Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Mzee tulia leo wajukuu zako umri ushakutupa. Naona umejipa cheo cha msajili wa vyama vya siasa. Bure kabisa
Mkuu Kobe la Makobe , mimi ndio kwanza naelekea 60, ukoo wangu ni watu wa umri mrefu, kila siku nashinda kwa msajili na sijawahi kuiomba hiyo inventory, usinjtie hasira nikaamua kuitafuta na kuibadika humu...
P
 
  • Thanks
Reactions: 30P
Mkuu Kobe la Makobe , mimi ndio kwanza naelekea 60, ukoo wangu ni watu wa umri mrefu, kila siku nashinda kwa msajili na sijawahi kuiomba hiyo inventory, usiitie hasira nikaitafuta na kuibadika humu...
P

Kumbe mabandiko yako huwa hadi uchukizwe ama ugali uguswe.? Ndio maana mwendazake alikusanua tu kuwa weww ni njaa. [emoji3][emoji3]
 
Ukomo wa mwenyekiti chadema nishida Sasa imegeuka imekuwa rushwa, siku wakibadilisha mwenyekiti ndo wataona kumbe Mali zote hazina hati za majina ya chama anyway wanajua wenyewe
 
Wanabodi,

Uendeshaji wa vyama vya siasa nchini, unaongozwa na sheria, taratibu na kanuni. Ikithibitika pasipo shaka kuwa chama fulani, kinakiuka sheria, taratibu na kanuni, kinapaswa kuwajibishwa, kuadhibiwa hata kufutwa, kutegemeana na tuhuma halisi!.

Miongoni mwa masharti ya usajili wa vyama vya siasa, ni kwa vyama hivyo, kuwasilisha katiba yake iliyopitishwa kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, ikithibitika pasipo shaka kuwa katiba ya CHADEMA iliyowasilishwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni Katiba "Fake" na sio ile katiba halisi ilipitishwa na Vikao Halali vya CHADEMA!, hili ni kosa kubwa linaweza kupelekea chama kufutwa!.

Tuhuma yenyewe ni hii na ilitolewa rasmi jana humu JF na mwana JF huyu.


Mara baada ya mwaJF huyu kuzishusha tuhuma hizi humu, uongozi wa CHADEMA umemsimamisha mmoja wa viongozi wake kwa kosa la kuutoa ukweli huu nje.

Maswali ambayo ni lazima CHADEMA wayajibu ni haya.

  • Jee ni kweli CHADEMA inaendeshwa kwa katiba fake na sio ile iliyopitishwa na vikao halali?
  • Jee ni nani alikinyofoa kipengele cha demokrasia ya ukomo wa uongozi ndani ya chama ili kutoa nafasi kwa uongozi wa kifalme na kisultani?
  • Ikithibitika kuna mtu alikinyofoa kipengele hicho kwa makusudi, atachukuliwa hatua gani?
  • Je ni nani alichomekea kipengele cha kumzuia mwanachama wa Chadema kutafuta haki yake mahakamani?.
  • Je mabadiliko ya "unyofoaji huo" yaliwasilishwa kwa Msajili wa Vyama?
  • Ikithibitika pasipo shaka kuwa CHADEMA walikiuka sheria taratibu na kanuni, jee watafanywa nini? (Masajili)
Baada ya kushushwa tuhuma nzito kama hizi, dawa sio kumsimamisha uongozi mtoa tuhuma, bali kutoa majibu ya kina kuhusiana na tuhuma hizi.

Namna rahisi ya kuthibitisha ni kupatikana kwa miniti za kikao kilichopitisha kunyofoa kipengele hicho cha ukomo wa uongozi na kuchomekea kipengele cha kuzuia wanachama wa Chadema kutafuta haki yao, mahakamani!.
Kisha zipatikane miniti za kikao chochote halali kilichopitisha unyofoaji huo!.

Kisha kwenda kwa Msajili kuthibitisha kama mabadiliko hayo yalifanyika kihalali.

