hiyo katiba fake imethibitishwa na msajiri wa vyama? na akaona utekelezaje wake ni fake? basi ofisi ya msajili wa vyama inatakiwa ifungiwe milele!!Acheni propaganda za kijinga ,akili za B7 kama uharo
fake kwa maana kwamba iliyopelekwa kwa msajili sio ile iliyokubalika katika vikao halali vya chama, kulingana na maelezo ya mleta hoja..tatizo lenu mambo madogo sana kama haya ya kuyajibu kwa majibu yaliyonyooka bila matusi hamuwezi...matusi si majibu ni moja ya njia ya kuonesha kua huna jibu..
 
WanaJF,

Pamoja na kuwa sitaki kuingilia mjadala katika hatua hii, naomba kuthibitisha kuwa:
I) Katibu Mkuu wa Chadema, kwa mujibu wa Katiba na Kanuni ya Chadema, ndiyo mhimili mkuu na mwenye jukumu la kutunza na kuhakikisha Katiba ya Chama inatunzwa.

2) Nataka kuwahakikishia wanachadema wote, kuwa nilikuwepo nimekuwa ndani ya Chadema kuanzia 1998 ambapo nilikuwa Makamu Mwenyekiti Bara, na baadaye 2003 Kaimu Katibu Mkuu, na hatimaye Katibu Mkuu. Hivyo nimeshiriki kikamilifu kuandaa Katiba ya 2004 na pia Katiba ya 2006 baada ya Rebranding ya Chama. Nataka niwahakikishie wanachadema, hakuna toleo lolote la Katiba ndani ya Chadema imeweka " muda wa Uongozi kuwa vipindi viwili tu", kuanzia Katiba aliyoiasisi Mzee Mtei na kupitishwa na Mkutano Mkuu, wala si ya 2004 au ya 2006. Kama kuna mtu anasema ilikuwepo na imeondolewa kinyemela, basi aonyeshe kifungu hicho kwenye Katiba yeyote ile, au miniti za kikao chochote kile.

3. Mimi Dr Slaa, ndiye niliyewasilisha Miniti za Mkutano Mkuu wa 2006 kwa Msajili ikiambatana na Katiba iliyopitishwa na Mkutano Mkuu. Tulichobishana Mimi na Msajili, na kwa maandishi, ni kuwa Msajili alit aka nimwasilishie nakala ya Katiba kwa Kiingereza. Nilimkatalia kwa msingi kuwa Katiba yetu ilipitishwa na Mkutano Mkuu kwa kiswahili na Mkutano Mkuu na hivyo siwezi Mimi kumpelekea kwa Kiingereza. Msajili alidai kuwa ni hitaji la kisheria. Nilimjibu kuwa sheria hiyo inapaswa kufanyiwa marekebisho. Hata hivyo, baadaye tulikubaliana kuwa nitengeneze " literal translation" lakini kwa mahitaji ya kisheria itatumika Katiba ya Kiswahili ambayo ndiyo iliyopitishwa na Mkutano Mkuu. Hivyo, ninathibitisha kuwa hakuna kipengele chochote kilichoingizwa kinyemela.

Wanachadema, wapenzi, na wananchi kwa ujumla, huo ndio ukweli. Kama mtu anadhani kuna utata aende kwa Msajili akague Katiba ya 1992, 2004 na 2006, nadhani utaratibu wa Msajili itaruhusu ukaguzi huo. Ndio njia pekee ya kuacha kabuni na kuwa watabiri kwa misingi ya waganga wa kienyeji. Tufanye kaki kisayansi, na tusiwatie hofu wananchi bila sababu.

Kama mtu Ana ajenda yake ya siri, huyo hatuwezi kumsaidia! Wananchi, tuna mambo ya muhimu zaidi kuliko hizi propaganda, tunahitaji kutumia muda wetu kwa mambo hayo, mathalan madai ya Katiba Mpya, kupigania maslahi ya Taifa na Watanzania hasa walala hoi ambao kila siku wanazidi kupigika, kupambana na manyanyaso Kama yaliyotokea Serengeti na Babati ambao wananchi wameteswa viajabu katika nchi inayojitangaza kuwa na utawala wa sheria nk.
Mkuu Dr. W. Slaa, kwanza, heshima yako!, maana ile kujibiwa tuu na mtu wa calibre yako pekee, ni heshima kwangu na kwa thread hii, hivyo majibu yako, nayaunganisha pale mbele ya thread as an authority.

Uwongo ukisemwa sana na kuachwa bila kukanushwa, hugeuka ukweli. Sambamba na tuhuma hii, mtoa tuhuma pia ameweka tuhuma nyingine nyingi, zenye kuhitaji majibu ya kina kama haya uliyonijibu hapa.

