Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Itathibitika pasipo shaka, proven beyond reasonable doubt, kuwa viongozi wakuu wa CHADEMA, walijua, walishiriki, na walihusika kwa namna moja au nyingine, katika upangaji au utekelezaji wa vitendo vyovyote vya kuvuruga amani na utulivu wa taifa hili!, Chama hiki kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa, na kitafutwa rasmi, scraped from the book of political parties, mara moja na bila huruma yoyote!.

Kauli hii, imetolewa leo na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji John Tendwa, katika maongezi yangu ya ana kwa ana,(please note ni maongezi na sio mazungumzo!) yalifanyika leo jioni katika hoteli ya moja mjini Dodoma.

Kama kawaida yangu, nipatapo nafasi, na sababu ya kuwepo Dodoma, huwa nakwenda Dodoma, na ni kawaida yangu kufikia hoteli hii ambayo huwa nafikia ambayo ni kama RV ya kujichanganya kwa urahisi na waheshimiwa mbalimbali na kubadilishana nao mawazo.

Siku ya leo jioni, nilikutana na Msajili wa vyama, Jaji John Tendwa, nikamsalimu, na akanikaribisha alipokuwa amekaa peke yake, hivyo nikamjoin kwa maongezi tuu, na sio mazungumzo!.

Niliulizwa swali kuhusiana na ile "bonafide genuine!" endapo itakutikana "beyond reasonable doubt!" na "the court of competant jurisdiction" kuwa ile kitu ni kweli na ni "bonafide genuine!", na ikithibitika viongozi wakuu wa CHADEMA waliijua, waliipanga na walishiriki sio tuu kwenye "actus reus!", bali pia kwenye "mens rea!", basi Msajili Tendwa, atakifuta rasmi Chama cha CHADEMA, bila huruma yoyote, wala kujiuliza mara mbili mbili, bila kujali the consequenses au repacussions za uamuzi huo, kwa sababu hivyo ndivyo katiba ya nchi inavyosema!, na yeye ameapa kuilinda katiba hiyo!.

Nikadadisi zaidi, iwapo hayo kwa CHADEMA, yatathibitika kuwa kufanywa na CCM, jee nacho, atakifuta bila huruma?!. Msajili kwanza alisita kidogo na kusema kama ni CCM, kwa vile hiki ni chama tawala, kikithibitika kufanya makosa hayo, hakiwezi kufutwa right away kwa sababu huko kutakuwa ni kuvunja serikali iliyopo madarakani, bali atakipeleka Mahakama Kuu ili mahakama itoe utaratibu wa nini cha kufanya endapo chama tawala kitapoteza sifa ya kuwa chama cha siasa wakati kingali madarakani!. Hii inamaanisha as of now, hatuna sheria yoyote ya kuibadili serikali nje ya balot box!, hata kama serikali hiyo itakuwa ni dhalimu kiasi gani!, na chama tawala, kikishashika madaraka, hata kivunje sheria vipi, kitaendelea kuwepo madarakani no matter what!.

My take
Wakati tunasubiria katiba mpya kuziadress such issues, kuna umuhimu wa kuyafanyia mapitio mamlaka ya msajili wa vyama, isije kutokea vyama vikafanya makosa ya kusitahili kufutwa, msajili akatimiza wajibu wake, watu wakaishia kulalamika bure kuwa hawakutendewa haki!.

Kwa kumalizia, nilimuulizia kidogo kuhusu kuijua JF, akasema anaijua sana na anaisoma, ila anakerwa na watu ambao wao kazi yao ni kutukana tuu na kuchangia kwa lugha zisizo heshima na staha kwa viongozi wa taifa hili!.

Naomba kuchukua fursa hii kuwaomba wana JF wenzagu, tunawajibika kuendelea kuijenga jf na kuilinda heshima ya jf kwa kuchangia kistaarabu kwa lugha za heshima na staha.