Naandika haya nikiwa ni mwananchi tuu wa kawaida ambaye ni mwanachama wa chama cha siasa, mwenye mamlaka kamili kuhoji jambo lolote kuhusu chama chochote, na sababu ni mimi pia ndiye ninayegharimia fedha za uendeshaji wa Chadema kupitia kodi yangu inayolipwa Chadema kama ruzuku!.

Pia naelewa fika kinachowakuta wakosoaji wowote wa chama "kitakatifu" humu jf, ila kwa vile hoja zangu ni za kweli, nasimama kwenye kweli, na ni ukweli tuu ndio utakao kiweka huru Chadema na sio timua timua au fukuza fukuza!.

Angalizo wa wapenzi wa Chadema, sijasema chama chenu kinafutwa, nimetoa angalizo tuu la tuhuma kwa chama chenu kuendeshwa kwa katiba feki!, tuhuma hizi zikithibitishwa, it's going to cost Chadema very dearly kwasababu Chadema hiyo katiba fake ya Chadema ya 2006 will be declared null and void, hivyo katiba ya Chadema kubaki ile ya 1992!.

Pasco.
Update 1. Majibu ya Katibu Mkuu wa Chadema.


Mkuu Dr. W. Slaa, kwanza, heshima yako!, maana ile kujibiwa tuu na mtu wa calibre yako pekee, ni heshima kwangu na kwa thread hii, hivyo majibu yako, nayaunganisha pale mbele ya thread as an authority.

Uwongo ukisemwa sana na kuachwa bila kukanushwa, hugeuka ukweli. Sambamba na tuhuma hii, mtoa tuhuma pia ameweka tuhuma nyingine nyingi, zenye kuhitaji majibu ya kina kama haya uliyonijibu hapa.

Kwa majibu hayo, na kwa vile wewe ndio mtendaji mkuu wa Chama, ni uthibitisho pia kumbe ulikuwa huijui katiba ya Chadema kuwa ina kipengele cha ukomo wa uongozi!, kama KM hajui kipengele muhimu kama hiki, who will know?.

Kwa vile CCM ndicho chama tawala, Chadema kiko kwenye mizani ya tukiaminie mwaka 2015 au bora kuendelea na CCM tuliyoizoea!, hivyo haya makando kando yoyote kuihusu Chadema, lazima yajibiwe ipasavyo kama hivi ulivyofanya hapa.

Asante sana kwa hili.

Kwa vile maelezo haya yako ni ya upande mmoja, nasubiri verification ya data toka kwa msajili, then niufunge rasmi huu mjadala.

Nashukuru tena.

Pasco.
Update 2: Majibu ya Msemaji Mkuu wa Chadema, Mhe. JJ.Mnyika.

Asante sana Mkuu JJ. Mnyika, nitajitahidi kutembelea kule ili kujiridhisha, ila kwa vile mzizi wa fitna kwenye uzi huu ni katiba ya 2004, kama unayo, nitashukuru tukiipata, tukaufunga huu mjadala rasmi.

Kama unachosema wewe ndio right, kuwa ile katiba ya 2006 sio marekebisho ya katiba ya 2004, bali ni katiba mpya, hata kama ni kweli, katiba ya 2004 ilikuwa na kipengele tajwa, na katiba ya 2006 ikawa haina, then at this juncture,

Nkuwekea uthibitisho wa Katiba ya Chadema ya 2006, sio katiba mpya bali ni marekebisho ya katiba ya 2004 kama inavyoeleza katiba yenyewe
"HIVYO BASI,
Sisi wajumbe wa Mkutano Mkuu uliofanyika tarehe 13/8/2006, Mjini Dar es Salaam tumeamua kuifanyia mabadiliko Katiba ya 2004 ya Chama chetu cha Siasa kinachoitwa CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO ili kuipa sura inayoendana na mtazamo na msukumo mpya wa FALSAFA yetu ya NGUVU NA MAMLAKA YA UMMA na Dira na Dhamira ya Chama kuanzia 2006 na kuendelea. Kuanzia sasa CHADEMA, kitaendeshwa kwa mujibu wa Katiba hii".