Kwa vile CCM ndicho chama tawala, Chadema kiko kwenye mizani ya tukiaminie mwaka 2015 au bora kuendelea na CCM tuliyoizoea!, hivyo haya makando kando yoyote kuihusu Chadema, lazima yajibiwe ipasavyo kama hivi ulivyofanya hapa.

Asante sana kwa hili.

Kwa vile maelezo haya yako ni ya upande mmoja, nasubiri verification ya data toka kwa msajili, then niufunge rasmi huu mjadala.

Nashukuru tena.

Pasco.
 
2) Nataka kuwahakikishia wanachadema wote, kuwa nilikuwepo nimekuwa ndani ya Chadema kuanzia 1998 ambapo nilikuwa Makamu Mwenyekiti Bara, na baadaye 2003 Kaimu Katibu Mkuu, na hatimaye Katibu Mkuu. Hivyo nimeshiriki kikamilifu kuandaa Katiba ya 2004 na pia Katiba ya 2006 baada ya Rebranding ya Chama. Nataka niwahakikishie wanachadema, hakuna toleo lolote la Katiba ndani ya Chadema imeweka " muda wa Uongozi kuwa vipindi viwili tu", kuanzia Katiba aliyoiasisi Mzee Mtei na kupitishwa na Mkutano Mkuu, wala si ya 2004 au ya 2006. Kama kuna mtu anasema ilikuwepo na imeondolewa kinyemela, basi aonyeshe kifungu hicho kwenye Katiba yeyote ile, au miniti za kikao chochote kile.

Kulingana na maelezo yako dr, katiba yenu haina ukomo wa kushika nafasi ya uongozi ndani ya chama...mwanachama anahaki ya kuwa kiongozi na kuwa mgombea halali katika chaguzi za chama baada ya vipindi viwili kupita..kama ikiwezekana anaweza ongoza milele.

Hamuoni kwamba kwa kufanya hivyo mnajenga utamaduni wa kifalme ndani ya chama na kuwanyima wanachama wengine wenye uwezo kugombea...

Kwa minajili hiyo si ajabu kwa mazoea ya kiutendaji, mkiweza kushika dola, mtashawishika kubadili Ibara ya 40(2) ya katiba ja Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, 1977...ili kuwapa nafasi ya kuwa wagombea halali wa urais zaidi ya vipindi viwili kama ilivyo katiba yenu ya chama??
 
Mtahangaika sana na chadema na kusahau kufanyia kazi ahadi maelfu kwa maelfu mlizotoa tangu 2005 hadi leo kama mmetimiza 5% ni bahati sana.mkija kustuka 2015 hii hapa na ndio kuyakuwa na kilio cha kusaga meno magamba ninyi.
 
Tatizo la wewe Pasco ni moja, kuleta hoja bila kuzifanyia tafiti. CHADEMA kiasi cha kuwa wasemaji wa chama hiki. CHADEMA ni mpango wa MUNGU, akuna wa kuwa kinyume chake.
Mkuu Only 83, utafiti hufanywa na watafiti, mimi sio mtafiti ni just a reporter kuripoti nilichoona, kuambiwa au kusoma. Tuhuma hizi nimezisoma humu jf, nimeuliza, wahusika mamejibu tena kwa ufasaha, bado Pasco ni tatizo?.
Pasco.
 
Pasco

Badilika mkuu usiwe na mawazo ya kudhani Chadema kitafutwa bila kuwa na sababu za msingi, maana sio mara ya kwanza kutuambia hivyo leo umekurupuka tena na mawazo yale yale angalia thread yako hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...dema-kufutwa-kwa-mujibu-wa-katiba-endapo.html

Nazidi kusema unaendeshwa kwa matukio ya kukurupuka, unakumbuka mara tu baada ya tukio la video ya Lwakatare ulituambia umeiona na ni "bonafide genuine" jaribu kuwa na ile aibu ya kawaida.
Mkuu Feedback, hizo sababu zikithibitishwa, ni sababu za msingi. Video ile nasema mpaka kesho ni "bonafide genuine!"
Na ikithibitika huo ulikuwa ni mpango wa Chadema kama chama, kinafutwa!.

Kwenye hili la aibu, kila mtu amegaiwa kiwango chake, bahati mbaya mimi mgao wangu ni mdogo, kiasi kwamba kwenye kuusema ukweli ninauamini, sina aibu hata chembe!.
Pasco.
 