Najua kuna wenzetu humu, kwa JF ni favorite past time na huja humu wakati hawana kitu kingine cha kufanya!.
Nawaomba mtuhurumie sisi ambao JF ni nyumbani kwetu, ni sebuleni kwetu na chumbani kwetu, tunashinda JF, tunalala JF, tunaamka JF, in short tunaiishi JF, kwetu JF is life we are living for!.

Wasalaam.
Pasco
Safarini Dodoma.

Mods naomba hii iwekwe juu tafadhali
cc Paw, Invisible

 
Mkuu MIMI Baba, sio kila anayeulizia chochote kuhusu Chadema, lazima ni CCM!. MIMI NIKO SOLO

Nakufahamu, nakuheshimu na nakushauri endelea hivyo ili mradi akili Mungu aliyokupa kwa hiari yake inatumika tofauti na wale akili zao zinavyotumiwa.
 
Chadema ni saccos ya wapiga dili! Mpaka misukule mje kustuka, watakuwa na majumba sio Dubai tu, bali mpaka ulimwenguni kote! Makamanda mpoo!
 
Tangu chama kilipoasisiwa hapajawahi kuwa na kipengere kinachoweka ukomo kwenye uongozi, lakini hiyo haikumfanya mzee Mtei kung'ang'ania uenyekiti wala mrithi wake mzee Makani. Sijui hofu yako inatoka wapi. Mimi nilidhani kwenye hoja za Mwigamba tungezama kwenye ukiukwaji wa kanuni za fedha na ufisadi mwingine wanaodaiwa kuufanya viongozi.
kwa hiyo mnataka kuwaambia watanzani kua nyie chadema mnafanya mambo yenu kwa "utashi" na "mazoea" wala si kwa kuwekeana mipaka, hakuna haki isiyo na mipaka, hata katiba inasema hivyo, kwa kufanya hivyo kifungu hicho kinakwenda kinyume na sheria mama ya nchi inayosema kua kila haki ina mipaka yake ili kuondoa matumizi mabovu ya hiyo haki kuwanyima wengine haki hiyo hiyo...ile kauli kwamba chadema ni saccos inaanza kujidhihirisha hapa..
 
Kwa hiyo, mwenyekiti na katibu wake ni wa milele? Haiwezekani wengine kuachiwa nafasi hizo?
Kwani huyo mwenyekiti anajichagua? Hakuna ukomo ila uchaguzi upo shida ninini? Nakuhakikishia kama JK angekuwa mwenyekiti wa Chadema na kwa utendaji wake, hata kama hakuna ukomo angeishia kipindi kimoja tuu.
 
Mkuu Only 83, utafiti hufanywa na watafiti, mimi sio mtafiti ni just a reporter kuripoti nilichoona, kuambiwa au kusoma. Tuhuma hizi nimezisoma humu jf, nimeuliza, wahusika mamejibu tena kwa ufasaha, bado Pasco ni tatizo?.
Pasco.
Genuine Bona fide
 
Kwani huyo mwenyekiti anajichagua? Hakuna ukomo ila uchaguzi upo shida ninini? Nakuhakikishia kama JK angekuwa mwenyekiti wa Chadema na kwa utendaji wake, hata kama hakuna ukomo angeishia kipindi kimoja tuu.

Misukule mnaamini kila kitu anachosema Paroko! Hamtaki kusikia kitu mbadala hata kidogo! Kaazi kwelikweli! Ngojeni wenzenu wapige hela nyie mnanyweshwa viroba na maandamano ya kutosha tu! Ha ha ha! Chezea chadema saccos wewe!
 
Hii post atakuwa ameandika Slaa mwenyewe sio Josephine Mushumbusi.

Post za Slaa utazijua tu jinsi zinavyojenga hoja.

Kweli kila mtu anafikiri kwa namna yake. Ila ulichoandika pengine kina ukweli japo sijawahi kuona bandiko la Huyo mwingine uliyemtaja , kama lipo naomba hata unitag niweze kuliona! Ila nimecheka sana sikutarajia ningekutana na comment ya namna hii.
 