I put my hands down, mjadala umesitishwa kwa sababu wenye chama wanasema katiba ya 2006 katiba ni mpya, na kwa vile katiba yenyewe imeandikwa kufanyiwa mabadiliko, lakini haijasemwa popote kuwa ni katiba mpya, then its not ok kama haina kipengele hicho na hakuna any munutes, kipengele hicho, kilinyofokaje?.

Kipengele chenyewe ni hiki
View attachment 2845553



View attachment 233612View attachment 233613

Pasco.
Update 3 Final Update- Majibu ya Tundu Lissu, atoa siri ya jinsi kipengele hicho kilivyo yeyuka au kuyeyushwa Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA
Kitu kilichobakia kuufunga rasmi huu mjadala, ni kwa mimi kupita Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa nchini, kukagua inventory ya Msajili wa vyama kuona hicho kilichofanyika mwaka 2006 kwa Chadema ni waliwasilisha katiba mpya ya Chadema, au waliwasilisha mabadiliko ya katiba?.
Paskali
Taarifa ya leo ya TL inathibitisha hoja za bandiko hili, hawa jamaa walikinyofoa kipengele hicho kinyemela wakakabidhi katiba fake kwa msajili, hivyo katiba ya
Chadema iliyopo ofisi
Msajilia way vyama ni fake!.

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu wakati akitangaza nia ya kugombea Uenyekiti wa CHADEMA Taifa amesema CHADEMA haina budi kurudisha utaratibu wa ukomo wa Madaraka kwani utaondoa uwezekano wa Viongozi kung'angania madaraka na kuandaa Viongozi wapya, kupatikana kwa mawazo mapya na itapunguza upambe na uchawa ulioshamiri pale kiongozi anang'ang'ania madaraka pale ambapo hakuna ukomo wa madaraka
Afadhali leo ndio TL amelizungumzia hili, anashangiliwa, kama hakuna ukomo, then hakuna kung'ang'ania madaraka,hili neno kung'ang'ania madaraka ni kumsema mtu kwa mlango wa nyuma!。

Msikilize TL hapa Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA

Siku nilipoibua hii issue ya ukomo wa madaraka, KM wa wakati huo, Dr Slaa, aliruka kimanga na kuniparua Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Haya sasa leo TL kayasema, nasubiria kama ataparuliwa!。
P
 
WanaJF,

Pamoja na kuwa sitaki kuingilia mjadala katika hatua hii, naomba kuthibitisha kuwa:
I) Katibu Mkuu wa Chadema, kwa mujibu wa Katiba na Kanuni ya Chadema, ndiyo mhimili mkuu na mwenye jukumu la kutunza na kuhakikisha Katiba ya Chama inatunzwa.

2) Nataka kuwahakikishia wanachadema wote, kuwa nilikuwepo nimekuwa ndani ya Chadema kuanzia 1998 ambapo nilikuwa Makamu Mwenyekiti Bara, na baadaye 2003 Kaimu Katibu Mkuu, na hatimaye Katibu Mkuu. Hivyo nimeshiriki kikamilifu kuandaa Katiba ya 2004 na pia Katiba ya 2006 baada ya Rebranding ya Chama. Nataka niwahakikishie wanachadema, hakuna toleo lolote la Katiba ndani ya Chadema imeweka " muda wa Uongozi kuwa vipindi viwili tu", kuanzia Katiba aliyoiasisi Mzee Mtei na kupitishwa na Mkutano Mkuu, wala si ya 2004 au ya 2006. Kama kuna mtu anasema ilikuwepo na imeondolewa kinyemela, basi aonyeshe kifungu hicho kwenye Katiba yeyote ile, au miniti za kikao chochote kile.