WanaJF,

Pamoja na kuwa sitaki kuingilia mjadala katika hatua hii, naomba kuthibitisha kuwa:
I) Katibu Mkuu wa Chadema, kwa mujibu wa Katiba na Kanuni ya Chadema, ndiyo mhimili mkuu na mwenye jukumu la kutunza na kuhakikisha Katiba ya Chama inatunzwa.

2) Nataka kuwahakikishia wanachadema wote, kuwa nilikuwepo nimekuwa ndani ya Chadema kuanzia 1998 ambapo nilikuwa Makamu Mwenyekiti Bara, na baadaye 2003 Kaimu Katibu Mkuu, na hatimaye Katibu Mkuu. Hivyo nimeshiriki kikamilifu kuandaa Katiba ya 2004 na pia Katiba ya 2006 baada ya Rebranding ya Chama. Nataka niwahakikishie wanachadema, hakuna toleo lolote la Katiba ndani ya Chadema imeweka " muda wa Uongozi kuwa vipindi viwili tu", kuanzia Katiba aliyoiasisi Mzee Mtei na kupitishwa na Mkutano Mkuu, wala si ya 2004 au ya 2006. Kama kuna mtu anasema ilikuwepo na imeondolewa kinyemela, basi aonyeshe kifungu hicho kwenye Katiba yeyote ile, au miniti za kikao chochote kile.

3. Mimi Dr Slaa, ndiye niliyewasilisha Miniti za Mkutano Mkuu wa 2006 kwa Msajili ikiambatana na Katiba iliyopitishwa na Mkutano Mkuu. Tulichobishana Mimi na Msajili, na kwa maandishi, ni kuwa Msajili alit aka nimwasilishie nakala ya Katiba kwa Kiingereza. Nilimkatalia kwa msingi kuwa Katiba yetu ilipitishwa na Mkutano Mkuu kwa kiswahili na Mkutano Mkuu na hivyo siwezi Mimi kumpelekea kwa Kiingereza. Msajili alidai kuwa ni hitaji la kisheria. Nilimjibu kuwa sheria hiyo inapaswa kufanyiwa marekebisho. Hata hivyo, baadaye tulikubaliana kuwa nitengeneze " literal translation" lakini kwa mahitaji ya kisheria itatumika Katiba ya Kiswahili ambayo ndiyo iliyopitishwa na Mkutano Mkuu. Hivyo, ninathibitisha kuwa hakuna kipengele chochote kilichoingizwa kinyemela.

Wanachadema, wapenzi, na wananchi kwa ujumla, huo ndio ukweli. Kama mtu anadhani kuna utata aende kwa Msajili akague Katiba ya 1992, 2004 na 2006, nadhani utaratibu wa Msajili itaruhusu ukaguzi huo. Ndio njia pekee ya kuacha kabuni na kuwa watabiri kwa misingi ya waganga wa kienyeji. Tufanye kaki kisayansi, na tusiwatie hofu wananchi bila sababu.

Kama mtu Ana ajenda yake ya siri, huyo hatuwezi kumsaidia! Wananchi, tuna mambo ya muhimu zaidi kuliko hizi propaganda, tunahitaji kutumia muda wetu kwa mambo hayo, mathalan madai ya Katiba Mpya, kupigania maslahi ya Taifa na Watanzania hasa walala hoi ambao kila siku wanazidi kupigika, kupambana na manyanyaso Kama yaliyotokea Serengeti na Babati ambao wananchi wameteswa viajabu katika nchi inayojitangaza kuwa na utawala wa sheria nk.

Hii post atakuwa ameandika Slaa mwenyewe sio Josephine Mushumbusi.

Post za Slaa utazijua tu jinsi zinavyojenga hoja.
 
Heshima yako mkuu Pasco,

Kuna muda huwa nasononeka sana napoona mandishi kama haya kutoka kwa Mmenye. Mkuu nadhani ww huna chama ila ww ni mfuasi wa EL ,so nadhani Ethics za vyama huzijui unachojua ni ethics za kusukumwa na fikra za watu unaowapenda kama unavyompenda EL.

Kutokana na hilo naweza kabisa kuamini hata haya unayoyachokonoa CDM kuna mtu unamsujudu kule CDM ndiye unayeungana naye kuleta allegation ambazo hujazifanyia uchunguzi kama hizi. Sio siri mtu huyo unayemsujudi nitakuwa kichaa kama siye Le comrade Zitto, zipo thread umezisahau kwamba ulikuwa unachangia kumjenga Le Comrade ukiikandia CDM . Sasa iweje leo uikndie CDM kuwa ina katiba fake kwa wimbo kuwa wewe ni mpenda maendeleo na ustawi wa CDM!.

