Pre GE2025 Huenda huu ukawa ndio mwanzo wa mwisho wa Siasa za Peter Msigwa

Pre GE2025 Huenda huu ukawa ndio mwanzo wa mwisho wa Siasa za Peter Msigwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Inawezekana kuwa ndio mwisho wa CHADEMA kama chama cha kwanza cha upinzani kama Msigwa atafukuzwa chama. Sidhani kama hili watalifanya, kwa vile CHADEMA inaelewa kuwa Msigwa ni JEMBE.
Huwezi kushindana na taasisi yoyote ukaishinda.
Unachoweza ni kuiacha taasisi au ukubaliane nayo.
Hakuna mtu mkubwa kuliko taasisi.
 
Mchungaji Msigwa kubali yaishe. Ubunge wa Iringa Mjini 2025 ni wako kupitia CHADEMA. Wasikudanganye ule upande mwingine kwa kukuhaidi kuwa Mkuu wa Wilaya.
 
CCM Kuna njia nyingi ambazo Msigwa anaweza kupita na kuwa mbunge. Mojawapo ni zile nafasi 10 za mwenyekiti wa ccm taifa a.k.a rais wa JMT. Kama Mbowe anazingua,. Msigwa ahame aingie ccm ambako atateuliwa kuwa mbunge Kisha waziri wa katiba na sheria na ndipo ataifuta chadema kupitia msajii wa vyama vya siasa.
 
Pamoja na yote yanayo semwa juu ya CHADEMA bado Peter Msigwa ni mnufaika kinara wa CHADEMA Jimbo la Iringa ( T )

Huenda Mch Peter Msingwa ndio mwanasiasa toka Upinzani atakayetangazwa mapema zaidi katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Oct 2025.

Duru za siasa za Upinzani zinamtaja Peter Msigwa kuwa ndio mwanasiasa anayependwa zaidi Ukanda wa Nyanda za juu kusini.

Ni Msingwa pekee mwenye nafasi ya kushinda Ubunge kwa zaidi ya 77% tofauti na ilivyo kwa Mpinzani wake wa karibu Joseph Mbilinyi.

Ukweli mchungu ni kwamba huenda Dkt Tulia Ackson akatetea Jimbo lake la Mbeya Mjini kwani Joseph Mbilinyi Sugu anapewa uwezekano mdogo wa kuibuka mshindi.

Turufu pekee ya Joseph Mbilinyi ni Jimbo la Mbeya Mjini kugawanywa kutokana na Ukubwa na wingi wa watu waliopo katika Jimbo hilo.

Si rahisi Mch Peter Msigwa kuwa Mbunge wa Iringa mjini kupitia CCM kwani muda uliosalia ni mfupi na Iringa ni ya Upinzani.

Siasa za sasa za Chama Cha Mapinduzi CCM ya Mama Samia ni mwendo wa demokrasia tu.

Mwanachama wa CCM akishinda kura za maoni ameshinda and verse versa is also true ila tu kama ni u-DC huo ataupata tu.

Ifahamike kuwa Probability ya Mch Peter Msigwa kushindwa kurudi bunge akiwa CCM ni moja ( 1 ) yaani ni hakika hatorudi.

Pamoja na mambo mengi yanayoizonga CHADEMA bado ndio Chama sahihi kwa sasa kwa Msigwa kupambania future yake.

Hata hivyo wajumbe kadhaa wa Kamati kuu ya CHADEMA nilipojaribu kuteta nao kwa nyakati tofauti tofauti.

Wengi wao wameonesha wazi hawajaridhishwa na Uchaguzi wa Kanda ya. Nyasa na hivyo ni muhimu Ukarudiwa.​
Mchungaji kaza haiwezekani Mtu aongoze taasisi miaka 30
 
Huwezi kushindana na taasisi yoyote ukaishinda.
Unachoweza ni kuiacha taasisi au ukubaliane nayo.
Hakuna mtu mkubwa kuliko taasisi.
Siongelei mtu,nami si mwanachama wa chama chochote.
Lakini ni ngumu mtu kuishinda taasisi aliyomo.
Iwe Kanisa,Chama cha Siasa,Kampuni etc.
Anachoweza ni kukaa kando au kukubaliana nayo.
Mmmmmm! KANU kama taasisi ilipotea baada ya Majembe kujitoa. CUF vile vile, NCCR Mageuzi nayo ilipitia njia hiyo hiyo. The next ni ANC, Kuondoka kwa Zuma ni janga kwa ANC. The Zuma efect imeipunguzia ANC 15% ya kura.
Pengine hujui nguvu ya Msigwa katika mikoa ya Iringa, Njombe na Mbeya. Kwa mtafaruku huu tu, Sugu anajua kuwa hana ubunge Mbeya lakini Msigwa ana uhakika wa 100% ya kurudi bungeni. Yahifadhi maneno yangu.
 
Wakuu Mfumo demokrasia ni nzuri kwa wanasiasa inapowapa nafasi lakini ikiwakataa wanaikana.

Miaka kumi ya msigwa kanda ilitosha kwa msigwa kufanya mabadiliko ya muda wa madaraka ya chama.

Sasa bahati mbaya mwenzake kamshinda na hajui lini ataaachia madaraka maana hakuna ukomo huko Chadema.

Na Mbowe alivomjanja anaweza kuruhusu marudio na ukashindwa pia.
 
Back
Top Bottom