Wassira amepata wasaidizi wengi sana na hiki kinachofanyika kinatokana na kauli yake kuwa CHADEMA KITAKUFA KABLA YA KUISHA 2013 sasa leo tunaingia Nov. chama bado kipo imara ndio maana wanazidi kuweweseka na mzee wa GOMBE ameumbuka
 
Nafasi ya Uenyekiti wa Chama mbona inawatoa watu jasho namna hii?Huku ni kuzunguka tu.....Hebu nendeni straight kwenye point.

Nadhani ikithibitika hivyo basi ofisi ya msajili nayo itabidi kuwajibika.Ni kwanini isemwe kipindi hiki na si wakati wowote?

Mkuu hapo kwenye red msajili atajibu yeye bado ni mgeni ofisini na issue haimhusu au umewasahau viongozi wetu?
 
Nafasi ya Uenyekiti wa Chama mbona inawatoa watu jasho namna hii?Huku ni kuzunguka tu.....Hebu nendeni straight kwenye point.

Nadhani ikithibitika hivyo basi ofisi ya msajili nayo itabidi kuwajibika.Ni kwanini isemwe kipindi hiki na si wakati wowote?

hebu pitia tena ulichoandika, ni aibu kwako kwa hoja dhaifu kama hii. Acha njaa fanya kazi
 
Pasco

Uko kwenye mlengo tata usiotimilika, tafsiri ya unachokiota ni kinyume chake

ishu ni huu utaratibu mpya wanaotaka kuanzisha chadema hapa Tanzania. Mfumo wa uwajibikaji sio mfumo mpya lakini utekelezaji wake unaonekana kuwa mpya miongoni mwa Watanzania, ndio maana imeanza kujengeka kuwa viongozi wa chadema wanaposimamia utekelezaji ama wa maadili kwa mujibu wa katiba ama wa kazi za kuimarisha chama, viongozi hawa huonekana kama wametengua na kupindisha katiba ya chama.

Niwatie nguvu wana CHADEMA na wana CCM (off course na vyama vingine na serikali pia) wanaoamini kwenye uwajibikaji, wasiache wala wasisite kusimamia uwajibikaji kwenye maeneo yao ya utendaji
 
Anaelalamika sana kumbe kaficha yake. Yakifichuka ni janga la radi mwituni. Sasa hili jambo ni zaidi ya yote. Uitishwe mkutano wa dharura, Chadema taifa isimamishe shughuli zote ili suala hili lishughulikiwe kisheria.
 
kwa hiyo mnataka kuwaambia watanzani kua nyie chadema mnafanya mambo yenu kwa "utashi" na "mazoea" wala si kwa kuwekeana mipaka, hakuna haki isiyo na mipaka, hata katiba inasema hivyo, kwa kufanya hivyo kifungu hicho kinakwenda kinyume na sheria mama ya nchi inayosema kua kila haki ina mipaka yake ili kuondoa matumizi mabovu ya hiyo haki kuwanyima wengine haki hiyo hiyo...ile kauli kwamba chadema ni saccos inaanza kujidhihirisha hapa..
Hofu yangu ni hiyo mipaka unayotaka wewe kugeuka kikwazo kwa demokrasia. Wacha waongoze kama ndio utashi wa wanachama ambao ndio wenye chama so long as hakuna anayezuiliwa kuwa-challenge. Huko kwenye chama chenu kiongozi anatakiwa awepo kwa muda gani?!
 
Pasco,

Ni nani atakayethibitisha kwamba katiba hii ni fake?

Maana katiba hii hii kabla haijawa katiba ilipitia kwa msajili, akaisoma akaipitisha.