Mara zote unapoleta habari tata unawapumbaza watu na ID hii instead ya verified acc yako . Hizi umezileta kama tuhuma humu JF kwa mnufaa ya nani? kwanini usingemaliza uchunguzi wako then ukaja na habari kamili ? Kwa nguli wa habari kama wewe kuja kwa style hii inaniumiza sana coz naona kama tuna miaka mingine 100 ya mabadiliko.
 
Last edited by a moderator:
Kama mtu Ana ajenda yake ya siri, huyo hatuwezi kumsaidia! Wananchi, tuna mambo ya muhimu zaidi kuliko hizi propaganda, tunahitaji kutumia muda wetu kwa mambo hayo, mathalan madai ya Katiba Mpya, kupigania maslahi ya Taifa na Watanzania hasa walala hoi ambao kila siku wanazidi kupigika, kupambana na manyanyaso Kama yaliyotokea Serengeti na Babati ambao wananchi wameteswa viajabu katika nchi inayojitangaza kuwa na utawala wa sheria nk.

Mkuu agenda ya siri haikosekani. Nashukuru kutuelekeza "wenye akili" kwenye vipaumbele si vya CHADEMA tu bali vya Watanzania wote.
 
Kulingana na maelezo yako dr, katiba yenu haina ukomo wa kushika nafasi ya uongozi ndani ya chama...mwanachama anahaki ya kuwa kiongozi na kuwa mgombea halali katika chaguzi za chama baada ya vipindi viwili kupita..kama ikiwezekana anaweza ongoza milele.

Hamuoni kwamba kwa kufanya hivyo mnajenga utamaduni wa kifalme ndani ya chama na kuwanyima wanachama wengine wenye uwezo kugombea...

Kwa minajili hiyo si ajabu kwa mazoea ya kiutendaji, mkiweza kushika dola, mtashawishika kubadili Ibara ya 40(2) ya katiba ja Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, 1977...ili kuwapa nafasi ya kuwa wagombea halali wa urais zaidi ya vipindi viwili kama ilivyo katiba yenu ya chama??
Tangu chama kilipoasisiwa hapajawahi kuwa na kipengere kinachoweka ukomo kwenye uongozi, lakini hiyo haikumfanya mzee Mtei kung'ang'ania uenyekiti wala mrithi wake mzee Makani. Sijui hofu yako inatoka wapi. Mimi nilidhani kwenye hoja za Mwigamba tungezama kwenye ukiukwaji wa kanuni za fedha na ufisadi mwingine wanaodaiwa kuufanya viongozi.
 
Na mimi nihitimishe kwa kusema kazi uliyotumwa hapa JF imefeli kabla hujaianza.

Rudisha bahasha ya kaki kwa wenyewe waliokutuma. Hujafanikiwa.

Hakuna kitufe cha like kimesepa, LAKINI nimejikuta nachekelea mchango wako YOU HAVE MADE MY DAY
 
Pasco, nilijua lazima utajitokeza kwenye hili na hasa kutokana na mawasiliano yako na kiongozi aliyesimamishwa ili kupisha uchunguzi, huwezi kuchunguza mtu akiwa ameshikilia ofisi, sasa hapa una jaribu kuupindisha ukweli .

pili, ni kuwa Hiyo taarifa kuwa katiba ilibadilishwa ni uongo mtupu kwani hata katiba ya awali haikuwahi kuwa na kipengele cha ukomo wa uongozi, haya ni mambo ya kukariri , mwenye kupinga aweke ushahidi wake walau wa hicho kipengele cha katiba na kilikuwa kifungu gani na kilisomekaje , sio kuendeleza uongo na uzushi kama huu kwenye mitandao. wekeni hicho kifungu . Wenye katiba ya zamani, katiba ya Chadema ilibadilishwa mwaka 2006 , sasa leo ni mwaka 2013 why muda wote huo hapakuwa na haya?

Pasco, Mwigamba mwaka 2006 wakati katiba ya Chadema inabadilishwa hakuwa kwenye chama na hakuwa na nafasi yeyote ile, wakati huo alikuwa anafanya kazi UN ICTR , sasa leo naye unamtumia kama reference na kuhukumu bila kujipa muda wa kufanya hata utafiti kidogo tu? Hebu jaribu kuutafuta ukweli , hizi ni propaganda za kitoto kwani nyaraka zilizopitishwa na mkutano mkuu 2006 zipo na wajumbe wa mkutano mkuu waliobakia na nakala , wekeni hapa , ila sio kupiga makelele kama unavyofanya , ukweli uko mmoja tu na huwa haugawanyiki.

Kwa hiyo, mwenyekiti na katibu wake ni wa milele? Haiwezekani wengine kuachiwa nafasi hizo?
 
Back
Top Bottom