3. Mimi Dr Slaa, ndiye niliyewasilisha Miniti za Mkutano Mkuu wa 2006 kwa Msajili ikiambatana na Katiba iliyopitishwa na Mkutano Mkuu. Tulichobishana Mimi na Msajili, na kwa maandishi, ni kuwa Msajili alit aka nimwasilishie nakala ya Katiba kwa Kiingereza. Nilimkatalia kwa msingi kuwa Katiba yetu ilipitishwa na Mkutano Mkuu kwa kiswahili na Mkutano Mkuu na hivyo siwezi Mimi kumpelekea kwa Kiingereza. Msajili alidai kuwa ni hitaji la kisheria. Nilimjibu kuwa sheria hiyo inapaswa kufanyiwa marekebisho. Hata hivyo, baadaye tulikubaliana kuwa nitengeneze " literal translation" lakini kwa mahitaji ya kisheria itatumika Katiba ya Kiswahili ambayo ndiyo iliyopitishwa na Mkutano Mkuu. Hivyo, ninathibitisha kuwa hakuna kipengele chochote kilichoingizwa kinyemela.

Wanachadema, wapenzi, na wananchi kwa ujumla, huo ndio ukweli. Kama mtu anadhani kuna utata aende kwa Msajili akague Katiba ya 1992, 2004 na 2006, nadhani utaratibu wa Msajili itaruhusu ukaguzi huo. Ndio njia pekee ya kuacha kabuni na kuwa watabiri kwa misingi ya waganga wa kienyeji. Tufanye kaki kisayansi, na tusiwatie hofu wananchi bila sababu.

Kama mtu Ana ajenda yake ya siri, huyo hatuwezi kumsaidia! Wananchi, tuna mambo ya muhimu zaidi kuliko hizi propaganda, tunahitaji kutumia muda wetu kwa mambo hayo, mathalan madai ya Katiba Mpya, kupigania maslahi ya Taifa na Watanzania hasa walala hoi ambao kila siku wanazidi kupigika, kupambana na manyanyaso Kama yaliyotokea Serengeti na Babati ambao wananchi wameteswa viajabu katika nchi inayojitangaza kuwa na utawala wa sheria nk.
Mkuu Dr. Slaa, msikie huyu

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu wakati akitangaza nia ya kugombea Uenyekiti wa CHADEMA Taifa amesema CHADEMA haina budi kurudisha utaratibu wa ukomo wa Madaraka kwani utaondoa uwezekano wa Viongozi kung'angania madaraka na kuandaa Viongozi wapya, kupatikana kwa mawazo mapya na itapunguza upambe na uchawa ulioshamiri pale kiongozi anang'ang'ania madaraka pale ambapo hakuna ukomo wa madaraka
Afadhali leo ndio TL amelizungumzia hili, anashangiliwa, kama hakuna ukomo, then hakuna kung'ang'ania madaraka,hili neno kung'ang'ania madaraka ni kumsema mtu kwa mlango wa nyuma!。

Msikilize TL hapa Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA

Siku nilipoibua hii issue ya ukomo wa madaraka, KM wa wakati huo, Dr Slaa, aliruka kimanga na kuniparua Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Haya sasa leo TL kayasema, nasubiria kama ataparuliwa!。
P
 
Pasco nimesoma mjadala ulioanzisha na majibu ya Dr Slaa. Suala la kwamba kuna kipengele kiliondolewa kinyemela halina ukweli, na kilichofanyika 2006 ni kuandika katiba upya Mjadala mwema. JJ
Mkuu John Mnyika, hili jambo leo TL amelisema, huu ni uthibitisho hili jambo mlilijadili, kwa siri bila kuandika minutes, mkaamua kukiondoa kipengele hicho kinyemela bila kuandika popote, kisha mkaibuka na katiba mpya ya 2006 bila kipengele hicho, hivyo ni kinyemela.