Labda uniambie aliyeipitisha katiba ya CHADEMA akithibitika aliboronga apigwe risasi nitakuelewa.
CHADEMA kwa hili halina kosa. Kosa ni la aliyeipitisha kama kweli aliipitisha ikiwa hakina kipengele cha ukomo!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
WanaJF,

Pamoja na kuwa sitaki kuingilia mjadala katika hatua hii, naomba kuthibitisha kuwa:
I) Katibu Mkuu wa Chadema, kwa mujibu wa Katiba na Kanuni ya Chadema, ndiyo mhimili mkuu na mwenye jukumu la kutunza na kuhakikisha Katiba ya Chama inatunzwa.

2) Nataka kuwahakikishia wanachadema wote, kuwa nilikuwepo nimekuwa ndani ya Chadema kuanzia 1998 ambapo nilikuwa Makamu Mwenyekiti Bara, na baadaye 2003 Kaimu Katibu Mkuu, na hatimaye Katibu Mkuu. Hivyo nimeshiriki kikamilifu kuandaa Katiba ya 2004 na pia Katiba ya 2006 baada ya Rebranding ya Chama. Nataka niwahakikishie wanachadema, hakuna toleo lolote la Katiba ndani ya Chadema imeweka " muda wa Uongozi kuwa vipindi viwili tu", kuanzia Katiba aliyoiasisi Mzee Mtei na kupitishwa na Mkutano Mkuu, wala si ya 2004 au ya 2006. Kama kuna mtu anasema ilikuwepo na imeondolewa kinyemela, basi aonyeshe kifungu hicho kwenye Katiba yeyote ile, au miniti za kikao chochote kile.

3. Mimi Dr Slaa, ndiye niliyewasilisha Miniti za Mkutano Mkuu wa 2006 kwa Msajili ikiambatana na Katiba iliyopitishwa na Mkutano Mkuu. Tulichobishana Mimi na Msajili, na kwa maandishi, ni kuwa Msajili alit aka nimwasilishie nakala ya Katiba kwa Kiingereza. Nilimkatalia kwa msingi kuwa Katiba yetu ilipitishwa na Mkutano Mkuu kwa kiswahili na Mkutano Mkuu na hivyo siwezi Mimi kumpelekea kwa Kiingereza. Msajili alidai kuwa ni hitaji la kisheria. Nilimjibu kuwa sheria hiyo inapaswa kufanyiwa marekebisho. Hata hivyo, baadaye tulikubaliana kuwa nitengeneze " literal translation" lakini kwa mahitaji ya kisheria itatumika Katiba ya Kiswahili ambayo ndiyo iliyopitishwa na Mkutano Mkuu. Hivyo, ninathibitisha kuwa hakuna kipengele chochote kilichoingizwa kinyemela.

Wanachadema, wapenzi, na wananchi kwa ujumla, huo ndio ukweli. Kama mtu anadhani kuna utata aende kwa Msajili akague Katiba ya 1992, 2004 na 2006, nadhani utaratibu wa Msajili itaruhusu ukaguzi huo. Ndio njia pekee ya kuacha kabuni na kuwa watabiri kwa misingi ya waganga wa kienyeji. Tufanye kaki kisayansi, na tusiwatie hofu wananchi bila sababu.

Kama mtu Ana ajenda yake ya siri, huyo hatuwezi kumsaidia! Wananchi, tuna mambo ya muhimu zaidi kuliko hizi propaganda, tunahitaji kutumia muda wetu kwa mambo hayo, mathalan madai ya Katiba Mpya, kupigania maslahi ya Taifa na Watanzania hasa walala hoi ambao kila siku wanazidi kupigika, kupambana na manyanyaso Kama yaliyotokea Serengeti na Babati ambao wananchi wameteswa viajabu katika nchi inayojitangaza kuwa na utawala wa sheria nk.
Ufafanuzi mzuri sana
 
kumbe unalitambua ilo waambie magamba wenzako kuwa Dr. Slaa ni moto wa kuotea mbali na hata usipowaambia wanalijua hili.

Hii post atakuwa ameandika Slaa mwenyewe sio Josephine Mushumbusi.

Post za Slaa utazijua tu jinsi zinavyojenga hoja.
 
Back
Top Bottom