Utaratibu wa utungaji wa katiba mpya, vitu vyote vilivyopo kwenye katiba ya awali ni lazima vijadiliwe, ama viboreshwe ama viondolewe, lakini kipengele hicho hakikujadiliwa popote, hakuna minutes zozote, kumbmlilijadili kwa siri, mkakiondoa kwa siri, kimya kimya, kinyemela.
Hivyo I was dam right

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu wakati akitangaza nia ya kugombea Uenyekiti wa CHADEMA Taifa amesema CHADEMA haina budi kurudisha utaratibu wa ukomo wa Madaraka kwani utaondoa uwezekano wa Viongozi kung'angania madaraka na kuandaa Viongozi wapya, kupatikana kwa mawazo mapya na itapunguza upambe na uchawa ulioshamiri pale kiongozi anang'ang'ania madaraka pale ambapo hakuna ukomo wa madaraka
Afadhali leo ndio TL amelizungumzia hili, anashangiliwa, kama hakuna ukomo, then hakuna kung'ang'ania madaraka,hili neno kung'ang'ania madaraka ni kumsema mtu kwa mlango wa nyuma!。

Msikilize TL hapa Tundu Lissu kama JPM, ni mtu mkweli. Asema ukweli jinsi ukomo wa uongozi ulivyoyeyuka CHADEMA

Siku nilipoibua hii issue ya ukomo wa madaraka, KM wa wakati huo, Dr Slaa, aliruka kimanga na kuniparua Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Haya sasa leo TL kayasema, nasubiria kama ataparuliwa!。
P
 
Wanabodi,

Uendeshaji wa vyama vya siasa nchini, unaongozwa na sheria, taratibu na kanuni. Ikithibitika pasipo shaka kuwa chama fulani, kinakiuka sheria, taratibu na kanuni, kinapaswa kuwajibishwa, kuadhibiwa hata kufutwa, kutegemeana na tuhuma halisi!.


Kitu kilichobakia kuufunga rasmi huu mjadala, ni kwa mimi kupita Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa nchini, kukagua inventory ya Msajili wa vyama kuona hicho kilichofanyika mwaka 2006 kwa Chadema ni waliwasilisha katiba mpya ya Chadema, au waliwasilisha mabadiliko ya katiba?.
Paskali
Kama mwanadiplomasia na mwanasiasa mwandamizi nchini, nimeifuatilia chadema kwa karibu sana na kwa muda mrefu, na nimethibitisha pasina shaka na kujiridhisha kwamba, chadema inakiuka sheria na masharti ya usajili wake, na kwahivyo inastahili kufutwa rasmi kisheria.
Mkuu Tilatila, Tlaatlaah , kwanza Naunga mkono hoja, mimi hili nilishauri siku nyingi toka kitambo sana, Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa

Walipotoa ile movie ya ile video ya Rwakatare, niliandika , Ikithibitika CHADEMA ilihusika na uvunjifu wa amani, then inapaswa kufutwa kwa mujibu wa katiba!, tena sikuishia kwa Chadema tuu, nilishauri vyama vingine vyote vifutwe, tuwe nchi ya chama kimoja, na CCM itawale milele! The Economist: Rais Magufuli ametangaza kufuta Upinzani ifikapo 2020 na kuirudisha Tanzania kuwa Nchi ya chama Kimoja

Na nikawasisitiza Watanzania Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.

Na kuna bandiko humu nilitoa ushauri wangu huu
Kiukweli mimi Pasco wa jf, kwa kauli moja, naunga mkono hoja, kuwa CCM ndio pekee iruhusiwe kusimamisha mgombea urais wa Zanzibar, tena sio tuu CCM ndio pekee wagombee urais Zanzibar, bali CCM ndio pekee wagombee urais wa JMT, kwa sababu CCM ndicho chama pekee chenye hati miliki ya urais wa JMT na Zanzibar kiliopewa na Mungu!, hii ni kufuatia long euksipiriensi ya uzoefu wa muda mrefu kwenye urais!.
CCM Oyeee...!.

Pasco
P
 
Back
Top Bottom